Soka: Ulaya dhidi ya Afrika

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Oi oi oi,

Wakuu leo nataka kufahamu kwanini Ulaya wanacheza mpira mzuri sana? Naangalia memchinya ARS na MUN, wanacheza vizuri sana bila kuvunja sheria za mpira.

Kulikoni huku kwetu watu wanacheza mpira kama wanacheza singeli na bado wanasifiwa wanajua kucheza?

Tunakwama wapi Afrika, namba kujua?
 
Wabongo tunajua kutikisika kama mayele tu.Ila mayele nae anajitahidi sana yule dogo

Mimi sioni kitu pale afrika wanatakiwa kukaza buti na kuacha majungu kama simba kila kukicha ugomvi nasikia mpaka wanatka kuuwana huko kwa uchawi

Kila mtu anamshika mwezie uchawi
 
Mimi sioni kitu pale afrika wanatakiwa kukaza buti na kuacha majungu kama simba kila kukicha ugomvi nasikia mpaka wanatka kuuwana huko kwa uchawi

Kila mtu anamshika mwezie uchawi
Waache wauane kwan tuna hasara gani
 
Bro wale wameshapiga hatua wako mbali sana,kule boli inatembea kweli kweli.

Kuna wakati unatizama game za ligi kuu unashindwa kutofautisha na mechi za vijana wa secondary hovyo kabisa.
 
Wenzetu wanacheza Soccer, sie tunacheza Kabumbu...

Huku ukiwa na pumzi na maguvu, tayari, ushakuwa mchezaji.

Sijawahi ona wenzetu wakipigana bambi(kibuyu) tangia nizaliwe.
 
kiongozi unakufuru kufananisha mpira wa ulaya na mateke ya bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…