Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna kitu,Sua ni chuo dhaifu,ili kuficha hayo tunasema ni pagumu.Pale ni hatari jamani
Unakutana na matofali ohooo
Si stationary kwa kassim,unit 1 up to 6
Sua acha kabisaa ila sio chuo kigumu kma wengi wanavodhani
Ila tatizo wanafunzi wengi hatupendi kusoma
Ngoja nikutajie mmoja kwanza , Al Akh Ibn Ghulaam unamjua ?Hhhhhhh ulijuaje kijana wataje huenda nawajua
Na ww ni mdau wa Msasua nini?Ngoja nikutajie mmoja kwanza , Al Akh Ibn Ghulaam unamjua ?
Ndio , ila Mimi bado naendelea kusoma na nipo Main huku.Hhhhhh namjua sana na mm ananijua sana juzi tu tuliongea kwa simu
Na ww ni mdau wa Msasua nini?
Bila kutaja course na mwaka uliohitimu, huu uzi ni batili.Introduction
Nimeamua kuanzisha uzi huu mahsusi unaohusu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kama njia ya kukienzi chuo hiki kikongwe na cha kipekee nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Awali ya yote naomba ku declare interest kwamba mimi ni mhitimu kutoka SUA miaka mingi iliyopita wakati huo mfumo wa ufundishaji ukiwa wa Term System. Kwa sasa ufundishaji unafanyika kwa mfumo wa Semester System au ukipenda unaweza kuuita Mfumo wa Mwendokasi.
About the University
Kama jina la chuo linavyosadifu, chuo kilianzishwa kwa jitihada na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama njia ya kuzalisha wasomi kwenye fani ya kilimo (ukulima na ufugaji) mnamo mwaka 1984 na kupewa jina la aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, ndugu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kupata taarifa zaidi kuhusu SUA, tembelea tovuti rasmi ya chuo (Welcome to Sokoine University of Agriculture (SUA) )
View attachment 2088281
Nembo ya chuo
Academics
Ili kufanikisha utoaji wa elimu kwa wanafunzi na wadau wengine, chuo kimegawanyika katika colleges 5 na deparments 6 (kwa mujibu wa tovuti ya chuo).
View attachment 2088293
Colleges
View attachment 2088302
Departments
Mwaznoni chuo cha SUA kilijikita kwenye ufundishaji wa masuala ya kilimo tu na kutoa shahada kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor’s degree) na kuendelea mpaka shahada ya uzamivu (PhD) pamoja na kozi fupi lakini kwa sasa kinatoa hadi kozi za astashahada na cheti katika fani mbalimbali. Sasa hivi kinafundisha masuala mengi yakiwemo ualimu, maendeleo vijijini na mwasiliano (tazama kielelezo hapo chini). Kwa hiyo, hiki si chuo cha kilimo tu kama wengi wanavyodhani bali sasa hivi kinajikita kufundisha kozi mtambuka zinazofundishwa katika vyuo vingine vya kawaida.
View attachment 2088303
Kozi zinazofundiswa
Academic facilities
Mojawapo ya hazina ambayo chuo cha SUA kinajivunia ni uwepo wa maktaba kubwa ya kitaifa ya kilimo ijulikanayo kama The Sokoine National Agricultural Library (SNAL) iliyoanzishwa rasmi mwaka 1991. Maktaba hii imesheheni vitabu, journals na machapisho mbalimbali ambayo wanachama wake nchini Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanaweza kuyafikia na kujisomea.
View attachment 2088305
The Sokoine National Agricultural Library (SNAL)
Pamoja na uwepo wa maktaba kubwa ya kimataifa, chuo pia kina kumbi mpya na nzuri za mihadhara tofauti na zile nilizoziacha miaka ile. Kwa ujumla miundombinu na huduma za ufundishaji zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
View attachment 2088307
Kumbi mpya za mihadhara (MLT9 & 10)
Kwa ushirikiano na wenzangu waliosoma na ambao bado wanasoma kwenye chuo hiki kikongwe na maarufu, tutajitahidi kuwaletea upadates mbalimbali zinzohusu chuo kwa kadri itakavyowezekana. Samahani mods naomba uzi huu uwe pinned ili wadau waweze kuupata kwa urahisi.
Nawasilisha.
Pia soma:
Chuo cha Sokoine (SUA) chashika namba moja Tanzania (Citations)
Moja kati ya kazi kuu za chuo chochote duniani ni TAFITI. Chuo chochote hapa duniani kitaonekana bora kama kina wana sayansi (academicians) bora walio tuliza akili na kuandaa tafiti na ku publish tafiti zao kwenye juornal za kitaifa na kimataifa! Kwa kuongoza kwenye citation ni ishara wazi...www.jamiiforums.com
Ubora wa elimu unaotolewa SUA, UDOM na UDSM
Habarini za muda wana jamvii kama kichwaa cha habari kinavo jieleza hapo juu kuna tofauti gani wa ubora wa Elimu unaotolewa chuo kikuu cha kilimo morogoro SUA na ile inayotolewa chuo kikuu cha Dodoma UDOM & UDSM hususan katika zile course za kilimo? Binafsi nina wanangu wanasoma course zinazo...www.jamiiforums.com
Ok endelea kusomaNdio , ila Mimi bado naendelea kusoma na nipo Main huku.
3 years later [emoji16] am here,, though nimemaliza 2022Kuna aliyesoma forestry sua humu
Upepo mbaya, nadhani kama nchi pia tunapitia nyakati mbayaSUA SAIVI SIJUI INA SHIDA GANI KWA KWELI
Hii umepigaje mwana SUASO?3 years later [emoji16] am here,, though nimemaliza 2022