Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
2,490
Reaction score
2,965
Wapendwa wanajf habari za usiku,

Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.

Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) na kushindwa kupata tempo nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga, tofali na tuition centre.

Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine basi niliamua kufanya biashara ya bodaboda.

Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh. 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilikuwa namfahamu lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafahamu sana.

Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa siku 10 pekee na muda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu, polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakini sioni matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaji katika maeneo ya mkoa niliopo.

Nawaza sana, nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo, Nimeamini hii dunia haina huruma.

Kuna muda nawaza ile hela bora ningeweka tu, kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nimebaki na kiasi cha laki 5 kwenye akaunti yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.

Kuna muda huwa nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa na njia rahisi ilivyoweza kupotea hii pesa, kuna muda niliona haya maisha hayana maana na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza hadi kuseparate na mtu wangu, Ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.

Muwe na usiku mwema.
 
Yani ulimpa deiwaka au mkataba?

Hukufunga tracker kwenye chombo?

Hamkupeleka mkataba serikali za mitaa ukasainiwe akiwa na mashahidi zake na picha zao wote passport?
Pole mkuu mimi ulitaka kunitokea mchezo kama huo, bahati nzuri nilimkamata boda wangu maeneo flani akiwa kajiachia vizuuri na boda langu, hapa tunaongea nimechukua boda na pesa yangu 400k+ ataitema, N.B tracker aliichomoa.
 
Mi nilichapwa 1M mzee baba na haikuwa yangu you can imagine nilikuwa na wakati mgumu kiasi gani
Kwenye harakati za utafutaji kupoteza ni sehemu ya maisha.

Jambo la msingi ni kupambana kupunguza risk za kupoteza.

Mimi nilifanya kazi za usiku, nikakusanya zaidi ya 1M nikaenda kulima mihogo huku Kibiti. Haikurudi hata 100.

So, ni kawaida tu.
 
Back
Top Bottom