Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Mkuu Ndachuwa, kwanza pole kwa hizo za TOL, ni kweli zilikuwa kimeo, ila mwaka huu gawio la kwanza litatoka!.
Pia nakiri gawio la hisa za CRDB ni dogo!, angalia hisa za TCC au TBL, watu wanavuna mahela!.
Ili uweze kufaidika na gawio la hisa, lazima hisa hizo ziwe nyingi!.

Wabongo na hisa safari bado ni ndefu!, mimi kuna wakati nilivuta vungu fulani la maana mahali fulani, nikaamua niweke kwenye FD nile gawio!, bongo shinda haziishi, within no time, nikapata shida inahitaji fedha, nikaitumia ile FD yangu kukopa beki ile ile, interest ya mkopo ni 20%pa, interest ya FD, ni 12.5% mwisho wa siku, nikajukuta nimefanya biashara kichaa!, unawekeza kupata 12.5%, unakopa kulipa 20%!.

Najipanga kuilist PPR, tutafute mtaji tukue!.
P.

naomba msaada wako benk gan inatoa fd ya 12.5% na kwa mudagani.
 
Amesema jinsi ya kampuni kujiunga na soko hilo la EGM, wamelegeza masharti ya kujiunga, ambapo hapo zamani, ili kampuni isajiliwe, ilipaswa kwanza iwe imefanya biashara kwa zaidi ya miaka 5!, pili lazima kampuni ionyeshe kuwa imekuwa ikitengeneza faida.

Kujiunga na EGM hakuna sharti la muda, au kutengeneza faida, yaani kampuni unaweza kuianzisha leo, na leo leo ukaisajili soko la hisa la Dar es Salaam, na kuuza hisa, unapata mtaji, unafanya biashara!. Hivyo lile sharti la kuonyesha faida au la kuwa lazima kwanza uwe ulifanya biashara halipo!.

Yaani uinaanzisha biashara leo, unajisajili DSE leo, unauza shares leo, unapata mtaji leo, ndipo unaanza biashara kesho!.

Asante kiongozi kwa taarifa...Ila hata mimi huwa nashangaa hawa watu wa DSE hawatoi elimu mara kwa mara.

Unajua sisi wabongo hatuna utaratibu wa kuulizia au kusoma au kutafuta habari juu ya jambo fulani, hivyo hawana budi kutuamsha kwa kutupa taarifa kama hivi, mimi nitaifuatilia hii kitu maana nina kampuni ila mtaji umekuwa mgumu naamini itawasaidia watanzania wengi.

Thanks kaka
 
Pasco alichuzungumzia mkurugenzi wa DSE ni kitu ambacho kipo UK, baada ya wao kuona uhitajikaji wa mitaji kwa wajasilimali wadogo ambao hawawezi kukidhi mahitaji ya kujisajili katika soko la shea la London, basi walianzisha chombo kiitwacho Alternative Investment Market (maarufu kama London AIM) Lengo kubwa la AIM ilikuwa ni kupunguza vikwanzo ambavyo vipo kwenye London Stock Exchange.

Lakini waliweka sheria ambayo ni lazima kuwe kuna chombo ambacho kinachukua dhamana ya kuchunguza (due diligence) hawa wajasilimali kabla hawaja ruhusiwa kujisajili na AIM, Hawa ndio huitwa nominated adviser (NOMAD. Hawa ni investment bank kama walivyo kina Marry Lynch, Goldman Sachs au JP Morgan.

Risk associated with this kind of Investment:
Lazima tukubali kwamba kuna risk kubwa sana kuwekeza kwa wafanya biashara ambao hawaja jiestablish. Na hapa lazima kuwepo na watu wenye ufahamu wa finance kwa hali ya juu.
 
Amesema jinsi ya kampuni kujiunga na soko hilo la EGM, wamelegeza masharti ya kujiunga, ambapo hapo zamani, ili kampuni isajiliwe, ilipaswa kwanza iwe imefanya biashara kwa zaidi ya miaka 5!, pili lazima kampuni ionyeshe kuwa imekuwa ikitengeneza faida.

Kujiunga na EGM hakuna sharti la muda, au kutengeneza faida, yaani kampuni unaweza kuianzisha leo, na leo leo ukaisajili soko la hisa la Dar es Salaam, na kuuza hisa, unapata mtaji, unafanya biashara!. Hivyo lile sharti la kuonyesha faida au la kuwa lazima kwanza uwe ulifanya biashara halipo!.

Yaani uinaanzisha biashara leo, unajisajili DSE leo, unauza shares leo, unapata mtaji leo, ndipo unaanza biashara kesho!.

nimeupenda sana huu mfumo, hakika wengi sasa watafanikiwa kuwa waekezaji lakini naamini kwamba tayari kuna mfumo mzuri wa uendeshaji ili wana hisa wasipoteze wanachowekeza.
 
Pasco alichuzungumzia mkurugenzi wa DSE ni kitu ambacho kipo UK, baada ya wao kuona uhitajikaji wa mitaji kwa wajasilimali wadogo ambao hawawezi kukidhi mahitaji ya kujisajili katika soko la shea la London, basi walianzisha chombo kiitwacho Alternative Investment Market (maarufu kama London AIM) Lengo kubwa la AIM ilikuwa ni kupunguza vikwanzo ambavyo vipo kwenye London Stock Exchange. Lakini waliweka sheria ambayo ni lazima kuwe kuna chombo ambacho kinachukua dhamana ya kuchunguza (due diligence) hawa wajasilimali kabla hawaja ruhusiwa kujisajili na AIM, Hawa ndio huitwa nominated adviser (NOMAD. Hawa ni investment bank kama walivyo kina Marry Lynch, Goldman Sachs au JP Morgan.

Risk associated with this kind of Investment:
Lazima tukubali kwamba kuna risk kubwa sana kuwekeza kwa wafanya biashara ambao hawaja jiestablish. Na hapa lazima kuwepo na watu wenye ufahamu wa finance kwa hali ya juu.
Mkuu Mtanganyika, sasa hapa ndipo watu kama nyinyi wenye exposure mnatakiwa kuisaidia nchi, lazima nikiri, kwenye biashara za kimataifa au biashara za uchumi mkubwa, Watanzania bado tuko nyuma sana. Kuna maswali mengi najiuliza kuhusu hii due diligence, kama ilifanyika kweli, TOL na Niko watu wasingeingizwa chaka!. Niliwahi kuuliza kwenye soko kuu, kwa nini brokers ni sita tuu?, bado sijapata jibu hivyo Mr. DSE akiripoti, nitaliuliza hili.

CMSA waliotoa nafasi za nomads, the response was very poor kwa Watanzania, bado sijajua situation as is now, ila nafuatilia kwa karibu.

Please tusaidie if we can learn anything from AIM ili tuisaidie EGM yetu!.
Pasco.
 
Mkuu Mtanganyika, sasa hapa ndipo watu kama nyinyi wenye exposure mnatakiwa kuisaidia nchi, lazima nikiri, kwenye biashara za kimataifa au biashara za uchumi mkubwa, Watanzania bado tuko nyuma sana. Kuna maswali mengi najiuliza kuhusu hii due diligence, kama ilifanyika kweli, TOL na Niko watu wasingeingizwa chaka!. Niliwahi kuuliza kwenye soko kuu, kwa nini brokers ni sita tuu?, bado sijapata jibu hivyo Mr. DSE akiripoti, nitaliuliza hili.

CMSA waliotoa nafasi za nomads, the response was very poor kwa Watanzania, bado sijajua situation as is now, ila nafuatilia kwa karibu.

Please tusaidie if we can learn anything from AIM ili tuisaidie EGM yetu!.
Pasco.

Mkuu kwanza nataka kusema hivi bureaucratic ambayo iko DSE ndio inachosha watanzania wengi wenye experience na mambo haya. Due Diligence process sio kitendo cha ubabaishaji, kwa kampuni kuna mambo lazima uangalie, kwanza Financial Statements ambazo ziko audited na credible financial firms na wametoa clean opinions.

Kama kampuni ni uzalishaji lazima uchunguze process zake za uzalishaji, management need to disclose mapato yao, lazima ujue vendors wote ambao kampuni iko nawo, vendor yoyote ambaye ni family members you need to disclose.

Any patents and trademarks lazima ziwe disclosed, technical roadmap hii kuonyesha future plans kama capital investments, Market Surveys and Competition analysis, lazima market itazamwe na washindani wa kampuni waangaliwe. Kingine muhimu sana ni Commercial Pipeline hapa ndio important things like future sales, commitments for potential sales.

Tukubaliane kwamba Tanzania kuna ukiritimba kwenye hii sector, wengi wanaofanya kazi kwenye DSE hawana knowledge with stock market, ndio maana mpaka leo hatuna commodity market while 70% ya Tanzania depends on commodities. Mimi niliwai kusema kwamba huko nyuma Watanzania wanazo surplus lakini DSE inashindwa kucapitalize.

Wengi walikuwepo pale DSE hawajui hata how stock market works, they have no knowledge. Huwezi kuwa na market ambayo trading volume ipo constant, lazima trade volume iongezeke. How unaongeza trading volume ni kwaku encourage many companies kuachana na Debt Finance (Very Popular in Tanzania) kuja kwenye equity Finance.

Kampuni kama Azam need to list at least 20% of the total ownership, IPP Media and many other. It is responsibility of DSE kuelekeza hizi kampuni that equity finance is cheaper than debt finance and less risk.

Kingine waliotunga sheria ya uwekezaji Tanzanai hawajui hata how NYSE works. Tukubali baba wa masoko ya shea ni New York Stock Exchange, na wapo wadau wengi wakitanzania wanaofanya kazi Wall Street ambao wanafahamu what is needed kuongeza liquidity kwenye DSE.

Lazima tutunge upya sheria za uwekezaji kwenye DSE. Haya mambo ya kusema sijui unaitaji 5 years of positive net income ili uweze kulist kwenye soko la mitaji that is insane, if I have 5 years of cash flow positive why bothered kuja kwenye DSE while each bank loves me?

I support the idea ya kuanzisha AIM, lakini hii lazima iende parallel na kutunga sheria yenye akili itakayo shawishi individual/bank/Finance institutions nyingi Tanzania kuwekeza kwenye NOMAD.

Sababu Nomad ndio anaye fanya due diligence, yeye ndie mentor wa hizi kampuni, yeye ndio anawasaidia jinsi ya kunadika business proposal, jinsi ya kuvets the idea, yeye ndie anawapeleka mbele ya potential investors wakubwa.

2011 i help kampuni moja ya maji taka (Headworks Inc), a USA entity kujilist kwenye London AIM, process yake sio complicated and costly kama ilivyo New York Stock Exchange. Lakini the vetting process is hard as anywhere else. In the end they didnt secure the deal sababu sales forecast zao zilikuwa too weak.

Tanzania needs a new policies in Stock Market and Private Equity. Potential Investors bado wamekaa na pesa zao au wanawekeza kwenye wazimu.
 
naomba mnisaidie jinsi ninavyoweza kuwekeza katika sok la hisa na je napataje faida na mingeniyoo nawasilisha
 
habari zenu wakuu wa jukwaa hili?
samahani ninaomba kuelekezwa mahali lilipo soko la hisa Dar es Salaam (DSE)
NITASHUKURU KAMA OMBI LITAFANYIWA KAZI.
 
nenda pale makutano ya morogoro road na bibi titi kunaghorofa nimelisahau jina ila linatazamana na dit kwa barabara ya bibi titi
 
Niliona PSPF Golden jubilee building, pale nje kuna notice board inaonyesha ni floor yangapi.
 
habari zenu wakuu wa jukwaa hili?
samahani ninaomba kuelekezwa mahali lilipo soko la hisa Dar es Salaam (DSE)
NITASHUKURU KAMA OMBI LITAFANYIWA KAZI.

Hizi hapa ni address za DSE kama ulivyoomba.

Dar es Salaam Stock Exchange,
14th Floor, Golden Jubilee Towers,
Ohio Street.


P. O. Box 70081, Dar es Salaam, Tanzania


Tel: 255 22 2135779, 2123983, 2128522


Fax: +255 22 2133849


Email: info@dse.co.tz
Website: DSE: Dar es Salaam Stock Exchange
Social media
twitter: https://twitter.com/dsetanzania
Facebook: https://www.facebook.com/dsetanzaniia
Blog: Dar es Salaam Stock Exchange
Youtube: dsetanzania - YouTube
Linkedin: tz.linkedin.com/pub/dse-tanzania/7a/345/b06/
 
Vema sana mmeamua kujiunga humu na social sites zingine, hongereni.

Bado kwa sehemu kubwa jamii ya watanzania inauelewa na utambuzi mdogo sana juu ya soko la mitaji, tunategemea darasa huru na pana katika mambo hayo.

Hili ni jukwaa lenu haswaa. Tunaomba muwe mnaandaa mada maalum na kutupia hapa.
 
LIJUE SOKO LA HISA, MOTIVATIONAL TALKS VIDEO, ni muendelezo wa vipindi vya Dar es salaam stock exchange, ambayo vinaendelea kuonyeshwa kwenye Television na Radio mbali mbali hapa Nchini

Link to video Kama ulikosa kuona.



Lijue soko la Hisa - Motivational Talks 1- #01 - YouTube

Kwa ratiba za vipindi vya TV na Radio angalia hapa kwenye hili Tangazo.

dse+Matangazo.jpg
 
Last edited by a moderator:
Ninachojua DSE ni soko la hisa,ila wana mawakala wao ambao ukifika kwao ndo waweza nunua hisa pia wanaweza kukuelimisha kuhusu faida za hisa,baadhi ya wakala ni Solomon securities, ckumbuki walipo pia kuna Orbit wapo Golden Jubilee 4th floor kama cjakosea,but for more information contact DSE verfied user humu or google contact.

Kwa msaada zaidi google DSE agents Tanzania wapo kama 10 hivi,ushauri mkuu get to know before buying shares na kuna mshirika ambao ukipata zile hisa kweli umewin kama TCC na TBL ila ndo shida kupata, but kama NMB, SWISSPORT, simba cement, twiga cement ni mashirika ukiinvest leo you will reap the benefits in the future.

Good Luck!!
 
Back
Top Bottom