Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SOKO LA KARIAKOO NA HARAKATI ZA TANU
Hii makala nimemwandikia ndugu yangu Kheri Chomba mwenyeji wa Kariakoo kumfariji kuwa asihuzunike pale inapotokea watu wakatucheza shere kwa kujifanya kuwa wao wanaujua mji kutushinda sisi wenyewe.
"Kheri siku moja katika miaka ya 1970s soko jipya limeshajengwa tulikuwa na kawaida ya kupunga upepo kwenye baraza la soko upande wa Tandamti mimi na rafiki yangu Tamim Faraj wa MUM.
Tukizungumza mengi kuhusu mchango wa soko katika harakati za kupigania uhuru wakati Abdul Sykes ni Market Master.
Pale tulipokuwa tunapenda kukaa kama soko la zamani lingekuwako ofisi ya Market Master ingekuwa kushoto kwetu.
Tamim akaniambia, "Uncle kama sisi hatutaandika historia ya Abdul Sykes basi jua vizazi vijavyo vitaamini TANU iliasisiwa na Nyerere.
Uncle lazima tuandike historia hii."
Tamim alinisaidia sana hasa katika uchambuzi wa mambo yalivyokuwa na kwa nini imekuwa hivi haikuwa vile.
Katika kitabu nimemshukuru kwa msaada wake kiasi nimesema ndani ya kitabu nashindwa kutofautisha baina ya maneno yangu na yale yake.
Unajua Market Master alikuwa Mwingereza Brian Hodges alipotoka ndiyo nafasi ile wakampa Abdul Sykes.
Ikawa Waingereza wamejipiga wenyewe risasi ya mguuni.
Nafasi ile ilimpa Abdul nguvu kubwa ya kuoganaizi wafanyabiashara wa pale sokoni nyuma ya TANU.
Abdul Sykes akiuza kadi za TANU pale sokoni na akamleta Nyerere pale akamkabidhi kwa Shariff Abdallah Omar Attas.
Balaa lake halisemeki.
Anaemjua Shariff Attas atajua haraka jungu lililokuwa likipikwa pale sokoni.
Jungu likatokota Town Clerk Mzungu huyo akaja kumvamia Abdul ofisini kwake akakamata kadi za TANU.
Abdul akapambana na Mzungu kidole machoni.
Abdul Sykes Kiingereza ndiyo lugha yake.
Pazuri hapa.
Soko likavuma kuwa Abdu anafukuzwa kazi.
Stori hii Mzee Kisaka anaijua maana alikuwa karani pale ofisini kwa Market Master.
Ikapigwa tawasil kondoo akachinjwa Mzungu asionekane sokoni pale.
Watu wanadhani Nyerere ndiye alikuwa wa kwanza kufanyiwa dua na wazee wa Dar es Salaam.
Pale sokoni alikuwapo Shariff Mbaya Mtu.
Watu wa nyuradi.
Kaburi lake liko pale Kisutu kwa masharifu.
Kheri wazee wetu walikuwa watu.
Mjomba wangu Bwana Hamisi alikuwa na ubao na hadi leo anao ingawa sasa ni mtu mzima vijana wake ndiyo wanatarazak.
Mjomba wangu yu hai hadi leo."
Kulia ni Shariff Abdallah Omar Attas.
Picha ya mwisho ni Nyerere akisindikizwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya UNO 1955 na akina mama wanne wa kwanza kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (huyu alikuwa mkewe Shariff Abdallah Attas), Bi. Titi Mohamed na kushoto wakwanza ni Bi. Tatu bint Mzee na Nyerere ni huyo katikati.