Soma kwa makini: Dalili zinaonesha kuwa huenda mkataba wa bandari ukasababisha vifo vya watu

Emeritus Prof.Shivji,Warioba,kadinali Pengo,Padre Kitime wapo group gani hapo?
Pesa haina ndugu wala rafiki, haina tajiri wala masikini, haina kiongozi wa dini wala muumini, haina mkubwa wala mdogo, mzee wala kijana.

Nafikiri sio mara ya kwanza kusikia watu wameuwana kwa sababu ya pesa, tena wengine baba mmoja mama mmoja. Pesa unaweza kuuwa mtu afu ukaiba pesa zake na kwenda kutoa sadaka kanisani au msikitini na viongozi wataichukua.

Kwahiyo hata na wao wakitupiwa bahasha na wazee wa bandari ni vigumu kuikataa, asikudanganye mtu.
 
Bandari yenu au bandari ya wazee wa bandari 😂😂

Maana imekuwa kama Congo watu wanafundishwa shuleni kuwa nchi yao ina utajiri wa almasi, lkn 95% ya hao wakongo hawajui hata almasi yenyewe inafananaje na ina faida gani kwao na nchi. Ni 5% tu ndo wanaijua almasi na wanafaidika nayo, huku hiyo 95% wamekalia kufundishwa tu shuleni 🤣🤣
Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka bandari yetu tu.
 
Serikali ya ajabu sana hii. Kama watu hawataki mkataba si wauvunje kwann wanatumia nguvu kubwa kuwalazimisha watu.
Jisemee wewe na wanaokutumia Usitusemee sisi wajanja na wenye akili tuliokataa kutumiwa.
 
kundi lingine ni makanisa kupitisha vitu bure na wengine kuviuza kariakoo mnuu ku makufuli aliwahi kusema
 
bandari itapewa mwekezaji mtake msitake mlie msilie mlete udini au msilete mbwai na iwe mbwai muwekezaji atakuja tu, pigeni kelele kwa miaka mnayotaka muhimu sasa makufuli hatukanwi na chadema wamemsahau nyumbu wameelekea bandarini wooote kama vile wanavuka masai mara kuelekea kenya
 
Huu ndio ukweli wenyewe watu wamelamba pesa kutetea mafisadi uendeshaji wa bandari usibinafsishwe ila wameshashindwa.
 
Kwa lugha nyepesi CCM wameshindwa kuwadhiti wezi wa bandarini lakini kisewe kibali cha kuwaleta DPWORD kwa mikataba mibovu
 
Kwa lugha nyepesi CCM wameshindwa kuwadhiti wezi wa bandarini lakini kisewe kibali cha kuwaleta DPWORD kwa mikataba mibovu
Ni kama vile Chadema ilivyoshindwa kuzuia wezi wa ruzuku, hadi wanapokuwa na ishu ya kichama wanaamua kuchangisha wanachama.
 
Ni kama vile Chadema ilivyoshindwa kuzuia wezi wa ruzuku, hadi wanapokuwa na ishu ya kichama wanaamua kuchangisha wanachama.
Tunaishi kwenye jamii mfu ambayo haiwezi kuhoji kwa sauti inayosika na tabia ya unyumbu, ya tuliowapa dhamana (herding behavior of entrusted people), Herding behavior is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of group objectives, (conflict of interest), or (amygdala), fear of their leaders
 
Kwahiyo unashauri wanachadema waache unyumbu, waanze kujifunza kuhoji mapema zinapopelekwaga ruzuku za chama chao ili siku wakitawala nchi viongozi wao wasije wakaendeleza wizi wao serikalini?

Kama mawazo yako ni hayo basi sahau, kule watu ni kama wamerogwa tayari. Chochote kitachofanywa na kiongozi mkuu ndio hicho hicho, wew kama hutaki hama chama na utaundiwa genge la kuitwa msaliti, mnafiki nk.
 
Comments reserved
 
Kwahiyo mmeshajipanga kuua wakosoaji Kwa hivyo visingizio vyenu?
 
Kwahiyo mmeshajipanga kuua wakosoaji Kwa hivyo visingizio vyenu?
Umesoma vizuri uzi au umekimbilia tu comment kinyume na ujumbe wa uzi wenyewe, ili angalau na wewe upewe chochote na wazee wa bandari??

Kabla ya kutumwa unatakiwa ujue kwamba mambo ya kuuwa wapinzani hiyo sio style ya uongozi wa raisi Samia.
Hata hao waliokutuma hapa JF wanajua kama raisi Samia hana historia au utamaduni wa kuuwa wapinzani wake.

1. Historia yake kubwa ni kuruhusu uhuru wa kutoa maoni kwa kufuata sheria na mipaka ya uhuru huo.

2. Uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote vya siasa bila kujali kama kuna watu wanautumia huo uhuru kwa malengo yao binafsi.

3. Kumlipa Lisu mamilioni yake aliyosema anadai na kumruhusu kurudi nyumbani salama.

So style ya uongozi wake inafahamika, japo kuna watu ambao wamekuwa wakitumia ujinga wa baadhi ya watanzania wenzetu kutengeneza propaganda zao. Wakiamini kuwa hilo kundi la wajinga lipo hapa kwa ajili ya kutetea propaganda zao wanazoanzisha kama hivi.

Hata wewe leo hii unaweza kukaa ndani kwako unaangalia tv afu ukajifanya kuandika kwamba unatafutwa na polisi au watu wasiojulikana. Baada ya muda utaanza kuona watu wanavyotiririka kuitukana serikali kwamba unatafuta hadi raia wa kawaida na wakati kiuhalisia wewe mwenyewe rohoni unajua kwamba hautafutwi na mtu yoyote.

Za kuambiwa changanya na zako by Dr Jakaya Kikwete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…