DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Wakati Barani Ulaya inajulikana wazi kuwa mchezo wa soka (Football) ndio namba moja kwa kupendwa na kufuatiliwa zaidi na Watu, Nchini Finland hali ni tofauti, wao mchezo wao namba moja ni ice hockey.
Mchezo huo unaongoza kwa umaarufu na kwa kufatiliwa na watu wengi Finland, hii inajumlisha wanaofuatilia kupitia TV na wanaofika uwanjani.
Finland ilitwaa ubingwa wa Dunia wa IIHF World Championship Mwaka 2022, 2019, 2011 na 1995, pia mpinzani wa jadi wa Finland ni Sweden, licha ya kuwa mara kadhaa wamekuwa na ushindani na Canada na Marekani.
Timu ya Taifa ya ice hockey inayojulikana kwa jina la "Leijonat" (The Lions) ni moja ya timu kubwa 6 "Big Six" za mchezo huo Duniani, nyingine ni Canada, Czechia, Urusi, Sweden na Marekani.
Chama cha Ice Hockey kimewekeza fedha nyingi kwa vijana wadogo kujifunza mchezo huo, pia timu ya Wanawake inashika nafasi ya 3 kwa ubora Duniani katika Takwimu za IIHF