Soma kisa hiki cha utapeli, ujifunze kitu

Soma kisa hiki cha utapeli, ujifunze kitu

Jamani yaan mashimo ya minara yachimbwe umbali gani huo kwamba kila mtu anachimba mashimo ya mnara mmoja halafu mpo watu 14 ina maana hiyo minara ipo 14 imekuwa nguzo za umeme au.
Ukishatapeliwa maswali kama haya ndo yanaleta maana, ila kabla ya kupigwa we utakua unawaza kuondoka na 80 yako hata uambiwe uchimbe wapi hutawaza
 
Aisee Kuna kisa kimoja Cha utapeli nikikumbuka hua nacheka sana, japo sio changu kilimtokea mshkaji wangu mmoja

Jamaa anadai walikua na kijiwe Chao wanakutana washkaji wengi tu, kulikua na pool table na vile vimashine vya kubet, anadai kijiwe kilikua na vijana wengi matozi tu na smart phone zilizoshiba....
Hii ni chai ya kijiweni
 
Aisee Kuna kisa kimoja Cha utapeli nikikumbuka hua nacheka sana, japo sio changu kilimtokea mshkaji wangu mmoja

Jamaa anadai walikua na kijiwe Chao wanakutana washkaji wengi tu, kulikua na pool table na vile vimashine vya kubet, anadai kijiwe kilikua na vijana wengi matozi tu na smart phone zilizoshiba.....
Mi napenda sana kusimuliwa visa kama hivi😆😆😆😆!

Lakini mkuu, namna ulivyosimulia kwa ufanisi, siye wewe kweli huyu uliyetapeliwa?

Maana sisi binadamu tukifanyiwaga visa, ni wachache sana hukiri madhaifu yao.

Wengi utasikia:..."kuna jamaa"..."kuna jamaa"...kumbe ni yeye alipigwa ama kut**bewa!
 
Waliibiwa kizembe kweli kuna la kujifunza kwanza usiwe na mazoea ya kuazimisha simu. Mfano mimi naweza kuwa sehemu mtu akaniomba simu apige kwa mtu...... Kama nina jero mfukoni nitampa akatie vocha kama sina basi utafuata masharti yangu huondoki mbele ya usawa wa macho yangu hutaki basi omba mwingine. Haka kamchezo kalishatokea kijiweni tena mtu tunayemjua kaomba simu apige kasepa nayo alafu alikua na plan za kuzamia kwa madiba basi akasepa ila hakufanikiwa akarudi kachoka sana aliemchukulia simu alimpa kipondo akaenda kulazwa mpka tukajua na siri yake kwamba ni muathirika.
 
Aisee nimecheka.....shimo uchimbe na simu imeenda 😂😂🙌
 
Mmh, yaani kila mmoja alipokuwa akimpa simu huyo mzee alikuwa akiendelea na shughuli ya kuchimba mashimo bila kuangalia mzee anaelekea wapi na simu yake? Kuna wingi wa chumvi kwenye mboga.
Labda wakiangalia pori hata wasiwasi wa kukimbiwa hawauoni..
 
Kisa hiki kinafanana na jamaa angu mmoja alikua anasoma ushirika...
Ye alikutana na jamaa kavaa suti amenyooka akampanga jamaa kuna project wanafanya inataka vijana 10 wenye laptop ambapo per day kila pc inalipwa 50k na anaetumia 15k..
Tapel akamwambia tafuta pc ata za kukod ambapo kila pc uliokod umwambie utampa 20k per day na jamaa ale 30k per pc..
Jamaa akachanganua 30k×10=300k per day project akaambiwa ni siku 5 akipiga maesabu yake akapata atakua na m1 na chenj..
Bc bhna jamaa akarudi chuo akaazima pc na tayari alikua ashapewa advance ya project yenyewe jamaa kwenye kuzunguka kwa masela zake akapata pc4 na yake ingekua ya 5 ...
Kesho yake jamaa akamtafuta uyo mshkaj akamwambia kapata pc tano akamwambia sawa amna shida leta pc nikaweke program za kufanyia kazi jamaa akampa tapel pc akapanda nazo gorofani jamaa alisubiri adi giza likamkuta jamaa hajaahuka
 
Japo story yako ni nzuri ila na wewe umetutapeli kama hao wazee tu .
1694056483173.jpg
 
Mmh, yaani kila mmoja alipokuwa akimpa simu huyo mzee alikuwa akiendelea na shughuli ya kuchimba mashimo bila kuangalia mzee anaelekea wapi na simu yake? Kuna wingi wa chumvi kwenye mboga.
Matapeli nadhani kuna mazingaombwe huyafanya ukiingia kwenye 18 zao.
 
shida ya watu wanatumia mazingira yao kutoa maoni, mtu anasema wanao bet hawana smart (hajatembea hata vijiwe vya mikoa jirani)

hao wazee wanaitwa kiboko ya mabishoo
 
Back
Top Bottom