Soko la nyanya

Soko la nyanya

lussajo

Member
Joined
Aug 20, 2016
Posts
28
Reaction score
37
Mimi ni mkulima toka dodoma. Nina nyanya lakini soko ni tatizo. kwa mwenye taarifa za soko msaada tafadhali
0629 046084
 
Upo Dodoma sehemu gani? taja mahali ulipo , vipi hilo soko likipatikana una uwezo wa kusupply mwenyewe mpaka sokoni? Nyanya ni bidhaa inayooza mapema so jibu hayo maswali. Vipi bei? unauza kwa debe au kilo ? Ongeza taarifa
 
Nipo kilomita 30 toka Dodoma mjini barabara ya kuelekea Kondoa. Ninauza kwa debe la lita 20 ni Tsh. 10,000 shambani negotiatable.
 
Mimi ni mkulima toka dodoma. Nina nyanya lakini soko ni tatizo. kwa mwenye taarifa za soko msaada tafadhali
0629 046084
KIPINDI HIKI KUUZA NYANYA NI NGUMU SANA SOKO LIPO LAKINI BEI IKO CHINI SANA,
 
HAPO NDIPO MTAONA UMUHIMU WA VIWANDA VYA KUSINDIKA NYANYA.....
NCHI YA VIWANDA VIWANDA WAANZE NA HIYO BASI

OVAA
 
Morogoro debe ni buku moja hadi mia saba
Eeee bwana eee umemiua jamaa yangu mwaka huu hii biashara ni kichaa hapa Dodoma.
lussajo pole hiyo bei ya 10,000/ sio kabisa km upo Makutupora au Mzakwe ungesogea hata hapo Msalato kwa Bukuku ukaulizia bei
Mjini Dodoma kisaDolin cha 5ltr ni sh 500/ kwa mlanguzi wa Soko kuu Majengo kwa hiyo debe (doom) ni 2,000/ (buku bee)
Du ni kuchoka tu sasa matikiti ndio usiseme yameshuka haswaaa
na joto hivi limeanza ziwahishe mkuu
 
Inasikitisha sana, mtu unalima then unakosa pa kuuza, sasa mtu utarudia tena kulima?Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri kwa wakulima. Kwanini kusiwepo insurance ya soko? Nchi zingine serikali inachukua jukumu la kugarantii soko ili wakulima wapate moyo wa kulima. Kwanini wasiruhusu wakulima wauze nchi za jirani mazao yao??
 
Mimi matikiti yamenipuna mtaji mwaka huu sina hamu.
 
Ni kweli Nyanya hazina bei nzuri kwa sasa, wiki mbili zilizopita wakulima walikuwa wanagawa nyanya bure maana zinaoza so sad. Pia kibiashara kabla hujaamua kufanya biashara tafuta soko kwanza ndipo uanze biashara. Kwa sasa kuna watu wengi wameingia kwenye kilimo na kuzidi uhitaji wa soko la ndani hivyo ni hatari maana hatuna viwanda vya kusindika na ku add value
 
Kwa TZ ni vigumu kutafuta soko la mazao ya kilimo kabla hujalima kwa sababu bei zinaendeshwa na uwingi / uchache wa bidhaa. Dawa yake ni hiyo tu ya usindikaji.
 
Njia za kupata soko kabla ya kulima zipo. Contract farming ni moja ya njia hizo - bei ya Mazao inakuwa fixed no matter what is happening in the market place kama bei imepanda au kushuka. Uzuri wa njia hii ni uhakika wa soko ila ni muhimu kuwa makini na vipengele vya mkataba. Changamoto kwa mkulima ni kuzalisha mazao bora kulingana na mkataba. Mnunuzi atafuatilia mchakato mzima wa uzalishaji kujiridhisha. Hii ipo na inafanyika hapa bongoland
 
Suala la kuwa na viwanda vya kusindika ni la muhimu sana
 
Njia za kupata soko kabla ya kulima zipo. Contract farming ni moja ya njia hizo - bei ya Mazao inakuwa fixed no matter what is happening in the market place kama bei imepanda au kushuka. Uzuri wa njia hii ni uhakika wa soko ila ni muhimu kuwa makini na vipengele vya mkataba. Changamoto kwa mkulima ni kuzalisha mazao bora kulingana na mkataba. Mnunuzi atafuatilia mchakato mzima wa uzalishaji kujiridhisha. Hii ipo na inafanyika hapa bongoland
Uko sahii lkn contract farming labda mwenye Cash Crops lkn kwa mazao ya Horticulture ni changamoto sana,pia na aina ya wakulima wetu wengi wanafanya kilimo cha kujikimu sio hasa cha biashara.
 
VINAHITAJIKA VIWANDA VYA KUSINDIKA NYANYAAAA ILI KUOKOA JAHAZI HILI....

OVA
 
Back
Top Bottom