Umenikumbusha jambo kuna mhadhiri mmoja anaitwa Dr Sarwatt, (marehemu) alikuwa na motes zake kwenye daftari alizoandika miaka ya 70 lakini bado alikuwa anangangania kufundisha notes hizohizo. Yaani hadi daftari limegeuka kuwa rangi ya njano. Ni shida.
Pia kuna baadhi ya wahadhiri wavivu walikuwa wanaenda kwenye internet wanapakua notes na kuja kutubwagia kama zilizvyo na kutumezesha nzimanzima. Tumetoka mbali sana aisee [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Dr. Sarwat alinifundisha notes zake nazikumbuka (course iliyohusianana na animal science). Nadhani mwamba yeye alikuwa anatafuta pesa tu make alikuwa anapesa sana yuke mzee.
Mwingine aliyekuwa habadilishi notes (naye ni marehemu mwenyezi Mungu amuweke mahali pema) ni Dr./Prof. Msumari wa idara ya soil science, tena alikuwa anatuambia kabisa someni notes zangu msisome chochote kingine. Ila hii haikuwa nzuri kwa sababu unam-discourage mwanafunzi kusoma vitabu vingine ili apanue uelewa zaidi ya notes zako tu!

Kweli kabisa mkuu; marehemu Prof Msumari alikuwa strict kwenye somo lake la soil biology. Kuna siku alitutungia maswali ya T/F halafu majibu yote akaweka TRUE, nikapasua yote. Pia kuna Prof mmoja wa irrigation engineering anaitwa Prof Thadei, huyu naye notes zake ni zile za miaka ya 70; naye amekariri hizo hizo hawezi kubadilisha kitu. Tatizo syllabus ya SUA imeorodhesha tu mambo ambayo wanafunzi wanapaswa kufundishwa lakini haiendi deep zaidi kama zile syllabuses za vyuo vidogo. Kwa hiyo, lecturer anafundisha kile anachojua tu. Lecturers wanaweza wakawa wanafundisha somo hilo hilo lakini utakuta kila mmoja anafundisha vitu tofauti kabisa. Ushahidi ni katika somo la botany ambalo lilifundishwa na Prof Temu na Prof Minjas katika madarasa tofauti. Notes za Temu zilikuwa deep wakati zile za Minjas zilikuwa shallow and narrow.
Dr. Sarwat alinifundisha notes zake nazikumbuka (course iliyohusianana na animal science). Nadhani mwamba yeye alikuwa anatafuta pesa tu make alikuwa anapesa sana yuke mzee.
Exactly. Alikuwa mtoro sana chuoni na alikuwa anafundisha ovyo ovyo tu ilmradi kutimiza lengo. Muda mwingi alikuwa akihangaikia miradi yake ya kuingiza pesa ndefu.
Introduction
Nimeamua kuanzisha uzi huu mahsusi unaohusu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kama njia ya kukienzi chuo hiki kikongwe na cha kipekee nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Awali ya yote naomba ku declare interest kwamba mimi ni mhitimu kutoka SUA miaka mingi iliyopita wakati huo mfumo wa ufundishaji ukiwa wa Term System. Kwa sasa ufundishaji unafanyika kwa mfumo wa Semester System au ukipenda unaweza kuuita Mfumo wa Mwendokasi.
About the University
Kama jina la chuo linavyosadifu, chuo kilianzishwa kwa jitihada na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama njia ya kuzalisha wasomi kwenye fani ya kilimo (ukulima na ufugaji) mnamo mwaka 1984 na kupewa jina la aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, ndugu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kupata taarifa zaidi kuhusu SUA, tembelea tovuti rasmi ya chuo (Welcome to Sokoine University of Agriculture (SUA) )
Academics
Ili kufanikisha utoaji wa elimu kwa wanafunzi na wadau wengine, chuo kimegawanyika katika colleges 5 na deparments 6 (kwa mujibu wa tovuti ya chuo).
Mwaznoni chuo cha SUA kilijikita kwenye ufundishaji wa masuala ya kilimo tu na kutoa shahada kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor’s degree) na kuendelea mpaka shahada ya uzamivu (PhD) pamoja na kozi fupi lakini kwa sasa kinatoa hadi kozi za astashahada na cheti katika fani mbalimbali. Sasa hivi kinafundisha masuala mengi yakiwemo ualimu, maendeleo vijijini na mwasiliano (tazama kielelezo hapo chini). Kwa hiyo, hiki si chuo cha kilimo tu kama wengi wanavyodhani bali sasa hivi kinajikita kufundisha kozi mtambuka zinazofundishwa katika vyuo vingine vya kawaida.
Academic facilities
Mojawapo ya hazina ambayo chuo cha SUA kinajivunia ni uwepo wa maktaba kubwa ya kitaifa ya kilimo ijulikanayo kama The Sokoine National Agricultural Library (SNAL) iliyoanzishwa rasmi mwaka 1991. Maktaba hii imesheheni vitabu, journals na machapisho mbalimbali ambayo wanachama wake nchini Tanzania na nchi mbalimbali duniani wanaweza kuyafikia na kujisomea.
Pamoja na uwepo wa maktaba kubwa ya kimataifa, chuo pia kina kumbi mpya na nzuri za mihadhara tofauti na zile nilizoziacha miaka ile. Kwa ujumla miundombinu na huduma za ufundishaji zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa ushirikiano na wenzangu waliosoma na ambao bado wanasoma kwenye chuo hiki kikongwe na maarufu, tutajitahidi kuwaletea upadates mbalimbali zinzohusu chuo kwa kadri itakavyowezekana. Samahani mods naomba uzi huu uwe pinned ili wadau waweze kuupata kwa urahisi.
Moja kati ya kazi kuu za chuo chochote duniani ni TAFITI. Chuo chochote hapa duniani kitaonekana bora kama kina wana sayansi (academicians) bora walio tuliza akili na kuandaa tafiti na ku publish tafiti zao kwenye juornal za kitaifa na kimataifa! Kwa kuongoza kwenye citation ni ishara wazi...
Habarini za muda wana jamvii kama kichwaa cha habari kinavo jieleza hapo juu kuna tofauti gani wa ubora wa Elimu unaotolewa chuo kikuu cha kilimo morogoro SUA na ile inayotolewa chuo kikuu cha Dodoma UDOM & UDSM hususan katika zile course za kilimo? Binafsi nina wanangu wanasoma course zinazo...
Probably atakuwa kastaafu maana kipindi kile tulichosoma pale (zaidi ya miaka 20 iliyopita) umri ulikuwa umesogea sana. Hawezi akawa bado anaendelea kufundisha.
Probably atakuwa kastaafu maana kipindi kile tulichosoma pale (zaidi ya miaka 20 iliyopita) umri ulikuwa umesogea sana. Hawezi akawa bado anaendelea kufundisha.
Sijakuelewa vizuri mkuu. Ukisoma degree kwa mfano ya Veterinary Medicine unaweza kujiajiri mwenyewe kwa kuuza pembejeo za mifugo na kutibu. Kuna kozi nyingi zinatolewa SUA ambazo ukihitimu unajiajiri mwenyewe mkuu. Fuatilia vizuri kwenye mtandao.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.