John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Desemba mwishoni mwaka jana, Klabu ya Yanga ilimtambulisha kipa Abdultwalib Hamidu Mshery kuwa imemsajili kutoka Mtibwa Sugar kuwa mchezaji wao.
Mshery akaingia na kufanikiwa kufanya kweli, lakini Mtibwa Sugar kupitia Ofisa Habari, Thobias Kifaru anaibuka na kudai kuwa Yanga hawajakamilisha mchakato wa makubaliano yao.
Inavyoonekana kuna mpunga ambao Yanga hawajamalizia kwa Mtibwa, timu hizo zilikuwa na makubaliano yao ya siri ndiyo maana Mshery akaendelea kucheza kama kawaida.
Sasa hoja ya Mtibwa kulalamika kwenye media kuwa Yanga hawajakamilisha makubaliano yao, hoja kubwa ni moja kama documents zipo si wafuate sheria tu na siyo kwenda kwenye vyombo vya habari kulalamika.
Na kama Mtibwa walitumia ‘uungwana’ wa kuwaamini Yanga kisha biashara ikafanyika 'kishkaji' basi hilo ni kosa lao na inatakiwa kuwa funzo kwao na kwa klabu nyingine zote kuwa soka sasa ni biashara hakuna ile biashara ya kishkaji.