Sokoine University of Agriculture (SUA) special Thread

Sokoine University of Agriculture (SUA) special Thread

Pale ni hatari jamani
Unakutana na matofali ohooo

Si stationary kwa kassim,unit 1 up to 6

Sua acha kabisaa ila sio chuo kigumu kma wengi wanavodhani

Ila tatizo wanafunzi wengi hatupendi kusoma
Hakuna kitu,Sua ni chuo dhaifu,ili kuficha hayo tunasema ni pagumu.
 
Bi
Introduction
Nimeamua kuanzisha uzi huu mahsusi unaohusu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kama njia ya kukienzi chuo hiki kikongwe na cha kipekee nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Awali ya yote naomba ku declare interest kwamba mimi ni mhitimu kutoka SUA miaka mingi iliyopita wakati huo mfumo wa ufundishaji ukiwa wa Term System. Kwa sasa ufundishaji unafanyika kwa mfumo wa Semester System au ukipenda unaweza kuuita Mfumo wa Mwendokasi.

About the University
Kama jina la chuo linavyosadifu, chuo kilianzishwa kwa jitihada na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama njia ya kuzalisha wasomi kwenye fani ya kilimo (ukulima na ufugaji) mnamo mwaka 1984 na kupewa jina la aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, ndugu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kupata taarifa zaidi kuhusu SUA, tembelea tovuti rasmi ya chuo (Welcome to Sokoine University of Agriculture (SUA) )

View attachment 2088281
Nembo ya chuo

Academics
Ili kufanikisha utoaji wa elimu kwa wanafunzi na wadau wengine, chuo kimegawanyika katika colleges 5 na deparments 6 (kwa mujibu wa tovuti ya chuo).

View attachment 2088293
Colleges

View attachment 2088302
Departments

Mwaznoni chuo cha SUA kilijikita kwenye ufundishaji wa masuala ya kilimo tu na kutoa shahada kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor’s degree) na kuendelea mpaka shahada ya uzamivu (PhD) pamoja na kozi fupi lakini kwa sasa kinatoa hadi kozi za astashahada na cheti katika fani mbalimbali. Sasa hivi kinafundisha masuala mengi yakiwemo ualimu, maendeleo vijijini na mwasiliano (tazama kielelezo hapo chini). Kwa hiyo, hiki si chuo cha kilimo tu kama wengi wanavyodhani bali sasa hivi kinajikita kufundisha kozi mtambuka zinazofundishwa katika vyuo vingine vya kawaida.

View attachment 2088303
Kozi zinazofundiswa

Academic facilities
Mojawapo ya hazina ambayo chuo cha SUA kinajivunia ni uwepo wa maktaba kubwa ya kitaifa ya kilimo ijulikanayo kama The Sokoine National Agricultural Library (SNAL) iliyoanzishwa rasmi mwaka 1991. Maktaba hii imesheheni vitabu, journals na machapisho mbalimbali ambayo wanachama wake nchini Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanaweza kuyafikia na kujisomea.

View attachment 2088305
The Sokoine National Agricultural Library (SNAL)

Pamoja na uwepo wa maktaba kubwa ya kimataifa, chuo pia kina kumbi mpya na nzuri za mihadhara tofauti na zile nilizoziacha miaka ile. Kwa ujumla miundombinu na huduma za ufundishaji zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.


View attachment 2088307
Kumbi mpya za mihadhara (MLT9 & 10)

Kwa ushirikiano na wenzangu waliosoma na ambao bado wanasoma kwenye chuo hiki kikongwe na maarufu, tutajitahidi kuwaletea upadates mbalimbali zinzohusu chuo kwa kadri itakavyowezekana. Samahani mods naomba uzi huu uwe pinned ili wadau waweze kuupata kwa urahisi.

Nawasilisha.

Pia soma:

Bila kutaja course na mwaka uliohitimu, huu uzi ni batili.
 
Back
Top Bottom