mwasambili
Senior Member
- Oct 28, 2013
- 151
- 77
Sure mkuu Co. Ikipata hasara na wewe unapata hasara, shareholders ikitokea Co. Imefilisika wao hua wa mwisho kulipwa kwenye kile kinachobakia baada ya wengine kua wamelipwa!! Jinsi ya kujua faida kuna namna mbili kupitia dividend/gawiwo na capital gain sijui kiswahili tunaiitaje! Faida kupitia gawiwo unalipata pale kwa mfano unamiliki hisa 5000 then Co. Ikatangaza kwenye kila hisa 1 utapata gawiwo la sh.100 then hapo utapata faida ya(5000×100)= sh.500,000# mkuu na Capital gain ni pale kwa mfano ulinunua kila hisa 1 kwa sh.500 na unahisa 5000 then ulitumia(500×5000)= sh.2,500,000 kama mtaji wako so ikitokea leo ukauza hisa zako na kila hisa ukauza kwa sh.1000 manake itakua ni 1000×5000(idadI ya hisa unazomiliki)=5,000,000 then faida yako hapo ni ile pesa uliyopata kipind umeuza hisa zako 5,000,000 kutoa pesa ulizonunulia hisa zako 2,500,000=2,500 000 pole kwa maelezo marefu mkuu wangu!!
kaka asante nimekuelewa, wiki ijayo nitaanza mchakato, nina kama laki tano hivi inatosha kuanzia, nitamuwekea mwanangu