Soka letu vs wachambuzi (washabiki) wetu

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Juzi kati kwa maana ya jumapili timu zetu mbili za Simba na Singida BS zilituwakilisha kwenye mashindano ya CAF.

Simba ikafuzu kwa goli la kanuni ila Singida BS ikatolewa kwa kufungwa 4.

Sasa, kazi ikawa kwa hawa wanaojiita wachambuzi ambao mie nadhani ni washabiki tu pale E Fm radio kwa siku mbili yaani jumatatu na jumanne katika kipindi chao cha michezo cha asubuhi wamejikita kujadili maoni ya mashabiki wa Simba wa mtandaoni.

Habari ya kutolewa Singida BG ikawa na nafasi kidogo mno tena siku moja tu ya j3.

Sasa leo Yanga kafungwa na Ihefu goli 2-1, kesho habari kubwa itakuwa kwa nini Yanga imefungwa na si kujadili mbinu walizotumia Ihefu kupata ushindi huu.

Pale E Fm mtu ninayemkubali ni Jemedari Saidi na kidogo Jeff Lea na Masoud, wale wengine si wachambuzi ni mashabiki tu kama si wachafuzi wa soka letu.
 
Hao ni Wachafuzi wa Mpira hawana lolote kwenye UCHAMBUZI maaana wako kwenye Payroll ya Jiesm mithili ya Kitenge na DP WORLD. Wako radhi wasifie hadi Jinsi Hesi anavyokunya
 
Juzi kati kwa maana ya jumapili timu zetu mbili za Simba na Singida BS zilituwakilisha kwenye mashindano ya CAF.
Simba ikafuzu kwa goli la kanuni ila Singida BS ikatolewa kwa kufungwa 4.
Sasa, kazi ikawa kwa hawa wanaojiita wachambuzi ambao mie nadhani ni washabiki tu pale E Fm radio kwa siku mbili yaani jumatatu na jumanne katika kipindi chao cha michezo cha asubuhi wamejikita kujadili maoni ya mashabiki wa Simba wa mtandaoni.
Habari ya kutolewa Singida BG ikawa na nafasi kidogo mno tena siku moja tu ya j3.
Sasa leo Yanga kafungwa na Ihefu goli 2-1, kesho habari kubwa itakuwa kwa nini Yanga imefungwa na si kujadili mbinu walizotumia Ihefu kupata ushindi huu.
Pale E Fm mtu ninayemkubali ni Jemedari Saidi na kidogo Jeff Lea na Masoud, wale wengine si wachambuzi ni mashabiki tu kama si wachafuzi wa soka letu.
Hivi watu wote hao kwenye kipindi kimoja huwa wanalipwa ?
 
Soka la bongo lina Mambo ya hovyo Sana,ajabu ya leo Baada ya mechi ya Ihefu na Yanga kuisha wachezaji walimfuata refa kumzonga kwamba amemaliza mechi kabala ya muda kuisha ikabidi refa awaonyeshe saa,lile tukio Ni la ajabu inaonekana refa anawaogopa wachezaji wa Yanga Hadi kuwaonyesha saa yake.....sijawahi kuona popote duniani Tangu nianze kuangalia boli.
Hizi timu za Kariakoo Zina nguvu kubwa Sana na mashabiki wapo sehemu mbali mbali hata hao wachambuzi wa mchele, watangazaji na wengine wengi ambao wapo kwenye vyombo vya soka,wanashindwa kuvumilia na kuonyesha mapenzi wazi wazi.
 
Hivi watu wote hao kwenye kipindi kimoja huwa wanalipwa ?
Nadhani ni 'betting' ndo inasababisha yote haya. Matokeo yakiwa sivo na walivobeti basi wataanza kuchokonoa kwenye mitando wenzao wanamaoni gani.
 
Back
Top Bottom