Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Wapendwa wanajf habari za usiku,

Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.

Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) na kushindwa kupata temple nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga,tofali na tuition centre.

Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine bas niliamua kufanya biashara ya bodaboda.

Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh1l 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilkua namfaham lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafaham sana.

Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa sku 10 pekee na mda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu, polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakin sion matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaj katika maeneo ya mkoa niliopo.

Nawaza sana, nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo, Nimeamini hii dunia haina huruma.

Kuna muda nawaza ile ela bola ningeweka tu ,kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nmebaki na kias cha laki 5 kwenye akaunt yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.

Kuna muda hua nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa ,na njia rahs ilivyoweza kupotea hii pesa,kuna muda niliona haya maisha hayana maana, na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza had kuseparate na mtu wangu ,ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.

Muwe na usiku mwema.
We jamaa tukio Hilo linakwambia wewe bado sio mjasiriamali so inakubidi ujifunze ujasiriamali, inabidii uwende kidogo kidogo kwa hiyo pesa ulitakiwa kabla hujakusanya kufikia yote hiyo ungekuwa unaizungusha kwenye biashara ndogo ndogo na kuachana na hivyo vibarua na kubakia na tution center kabla hujakusanya yote hiyo. Boda boda ungenunua kwa hela ya kutokujichosha.
 
Pole sana mkuu umepoteza pikipiki ila nguvu, akili na maarifa bado unayo so usife moyo ndugu
Shukran
we jamaa tukio Hilo linakwambia wewe bado sio mjasiriamali ko inakubidi ujifunze ujasiriamali inabidii uwende kidogo kidogo kwa hiyo pesa ulitakiwa kabla hujakusanya kufikia yote hiyo ungekua unaizungusha kwenye biashara ndogo ndogo nakuachana na hivyo vibarua nakubakia na tution center kabla hujakusanya yote hiyo. Boda boda ungenunu kwa hela ya kutokujichosha.
Nimekuelewa, lkn unamaana nngeachana na shuguli zote zilizonipa hiyo ela then nibaki na moja?
 
Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi,nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Pole Sana Mungu akupe nguvu subira pia! Upate zingine zaidi ya hizo kwa njia nyepesi ambayo haukuitegemea! Kwa Mungu hakuna kubwa amini hivyo
 
Dunia nzuri Ila wanadamu wengi hawaaminiki, unajua saa yingine ukifikiria Ndungai alivyoSEMA vijana hawaaminiki tunakebehi Ila Ni ukweli kabisa, imagine mkasa Kama wa huyu bwana mdogo....Alie muamini kijana mwezake na kumpatia Akira ya boda, kilichotokea, vijana wengi wako hivyo.....hawana mitaji Ila wakisaidika tu watakuzunga na watakuacha njia panda
 
Wapendwa wanajf habari za usiku,

Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.

Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) na kushindwa kupata tempo nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga, tofali na tuition centre.

Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine basi niliamua kufanya biashara ya bodaboda.

Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh. 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilikua namfahamu lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafahamu sana.

Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa siku 10 pekee na muda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu, polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakin sioni matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaj katika maeneo ya mkoa niliopo.

Nawaza sana, nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo, Nimeamini hii dunia haina huruma.

Kuna muda nawaza ile hela bora ningeweka tu, kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nimebaki na kiasi cha laki 5 kwenye akaunti yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.

Kuna muda huwa nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa ,na njia rahisi ilivyoweza kupotea hii pesa, kuna muda niliona haya maisha hayana maana, na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza hadi kuseparate na mtu wangu ,ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.

Muwe na usiku mwema.
Pole sana mkuu najua inauma ila hakuna namna jipange kwa staili nyingine kikubwa uhai
 
Kumbe nilikuwa sahihu kumpokonya chombo yule jamaa, ila haya mambo ndiyo maana watu wanarogwa.
 
Haya ni mapito mkuu, muhimu uhai. Mwaka 2017 nilitapeliwa 10M Njombe, hapa nilidanganywa kwa ajili ya kilimo cha viazi lakini hela ikaliwa na sikupata chochote, na 2.2M na ndugu yangu wa karibu ambayo nilimtumia akanunulie shamba la miti lakini shamba sikupata mpaka muda huu naandika hapa.
Katika dunia ya sasa muamini Baba/Mama yako tu ndicho nilichofundishwa kupitia hii kadhia. Mungu ni mwema bado napambana mdogo mdogo na imebaki historia tu
 
Haya ni mapito mkuu, muhimu uhai. Mwaka 2017 nilitapeliwa 10M Njombe, hapa nilidanganywa kwa ajili ya kilimo cha viazi lakini hela ikaliwa na sikupata chochote, na 2.2M na ndugu yangu wa karibu ambayo nilimtumia akanunulie shamba la miti lakini shamba sikupata mpaka muda huu naandika hapa.
Katika dunia ya sasa muamini Baba/Mama yako tu ndicho nilichofundishwa kupitia hii kadhia. Mungu ni mwema bado napambana mdogo mdogo na imebaki historia tu
Muamini Baba na Mama??? Kwenye pesa?
 
Back
Top Bottom