Soko la ufuta likoje kwenye mkoa uliko?

Soko la ufuta likoje kwenye mkoa uliko?

Hapo mzee una kama million 10 hivi, hongera sana kwa kupiga kilimo. Ulilima heka ngapi?
Million 10 haifiki, ingekuwa labda kilo ni 5000, naulizia soko dodoma wananambia bei ni 3700 per kg
 
Amani iwe kwenu,

Ufuta ni zao moja zuri sana kibiashara, hapa nilipo ni nimevuna takribani gunia kama 20 ivi.

Uliko bei ya ufuta ikoje?, ili tuangalie soko sehemu nzuri.
Nilipo ufuta haulimwi.
 
Hongera sana mkuu, na kwa hila ekari ulitumia wastani wa kiasi gani cha fedha mpaka unavuna ufuta halisi. Itapendeza ukaweka na mchanganuo wa matumizi husika.
Ekari nane mkuu
 
1. Kama shamba ni la kukodi
Ekari moja = 30,000
2.Mbegu kilo 3 per ekari @4000
3.palilizi per ekta = 25,000
4. Uvunaji= 18, 000 per ekta
5. Upandaji =2,500 per ekta
6.kupiga( kukung'unta) = 3000 per gunia
7.kulima kwa trekta = 40, 000 per ekta

Gharama za msingi ni hizo, na huku nilikolimia, ekari moja inaweza toa hadi gunia 3 .
 
Hongera sana kaka, nitakucheki ili tuwasiliane kwa kina.
1. Kama shamba ni la kukodi
Ekari moja = 30,000
2.Mbegu kilo 3 per ekari @4000
3.palilizi per ekta = 25,000
4. Uvunaji= 18, 000 per ekta
5. Upandaji =2,500 per ekta
6.kupiga( kukung'unta) = 3000 per gunia
7.kulima kwa trekta = 40, 000 per ekta

Gharama za msingi ni hizo, na huku nilikolimia, ekari moja inaweza toa hadi gunia 3 .
 
Bei ya jana mnada wa Songea vijijini 3700. .. choma choma washastuka minada inashuka tu, kutoka bei 4540 songwe week tatu zilizopita leo 3700.... Chomachoma wakinunua hadi3400. Ila kwasasa chomachoma 2500.... Kuna uwezekano soko likashuka zaidi kwasababu ufuta upo mwingi sana kuanzia kilwa, Ruangwa,liwale na tunduru Ruvuma...

Soko la dar limeshuka zaidi hadi 3500. Wananunua wachina... Ila wanapata ufuta unaotoka moro kilosa,, ila kwa kusini kote ni stakabadh ghala Tu, hauwezi kusafirisha kupeleka dar.

Kama una pesa zako tulia tu kwanza, soko likiyumba katikat hapa ya mwenz wa sita.. chomachoma bei zitashuka zaidi hapo hapo ndo wataalamu wa hizi kazi ndo wanaingia porini kuzoa ufuta kwa bei rahis ya 2000, mwishoni bei inakuja kustuka hata kwa 3500-4000.
 
Hii ndo shida ya ufuta, unapanda weak moja, baada ya hapo unaporomoka hatari
 
Back
Top Bottom