Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Inabidi ujue kwanza kampuni unayotaka kununua hisa 'book value' yake imesimamia wapi.

Kwa mfano mtu anakwambia hisa za swala zilianza kwa sh 600 na sasa zinauzwa 1840 fine that looks profitable at the moment kama nia ni kununua na kuuza hisa. Lakini kama nia ni kununua kwa madhumuni ya kupokea dividend Swala Oil aina hata kitalu let alone ujui maisha yake ya baadae yakoje na iwapo ikipata kitalu ikakosa mafuta au gas ujue ndio mwisho wako na ukute waliowazuga kununua wao ndio wanauza sasa na kusubiri matokeo ya Swala Oil.

Kwa maana hiyo thamani ya hizo share ni kwa sababu tu mtu kakuaminisha Swala Oil inathamani hiyo kutokana na demand zake sokoni lakini si kwamba kuna kampuni ambayo inaweza wekewa value hata kama inafilisiwa unaweza ambulia chochote kutokana na shares ulizonazo,Swala Oil kwa sasa inaweza potea haraka kama ilivyoingia sokoni just by putting its first investment.

Vile vile ata kama unanunua hisa kwenye kampuni ambayo kweli inafanya kazi unatakiwa kujua pia faida inazoingiza na madeni iliyonayo na kama kweli kuna biashara ya kuweza kulipa hayo madeni; kwa sababu unaweza kununua leo hisa kwa bei ya juu lakini baada ya muda mchache ukaja sikia kumbe kampuni inashindwa mudu madeni yake na inatakiwa kufilisika as in what happened na Precision Air ukajikuta auna namna ya kuuza kwa faida or your shares are wiped out baada ya wadai kuchukua chao kwanza.

In short kama hujui 'booka value' ya kampuni una nunua on impulse only, market speculations and just gambling; lakini kama unajua thamani ya kampuni, madeni yake, malengo yake na faida zake za kibiashara unaingia ukijua hela yako hiko salama zaidi na kama uko makini unaweza kuwahi pia kutoka mambo yakianza kwenda mrama.
 
Happy Feet , wengi wetu wabongo hununua kwa lengo la kuuza zikipanda. wengi hatulengi dividend kwakuwa tunapesa ndogo.

Cha msingi ni kununua zikiwa chini, zikipanda uza. Ninamshikaji wangu alinunua hisa za NMB zikiwa zinauzwa sh. 800 alinunua hisa 10,000 leo hii hisa za NMB zinauzwa 4,500. Zidisha hapo

Hasara zipo pia, tena sana tu.
 
Last edited by a moderator:
Kuwekeza kwenye masoko ya hisa kuna faida kubwa lakini vilevile kuna riski kubwa, na hiyo ni theory ya kibiashara high return always associated with high risk.

Hizi stock zipo za aina kuu mbili , kuna common stock na preffered stock. kama kampuni inafirisika wenye preffered mnakuwa wa kwanza kulipwa na wenye common mnakuwa wa mwisho. na hizo common stock zipo za aina mbili , nyingine traded katika IPOs.

Si razima ununue hisa , unaweza ukanunua bonds katika bond market market na ukapata faida kubwa kwa muda mfupi. zipo bonds za miezi mitatu , mwaka , hadi miaka kumi.

Kabla hujanunua hisa kwenye co yoyote inabidi inabidi ufanye speculation , kwa sababu co ikipata hasara na wewe utakuwa umepata loss. Ni pm nikuelekeze jinsi ya ununuaji wa hisa na makampuni ambayo utatengeneza faida, siwezi kuyataja hapa itakuwa nafanya promo.

Mkuu umeongea neno jipya hapa, Bonds , hizi unapata wapi au pale DSE? Au Bond ndo fixed Account?
 
Happy Feet , wengi wetu wabongo hununua kwa lengo la kuuza zikipanda. wengi hatulengi dividend kwakuwa tunapesa ndogo.

Cha msingi ni kununua zikiwa chini, zikipanda uza. Ninamshikaji wangu alinunua hisa za NMB zikiwa zinauzwa sh. 800 alinunua hisa 10,000 leo hii hisa za NMB zinauzwa 4,500. Zidisha hapo

Hasara zipo pia, tena sana tu.
Kila mtu anaingia kwenye hizo sector akiwa na plan zake nimesoma ripoti yao ao jamaa mwaka jana wametoa dividend kwa shareholders almost 34bn sh. at 68 TSH per share kwa hivyo hata kwa kubaki na umiliki hapo ina lipa na biashara inaonekana strong na inayokuwa kwa sasa shares 10000 za mpwa wako mgao wake ingawa si karibu na faida ya aliyouzia. Na mwaka huu tena benki imeshakubali kutoa mgao sh.45bn at 90TZS kwa hivyo wenzake bado wanavuna vizuri tu kwa kubaki na shares zao. Sometimes na muda wa kuuza una matter ndio maana kila mtu na mbinu zake na information is power in that game kuna wengine wanakuja wakati wa mavuno.

Tunarudi pale pale muhimu ni ufahamu wa kampuni mtu anayo enda nunua shares zake na mikakati yake if they think putting their money in shares is better as opposed to a savings account, au labda mwengine ndio kundi la mshikaji wako na wewe mko huko kwa kununua na kuuza looking for a quick buck either way due diligence and being up to date with information in the company you are investing in; is of crucial importance to avoid unnecessary losses and being in the best deciding position.
 
Happy Feet , nakubaliana nawewe kuwa kuifahamu kampuni ndio principle ya kwanza kabla hujafanya uamuzi wa kununua hisa.

Ila ninachopinga mimi ni kuwa faida ya dividend ni ndogo sana na sio ya kuitegemea kabisa. Labda kama nakosea jinsi wanavyopiga hesabu nitaomba unirekebishe kupitia mfano ule ule wa jamaa mwenye hisa elfu kumi za NMB.

Umesema gawio la mwaka huu ni sh. 90 kwa share, hivyo ukichukua hiyo:
90(gawio)x10,000(share)=900,000 (mwaka mzima)
Na kama alinunua sh. 800x10,000=8,000,000
Akauza kwa 4,500x10,000=45,000,000

Hata kama alikaa miaka miwili au mitatu mpaka kupanda bei yupi anafaida hapo?

Huyo anaepokea laki tisa kwa mwaka itamchukua miaka 50 kuja kufikisha hiyo pesa 45 mil.

Kama nimekosea hesabu ya dividend nirekebishe ila kama hesabu hiyo nipo sawa usiingie kwenye hiyo game kwa kungojea dividend labda uende TBL wao wanatoa 400/share japo ukipiga na gharama ya share zao ni yale yale.
 
Last edited by a moderator:
MCHUNGUZI HURU Mkuu ndio maana nikasema kila mtu inabidi awe informed kwenye maswala ya investment na kuingia kwa mkakati na labda kweli investors wengi ni watu wa kukurupuka ndani ya Tanzania. Delving a little deeper in the company and after learning how much NMB pays in dividends siwezi kununua shares 10000 kwa bei ya 4500 na kusubiri share holders meeting iamue kama mwaka ujao wataamua kiasi gani tena hata kama inaonekana biashara inakuwa.

Kwa sasabu hiyo hiyo millioni 45 kama ningeiweka humo humo NMB in their savings account wananipa 10% annual interest yaani 4.5m TSH au kama nina kiwanja naweza jenga na hiyo hela na kupata a way better return in the rental market au hata nikunua nyumba za NHC za kigamboni at 50m napata better return nikipangisha na bado nina asset ambayo ni better compared to a share purchase in my eyes.

Kwa mtu makini awezi kununua hizo stock at that price simply ni ukichaa and that is not an advise which would be given by a clever investment advisor because there are several better ways to invest as opposed to buying those stocks that just pure gambling.

Sasa basi what fueled this increase in share prices za NMB its just hype kwenye facts sheet hakuna cha zaidi kwa sababu dividends are not luring compared to their savings accounts with interest payments vilevile rough estimate ya shares kama tunagawanya 45bn/90=500m shares (kama kuna walakini wa namba you get the gist so you should do the maths elsewhere). Hiyo 500m mara 4500 bei ya sasa ya shares ina maana market inadhani NMB is worth 22500 (by marking to market) way of the book value kwa sababu kampuni yenyewe hipo hivi
During this AGM, NMB Chief Executive Officer, Mr. Mark Wiessing, made a presentation to the members of NMB on the progress made by the bank in 2013. He said "Once again this year NMB Plc has achieved impressive financial results. Revenues increased by 18% to Tzs 422 billion, Loans up 20% to Tzs 1,614 billion, deposits up 13% to Tzs 2,583 billion. This performance resulted in a PAT of Tzs 134 billion, being 37% up from last year". Source; their website

Kwa maana hiyo biashara ina rely heavily na deposits zilizopo kufikia malengo ya business; hila sidhani kama wana assets ambazo zinafikia market valuation na believe me serikari kama inaamua kuchochea maendeleo na ku limit interest rates zirudi at single digits hiyo profit ya 134bn would decrease rapidly na sidhani kama dunia nyengine shares zinaweza kuwa sawa na initial asking prices ya 800 Tsh (which is close to the book value of the company in share prices by the looks if they are to release new IPO's in the near future) kwa maana shares za 4500 are way overpriced.

Jumlisha na madeni yake if things were to go wrong that could prove to be a very bad investment at 4500 a share ingawa sioni mambo kwenda mrama kwa sababu serikari zetu azinaga taratibu za ku-regulate banks (in monetary policies thinking) ili kuchochea maendeleo ya uchumi na biashara na ata kama wangetaka kwa 'business model' za namna hii kwenye mabenki tusitegemee tushushiwe interest rates leo wala kesho maana kama wote wapo hivi kuwapunguzia rates za benki akiba za watu zinaweza potea hivihivi kirahisi kwa sababu madeni yenyewe yao mengi ni ya nje na bado wamekopesha watu wakitegemea (that is a whole lot of a debate) thereby ukiwaambia wapunguze rates hawa kasheshe be it at the cost of developing quicker macro-economically.
 
Ndugu wana JF, napenda kufahamu zaidi kuhusu jinsi ya kuwekeza kwenye soko la hisa katika mambo yafuatayo:-
1.Kujua hisa zenye faida
2.Mtaji unatakiwa kuweza kupata faida hasa kwa mtu mwenye kipato cha kati
3.Ni hisa za kampuni gani zenye faida katka uwekezeji.

Ntapenda kujifunza kutoka kwenu ukizingatia mie ni mfanyakazi napata muda mchache sana kusimamia bihashara nyingine.

Mkuu una nia njema sana katika ulimwengu wa biashara.
Binafsi nilienda DSE pale ofisini kwao Golden Jubilee Tower nikapata ufafanuzi wa kina na maelezo yakinifu.
Mostly, biashara hii DSE wanafanya kupitia brokers na brokers maarufu waliopo kwenye game ni Vertex, Orbit na wengineo kadha wa kadha.
Hisa ziko za makampuni mengi pale ila so far yanayofanya vema ni TBL, TCC, TWIGA, DCB, NMB, SWALA, na nyingine nyingi tu.

DSE hawauzi hisa direct to customer isipokuwa through their brokers kama nilivyokutajia hapo juu kwa uchache.
Its a nice investment kama ukifatilia kwa karibu and if you have money to invest with no quickness to get your investment back in a short period of time.

I have tried in a nutshell to cast a light on the matter but if you go to their offices (DSE) they will give you all the necessary details.
 
Kuwekeza kwenye masoko ya hisa kuna faida kubwa lakini vilevile kuna riski kubwa, na hiyo ni theory ya kibiashara high return always associated with high risk.

Hizi stock zipo za aina kuu mbili , kuna common stock na preffered stock. kama kampuni inafirisika wenye preffered mnakuwa wa kwanza kulipwa na wenye common mnakuwa wa mwisho. na hizo common stock zipo za aina mbili , nyingine traded katika IPOs.

Si razima ununue hisa , unaweza ukanunua bonds katika bond market market na ukapata faida kubwa kwa muda mfupi. zipo bonds za miezi mitatu , mwaka , hadi miaka kumi.

Kabla hujanunua hisa kwenye co yoyote inabidi inabidi ufanye speculation , kwa sababu co ikipata hasara na wewe utakuwa umepata loss. Ni pm nikuelekeze jinsi ya ununuaji wa hisa na makampuni ambayo utatengeneza faida, siwezi kuyataja hapa itakuwa nafanya promo.

Cjui namna ya kupm coz hata no zako czijui, naomba unisaidie mawasiliano yako plz
 
Nimeona leo nishare na nyinyi kuhusu soko la hisa na jinsi ya kunufaika nalo.Kwa kifupi kuwa na hisa ni kumiliki sehemu ya kampuni au kuwa mmiliki wa kampuni hiyo kwa maana hiyo unakuwa na nafasi ya kushiriki kufanya maamuzi ,kupata faida au hasara katika kampuni hiyo.

Unanunuaje Hisa?

Hisa katika soko la hisa dare s salaam huuzwa na brokers kama orbit securities, na wengineo wapo wengi tu ila hawa ndio ninawafahamu. Unaweza pata taarifa zaidi kupitia website ya soko la hisa la dare s salaam www.dse.co.tz.

Faida za kununua hisa;
i) Hisa hukuwezesha kupata gawio la faida ya kampuni hiyo ikiwa itatangaza faida .

ii)
Ukiwa na mwanahisa unaweza kutumia cheti cha hisa (share certificate) kuombea mkopo, ingawa hili ni jambo geni kwa Tanzania .

iii)
Hukulinda dhidi ya anguko la thamani ya fedha kwa kuwa fedha huwa na tabia ya kupoteza thamani unaponunua hisa inaweza kukulinda kwa kuwa hisa huwa na tabia ya kupanda thamani kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa.

iv)
Unaweza nunua na kuziuza wakati wowote.

Jinsi ya kununua hisa kwa kampuni unalohitaji;

Unapofika kwenye soko la hisa la dare s salaam kuna makampuni mengi yaliyoorodheshwa kuuza hisa zao mfano CRDB, NMB, USL, DCB, KCB, SWISS PORT, TBL, TTP na nyingine nyingi.

Sasa ni kampuni ipi ununue hisa ni vyema ukaangalia mambo yafuatayo;

i) Performance ya kampuni. Mfano kampuni kama inafanya kazi vizuri kwa weledi na inamategemeo ya ukuaji wa kampuni hiyo kama kutanua matawi, kuongeza product au kukua kwa biashara katika kampuni hiyo basi hiyo ni kampuni nzuri mfano.

Ukisikia kampuni imetanua soko lake kama CRDB ilivyofungua matawi nchi za nje inamaana ya kuwa faida ya kampuni hiyo itaongezeka na hivyo gawio linaweza kuwa kubwa na wewe kupata faida na pia bei ya hisa itaweza kuongezeka hivyo utapata faida pia pindi ukiamua uza hisa zako.

ii)
Bei ya hisa na uimara wake (stable share price) kuna kampuni ambazo bei zao za hisa wakati wote ni nzuri kwa maana hazishuki sana au mara kwa mara na pia zina tabia za kuongezeka mfano TBL , SWISS PORT, TCC.

iii)
Wakati wa kununua hisa . ni muhimu pia kuangalia ni wakati gani unanunua hisa mfano. Wakati ambao hisa ndio zinaingizwa au kuuzwa kwa mara ya kwanza kwenye soko la hisa bei huwa ni ndogo sana na baada ya hapo mara nyingi bei huongezeka ingawa kuna wakati hushuka pia .

Lakini bei ya hisa hupanda kushuka kutokana na nyakati katika mwaka mfano ifikapo mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka bei hushuka na kuwa ndogo zaidi ila katikati ya mwaka bei huanza kupanda kwa kasi kubwa zaidi

iv)
Uwepo wa taarifa nzuri katika Sekta iliyo kampuni hiyo au katika kampuni hiyo. Mfano imekuwa ikisikika kuwa benki ya CRDB itakuwa inatumika kulipia mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali basi siku ukisikia imeingia mkataba huo au imeanza kutumika kulipia mishahara hiyo basi nenda kanunue hisa hizo haraka kwani bei ya hisa itaanza kupanda na pia gawio la faida litakuwa kubwa.

Mfano mwingine ni kwa kampuni ya SWISS PORT kampuni hii inadeal na mizigo kwenye viwanja vya ndege,nafikiri taarifa ya kutanuliwa kwa uwanja wa ndege ya Dare s salaam inafahamika hivyo ni wakati mzuri kununua hisa wakati huu kwani pindi uwanja utakapokamilika basi kampuni itakuwa na biashara kubwa bei ya hisa itaongezeka na faida pia

v)
Wingi wa makampuni katika soko la hisa. Mfano kuna mabenki zaidi ya matano hii inamaana benki hizi zinagombea wateja hii ni kwa wateja wote wale wanaowahudumia na wale wa kwenye soko la hisa hivyo bidhaa zao zipo za kutosha na bei itakuwa ya kawaida mambo ya demand na supply. Kwa bei ya leo kampuni inayoongoza ni TCC- 17000, TBL 15000, JHL 10620, SWISS 6600,ACA-6540. Makampuni haya yote yanafanya shughuli tofauti na bei zake ni nzuri zaidi.

Ushauri kwa wanaotaka kununua hisa;
Kama unahela ya ambayo umeiweka tu mahali ukiwa na lengo la kufanya kitu baada ya mwaka au miezi kadhaa ijayo nenda soko la hisa kanunue hisa za SWISSPORT kwa jinsi bei inavyoongezeka kuna uwezekano mkubwa mwakani muda kama huu bei ya hisa yake moja itakuwa mara mbili zaidi ya bei ya sasa, kwa kifupi ukija kuuza hisa ulizonunua wakati huu basi mwakani zitakuwa mara mbili zaidi kudeclare interest mimi ni mwanahisa tu wa soko la hisa la Dar es salaam.

Nakaribisha na wataalamu wengine waweze kuchangia kuboresha zaidi.
 
Naomba kujua. Hii biashara inawezekana kufanyika online yaani bila kutembea physically kwa broker au dealer au DSE?

Namaanisha kuifanya popote ulipo na kupata taarifa za kupanda na kushuka (fluctuations) kwa hisa za kampuni tofauti?
 
je kama kampuni ikipata hasara na mimi napata hasara?
na kwa mfano nikitaka kujua faida nafanyaje?
 
mfano nikiwa na kama milioni moja mwakani mda kama huu ntakuwa na shilingi ngapi?(zingatia kampuni yoyote inayofanya vizuri)
 
je kama kampuni ikipata hasara na mimi napata hasara?
na kwa mfano nikitaka kujua faida nafanyaje?

Sure mkuu Co. Ikipata hasara na wewe unapata hasara, shareholders ikitokea Co. Imefilisika wao hua wa mwisho kulipwa kwenye kile kinachobakia baada ya wengine kua wamelipwa!

Jinsi ya kujua faida kuna namna mbili kupitia dividend/gawiwo na capital gain sijui kiswahili tunaiitaje! Faida kupitia gawiwo unalipata pale kwa mfano unamiliki hisa 5000 then Co.

Ikatangaza kwenye kila hisa 1 utapata gawiwo la sh.100 then hapo utapata faida ya(5000×100)= sh.500,000# mkuu na Capital gain ni pale kwa mfano ulinunua kila hisa 1 kwa sh.500 na unahisa 5000 then ulitumia(500×5000)= sh.2,500,000 kama mtaji wako so ikitokea leo ukauza hisa zako na kila hisa ukauza kwa sh.1000 manake itakua ni 1000×5000(idadI ya hisa unazomiliki)=5,000,000 then faida yako hapo ni ile pesa uliyopata kipind umeuza hisa zako 5,000,000 kutoa pesa ulizonunulia hisa zako 2,500,000=2,500 000 pole kwa maelezo marefu mkuu wangu!!
 
Back
Top Bottom