Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilipo ufuta haulimwi.Amani iwe kwenu,
Ufuta ni zao moja zuri sana kibiashara, hapa nilipo ni nimevuna takribani gunia kama 20 ivi.
Uliko bei ya ufuta ikoje?, ili tuangalie soko sehemu nzuri.
Karibu nikuiwai tuDar!! nitafikaje huko, naitamani hiyo bei
Hongera mkuuEkari nane mkuu
Huku kusini tunasubiri mnada tuanze kunywesha mbuzi soda
Ekari nane mkuu
1. Kama shamba ni la kukodiHongera sana mkuu, na kwa hila ekari ulitumia wastani wa kiasi gani cha fedha mpaka unavuna ufuta halisi. Itapendeza ukaweka na mchanganuo wa matumizi husika.
1. Kama shamba ni la kukodi
Ekari moja = 30,000
2.Mbegu kilo 3 per ekari @4000
3.palilizi per ekta = 25,000
4. Uvunaji= 18, 000 per ekta
5. Upandaji =2,500 per ekta
6.kupiga( kukung'unta) = 3000 per gunia
7.kulima kwa trekta = 40, 000 per ekta
Gharama za msingi ni hizo, na huku nilikolimia, ekari moja inaweza toa hadi gunia 3 .
Hii ndo shida ya ufuta, unapanda weak moja, baada ya hapo unaporomoka hatariBei ya jana mnada wa Songea vijijini 3700. .. choma choma washastuka minada inashuka tu, kutoka bei 4540 songwe week tatu zilizopita leo 3700.... Chomachoma wakinunua hadi3400. Ila kwasasa chomachoma 2500.... Kuna uwezekano soko likashuka zaidi kwasababu ufuta upo mwingi sana kuanzia kilwa, Ruangwa,liwale na tunduru Ruvuma...
Soko la dar limeshuka zaidi hadi 3500. Wananunua wachina... Ila wanapata ufuta unaotoka moro kilosa,, ila kwa kusini kote ni stakabadh ghala Tu, hauwezi kusafirisha kupeleka dar.
Kama una pesa zako tulia tu kwanza, soko likiyumba katikat hapa ya mwenz wa sita.. chomachoma bei zitashuka zaidi hapo hapo ndo wataalamu wa hizi kazi ndo wanaingia porini kuzoa ufuta kwa bei rahis ya 2000, mwishoni bei inakuja kustuka hata kwa 3500-4000.