jumamwaki
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 244
- 225
Habari wapendwa.
Tukiwa tupo mbioni kumsaidia mh rais samia kwenye kuleta maendeleo kuna baadhi ya mambo ambayo huenda yanasababishwa na viongozi kwa kujua yaani makusudi au kwa kutojua.
Nianzie kwenye mambo yafuatayo kwenye jiji letu la mbeya ambayo kwa kweli yanakera sana .
#soko la sido ni miongoni mwa masoko makubwa nchini tanzania , soko ambalo lina utaratibu wa kila baada ya muda fulani kufanyika uchaguzi wa viongozi wa soko.
Lakini ni miaka mingi inaenda kukatika bila kufanyika uchaguzi wa viongozi wa soko.
Swali kwa mkurugenzi wa jiji.
Napenda kuuliza uongozi wa jiji la mbeya kwa kuanza na mkurugenzi wa jiji la mbeya .Swali langu ni moja tu
Je, unatambua kuwa ni muda umepita bila kufanyika uchaguzi wa uongozi kwenye soko la sido? Ikiwa unatambua kuna changamoto gani ambayo ni ngumu kuwashilikisha wananchi waliopo kwenye soko husika ?
2. Hivi karibuni uchaguzi uliiitishwa na ghafra ukahailishwa je unatambua hilo,
Ikiwa unalitambua kwa nini usiitishe kikao kuwaeleza wafanya biashara wa soko la sido kuhusu changamoto kama zipo .
3. Miundo mbinu ya soko la sido hadi maeneo ya kabwe .
Ni maeneo ambayo yanasahaulika sana kuhusu ukusanyaji wa taka , takataka zinawekwa kwa muda mrefu ukilinganisha na matumizi ya eneo husika na idadi ya watu wanaolitumia , hivi kwamba kuna muda unakuta harufu ni kali mno jambo ambalo huleta athari kiafya hususa ni kwa walio maeneo ya karibu na wauza vyakula .
4. Wezi na vibaka kuongezeka
Maeneo ya kabwe kwa sasa sio salama sana , kuna hatari sana mida ya kuanzia saa mbili na kuendelea watu wanaibiwa na kuumizwa
Kwa kweli mambo haya ni kero sana kwenye jiji la mbeya .
Tafadhari karibu kwa maoni mengine kuhusu jiji letu la mbeya .