kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,094
- 3,108
Habarini za uzima wakuu, poleni na majukumu yanayo wazonga, mungu atupiganie kwenye maradhi yeyote yale.
naombeni niwape story fupi kabisa ndeni mnipe ushauri kabla sijafanya maamuzi yangu binafsi ambayo yatatokana na mawazo yenu bora kabisa.
Mimi nilitolewa kijijini na shangazi yangu kuletwa mjini kwa ajili ya kusoma, nisema kweli wa mungu nilisoma kwa taabu sana, na kupitia kwenye hali ngumu sana ya maisha, nilikuwa napata kipigo kizito sana kutoka kwa huyu anti yangu mpaka nazilai (mpaka kuna siku nilikwenda kituo cha polisi kuomba wanisafirishe nirudi kwa mama yangu), akaja akawaambia polisi mimi ni muongo sana.
maisha yakasogea wakati nakaa nyumbani kwake huko mjini (jijini dsm), nikamaliza kidato cha nne..matokeo hayakutoka sawa, nikaingia kwenye vibarua vya kwenye makampuni ya waidi kufanya kazi kama kibaru huku nikizichanga (nilibahatika kupata pesa kwaajili ya ada ngazi ya certificate) nikasoma certificate nikiwa nakaa kwa rafiki yangu nikiwa nimekimbia kwa shangazi yangu yule
Hatimaye nilimaliza certificate, nikaingia kwenye kutafuta kazi kwa level yangu ya certificate sikubahatika kupata kazi ya kuajiliwa nikarudi kwenye kile kiwanda kama kibarua (kwa kuwa walikuwa wanajua utendaji wangu wa kazi haikuwa ngumu kunikataa) basi nikaanza kupiga kazi tena pale, mpaka nikapata ada ya diploma (hapa nililenga kwenda kusoma chuo cha serikali maana niliona ada ni nafuu sana) short the story nilisoma na kumaliza diploma, kwa level ya degree niliomba mkopo na nikapata asilimia 96% ya mkopo na kumaliza degree yangu ya kwanza.
tangu nimeondoka kwake moyo wangu umekuwa mzito sana kwenda hata kusalimia, yaani nikiwaza yale niliopitia kiukweli kabisa moyo wangu unakuwa mgumu sana, ila waswahili wanasema akutendea ubaya ana wema wake pia, huyu shangazi yangu kwenye mambo mawili alikuwa akinisaidia kabisa (matibabu ikitokea naumwa, hana uchoyo wa chakula kabisaa)
Baada ya kuhangaika kutafuta ajira sana baada ya kumaliza chuo (3 years pasipo kazi) hatimaye Mungu akaniona nikapata kazi japokuwa ni project ya muda flani tuu. nikajichanga kweli kweli sikutaka kupoteza hata sent tano kwenye mambo yasio na muhimu. Hatimaye nikaweza kupata pesa kiasi kadhaa, nikawa na mawazo mawili kichwani kwangu. (ntayaeleza hapo chini ayo mambo)
Mama yangu anakaa kijiji kwenye nyumba ya udongo bado anafanya kazi ya kuuza genge ambao mtaji haufiki ata elfu 50, mama yangu umri umeenda pia nguvu kazi imepungua upande wa huyu shangazi yangu anakaa mjini amepanga tu hana nyumba ana kiwanja tu uko chanika na umri wake umetembea sana, nguvu kazi imepungua sana kwake, biashara anazofanya ni hizi ndogo ndogo ambazo naona kwa sasa anatakiwa apumzike kiukweli.
Kuna mazuri ambayo nikiyawaza kwake (huyu shangazi yangu) nahisi natakiwa kumfanyia jambo ambalo linaweza kuwa jema kwake, uwezo wangu kipesa sio mzuri kabisa, sina kazi kwa sasa, niliwaza ivi wakuu: hapa nina milion 20 cash. nyumbani kwetu ni mwanza. niliplan nifanye ivi
1. hii pesa yote nikatafute nyumba ambayo ipo kwenye hali nzuri na eneo kubwa kwa kule mwanza niinunue baada ya kuinunua nimuambie shangazi yangu akakae pale apumzike, nimchukue na mama yangu pia akae pale apumzike, kuhusu ni jinsi gani nitawahudumia naamini kwa kudra za mwenyezi mungu nikipata kidogo tutagawana. (baada ya kununua nyumba mimi nianze upya (zero start) kwenye utafutaji kama mtoto wa kiume, na matokeo yatajulikana mbele ya safari uko)
2. Nichukue hii pesa nianze biashara na kujiweka katika hali nzuri ya uzalishaji wa kutafute pesa ya kufanya wazo kama ilo nililofikiria hapo juu. niliwaza kuingia kwenye biashara ya uber nikiwa mimi ndio mwenye chombo na mtafutaji pia na kufungua biashara zingine. ii mwisho wa siku niweze kufikia lengo la kupata pesa kwa ajili ya kufanya ilo wazo la hapo juu la kununua nyumba na kuwaweka awa wazazi wangu.
Karibu kwa ushauri wenu ndugu zangu. nitapokea kwa mikono miwili.
Note: kwa sasa kuna sehemu (DSM) nimepanga chumba kimoja, nikitafakari nafanya nini katika senario hii.
Karibuni.