Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Wapendwa wanajf habari za usiku.
Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.

Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) Na kushindwa kupata temple nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga,tofali na tuition centre.

Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine bas niliamua kufanya biashara ya bodaboda.

Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh1l 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilkua namfaham lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafaham sana.

Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa sku 10 pekee na mda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu,polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakin sion matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaj katika maeneo ya mkoa niliopo.

Nawaza sana ,nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo,. Nimeamini hii dunia haina huruma.

Kuna muda nawaza ile ela bola ningeweka tu ,kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nmebaki na kias cha laki 5 kwenye akaunt yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.

Kuna muda hua nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa ,na njia rahs ilivyoweza kupotea hii pesa,kuna muda niliona haya maisha hayana maana, na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza had kuseparate na mtu wangu ,ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.

Muwe na usiku mwema.
Pole sana kaka, tambua kuwa changamoto ni sehemu ya maisha. Kila jambo hutokea kwa sababu zake, usiogope, pia jifunze kupokea dissappointment; maisha yana mambo mengi sana.. na kimsingi dunia imejaa changamoto kuliko mtelezo.

Kuna watu wamepitia na wanapitia changamoto zaidi ya zako

Tambua ktk kutafuta kuna kuanguka na kuinuka, hasa ktk masuala ya fedha: unavyoingia katika mfumo wa biashara, kupata hasara au kufilisika ni jambo la kawaida sana.

Mwachie Mungu, endelea kupambana na utapata zaidi ya hiyo.

Mungu awe pamoja nawe
 
Kwenye harakati za utafutaji kupoteza ni sehemu ya maisha.

Jambo ka msingi ni kupambana kupunguza risk za kupoteza.

Mimi nilifanya kazi za usiku, nikakusanya zaidi ya 1M nikaenda kulima mihogo huku Kibiti. Haikurudi hata 100.

So, ni kawaida tu.
Wakati ule tunapayuka humu kuhusu kilimo cha mihogo ukaona tunademka eh😅!
 
Utafutaji ni vita, kuna kupigwa na kuna kupiga, ila mafanikio hayaji kwa kurudi nyuma na mpiganaji anayepigana vita kwa kurudi nyuma hajawahi kushinda vita,akirudi nyuma, karudi nyuma kujipanga na mapambano., pesa uliopoteza itumie kama funzo kwa kurekebisha ulipokosea na nini ukifanye ili kosa kama hilo lisije likatokea tena kwako.
 
Mkuu pole sana ila kukosea Ni kujifunza so don't give up. Naomba nikushauri pesa unayopata kwa muhanga au unayoitegemea usimpe mtu akutunzie au akuzalishie utakuja juta as long as bado unatafuta tumia muda wako kusimamia biashara zako mwenyewe,usimuamini mtu kwenye pesa sio Nabii, padri Wala shekhe wengi wetu dhaifu kwenye Jambo linalohusu pesa. Pole sana
 
Mkuu pole sana,Ila kukosea Ni kujifunza so don't give up,Naomba nikushauri pesa unayopata kwa muhanga au unayoitegemea usimpe mtu akutunzie au akuzalishie utakuja juta,as long as bado unatafuta tumia muda wako kusimamia biashara zako mwenyewe,usimuamini mtu kwenye pesa sio Nabii,padri Wala shekhe wengi wetu dhaifu kwenye Jambo linalohusu pesa.Pole sana
Asante sana mkuu
 
Utafutaji ni vita, kuna kupigwa na kuna kupiga, ila mafanikio hayaji kwa kurudi nyuma na mpiganaji anayepigana vita kwa kurudi nyuma hajawahi kushinda vita,akirudi nyuma, karudi nyuma kujipanga na mapambano., pesa uliopoteza itumie kama funzo kwa kurekebisha ulipokosea na nini ukifanye ili kosa kama hilo lisije likatokea tena kwako.
Asante sana
 
Mkuu,mazingira na muda haukuruhusu basi tu hata nikielezea ilivyokuwa ni kama maajabu yalipangwa kufanyika Siku hiyo.
Nairejesha taratibu lakini bado ni swala limefanya akili yangu isiwe sawa.
Pole sana mkuu. Huo mtihani wa marejesho ni mzito sana.
 
Mi nilichapwa 1M mzee baba na haikuwa yangu you can imagine nilikuwa na wakati mgumu kiasi gani
Mzee mimi nikiwa chuo nlichapwa zaidi ya mls 2 tena boom za watu kama sita. Halafu nilichapwa kibwege sana. Yani nilichukuliwa mpaka RB. Chuo ilikuwa ni shida nashukuru Mungu nliishi kwachale polisi hawakunikamata, Mungu akaja kunipa kazi nikiwa likzo ambayo likzo ya mwez niliingza kama mls 4 nikawalipa wote na chenj ikabaki nikarudi chuo nikiwa mnene.
Jamaa aliyeniingiza matatzon mpaka leo namwona yeye alishasahau ni mimi nishasahau ila alinifundisha kitu.
Ukiskia fursa ambayo ni too good to be true, jua siyo true
 
Ndondocha mkuu sikia, pole sana ila:-

1. Usijaribu kukatia tamaa usafiri wako. Kusanya details muhimu za huyo boda, kama vile namba yake ya simu aliyokuwa akitumia, taarifa za watu wake wachache ambao ulikuwa ukiwafahamu au kuwaona naye, kama kuna makubaliano yoyote ambayo mliandikishana hakikisha unatunza vizuri kabisa, meseji yoyote ya miamala au za kawaida za mara ya mwisho kuwasiliana naye hifadhi mkuu.

2. Piga hesabu kwa miezi yote ambayo alikuwa na usafiri wako mpka kufikia siku ya mwisho ambayo alitoweka ni kiasi gani jumla ambacho angetakiwa kurejesha, pia muda ambao umemtafuta na gharama zote ulizoingia ziongeze kwenye hiyo 1.8M.

3. Usiwategemee sana polisi, japo umefanya vema kutoa taarifa polisi ila hii kitu ifikirie wewe vizuri kabisa namna unavyoweza mkamata na hatakama ikija mbinu ambayo kwa wakati huu huna uwezo nao kuutekeleza iandike sehemu. Tengeneza list ya mbinu zote ambazo utaona zitakufaa kumpata. Kama ni muhamiaji, fuatilia wapi alipotokea in short kuwa na details kamili.

3. Baada kukusanya taarifa na kuandaa hizo mbinu zote, now relax na uendelee na maisha yako kama kawaida, yaani awepo kwenye target ila mfanyie kazi taratibu na uwe na nia ya dhati kabisa kumpata.

4. Piga mishe zako ila endelea kumsaka. Ipo siku utakutana naye na utapata pesa zako zote kiulaini.

5. Katika maisha ups and down hazikwepeki ila hizi zinazosababishwa na mwanadamu mwenzio huwa naona ni makusudi na siyo za kukaa na kulalamika sana we mtafute mtu wako akupe chako. Ila zile ups and downs ambazo zinatokea kwasababu ya natural calamities hizo ni kumuomba Mungu akuepushe nazo maisha yaendelee.

Hii mbinu nimeitumia na naendelea kuitumia na yeyote anayejaribu nidhulumu haki yangu huwa zinarudi na faida juu.

Mwaka 2019 nililima na jamaa shamba heka mbili maharage jamaa kwakuwa yeye ndiyo alikuwa anafanya kila kitu akaamua baada ya mavuno auze kila kitu kisha anipige chini. Na alifanya hivyo, aliuza kisha akaniblock namba zote na sikujua wapi alipo. Nilitumia mbinu hizo hapo juu ukiongeza na knowledge ya ki-intelijensia niliyonayo hatimae nilifanikiwa kumpata na hakutegemea.

Kama kawaida nilipiga hesabu zangu zote na alilipa mwaka huu January tena miamala alikuwa anafanya mwenyewe kwa simu yake.

Chako ni chako ukiamua kukipotezea kinapotea kweli ila ukitambua mateso na shida ulizopitia wakati wa kuzitafuta huwezi acha chako kipotee kiurahisi hivyo.

Mkuu pambania mali yako hii dunia ndogo sana ukipania kumtafuta mtu. Mwanadamu kuna namna ya kuishi naye, usimuamini mtu hata mmoja.

Kila la kheri boss.
 
Back
Top Bottom