Utatajirika bila biashara uliyowekeza kufanya vizuri? Faida kwenye hisa (i) Mgawo wa faida (dividend) (ii) Kuongezeka kwa thamani ya hisa (increase in intrinsic value) kwa kuangalia ufanisi wa mbeleni
Mkuu Ndachuwa, kweli Watanzania ni masikini sana wa mawazo, ndio maana kila uchao, wazungu wanakuja kujivunia mihela na kuhamishia kwao!.
Hebe angalia, juzi nilikuwa Bahi, kuna Mgogo fulani alikuwa na ngombe 800 wake 4 akiishi nyumba ya tembe!, ana watoto lukiki, kazi yao ni kuchunga ng'ombe!. Sasa ameshauriwa kuuza ngombe 600, amejenga nyumba 4 za kisasa kwa kila mke, amenunua magari 4 ya kisasa kwa kila nyumba, yeye naye ana gari lake, ana trekta, ameajiri wafanyakazi, sasa watoto wanakwenda shule kwa magari!.
Mtu kama huyu angapatiwa alimu ya hisa, akawekeza kwenye hisa, saa anakaa miguu juu, anakula tuu gawio!.
Ziko familia chache za wabongo, wao walifunguka macho zamani, wakanunua hisa kwenye IPO, leo watoto wao na watoto wa watoto wao, tangu wanazaliwa, mpaka watakapo kwenda kaburini, tayari, ni matajiri wa kutupa, hawahitaji kufanya kazi to earn a living, wanaweza kuishi maisha ya raha mustarehe huku wakitumbua maraha bila kufilisika!, ila pia ndio kwanza, wanaendelea kumiliki hisa na hilo gawio wanalitumia kuendelea kununua hisa!.
Kama sisi maskini hatutaungana kumiliki uchumi wetu, amini asiamini, watoto wetu, na watoto wa watoto wetu, wataishia kuwa wapangaji milele ndani ya nchi yao!. Wenye nacho, wanaongezewa!, wasio nacho, wananyanganywa hicho kidogo walichonacho na kuongezwa kwa wenye nacho!.
DSE sasa, ndio imetupa fursa akini sisi nasi tuingie kwenye kundi la wenye nacho, kwa sisi masikini kichangia hivi hivi katika umasikini wetu, tuwezeshane, tuweze!.
Pasco.