Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Haya ni mapito mkuu, muhimu uhai. Mwaka 2017 nilitapeliwa 10M Njombe, hapa nilidanganywa kwa ajili ya kilimo cha viazi lakini hela ikaliwa na sikupata chochote, na 2.2M na ndugu yangu wa karibu ambayo nilimtumia akanunulie shamba la miti lakini shamba sikupata mpaka muda huu naandika hapa.
Katika dunia ya sasa muamini Baba/Mama yako tu ndicho nilichofundishwa kupitia hii kadhia. Mungu ni mwema bado napambana mdogo mdogo na imebaki historia tu
Muamini Baba na Mama??? Kwenye pesa?
 
Mkuu km una lak tan chez na chart tu ndani ya wik pesa yako inarud
 
Dunia nzuri Ila wanadamu wengi hawaaminiki,unajua sanyingine ukifikiria ndungai alivyo SEMA vijana hawaaminiki tuna kebei Ila Ni ukweli kabisa,imagine mkasa Kama wa huyu bwana mdogo....Alie muamini kijana mwezake na kumpatia Akira ya boda,kilicho tokea,vijana wengi wako hivyo.....hawana mitaji Ila wakisaidika tu watakuzunga na watakuacha njia panda
Sahihi, huruma imeniponza pia
 
Wapendwa wanajf habari za usiku,

Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.

Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) na kushindwa kupata tempo nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga, tofali na tuition centre.

Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine basi niliamua kufanya biashara ya bodaboda.

Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh. 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilikua namfahamu lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafahamu sana.

Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa siku 10 pekee na muda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu, polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakin sioni matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaj katika maeneo ya mkoa niliopo.

Nawaza sana, nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo, Nimeamini hii dunia haina huruma.

Kuna muda nawaza ile hela bora ningeweka tu, kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nimebaki na kiasi cha laki 5 kwenye akaunti yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.

Kuna muda huwa nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa ,na njia rahisi ilivyoweza kupotea hii pesa, kuna muda niliona haya maisha hayana maana, na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza hadi kuseparate na mtu wangu ,ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.

Muwe na usiku mwema.
Hizi zikiondoka hazipatikani, wanapeleka ziwa Victoria machine inafungwa kwenye boti za uvuvi vifaa vingine wanauza
 
Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi, nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Milioni 6.
Tofali 800= 800000
Cement 10= 150000
Mchanga = 150000
Nondo= 150000
Bati = 500000
Madirisha manne = 800000
Mbao = 300000
Ufundi = 500000
Chumba na sebule umehamia na chenji
 
Simama. Nenda kwenye kioo kikubwa. Jiangalie kwa muda. Tabasamu... sema kwa sauti.. asante Mungu mimi bado mzima na nina afya tele na mikono yangu na akili zangu ni timamu. Nitie nguvu Mungu wangu.... nasonga mbele na wewe utanipigania na ninaamini nitapata zaidi ya hizi nilizotapeliwa.
Jivike ujasiri... jisahaulishe yaliyopita... anza kupanga mipango mipya ya kujikwamua kwa imani.
Usiendelee kuwaza na kuumia sana.... utauumiza moyo na hutaweza kuutibu! Songa mbele.
 
Nimecheka asee eti maisha hayana huruma, afu umetanguliza pesa mbele sana huwezi kujua labda mshikaji kadei, muwazie na mchizi kidogo.
 
Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi, nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Hivi inakuagaje paka unaibiwa pesa yote hii?
 
Nikirudi home madogo wanapenda sana kuniambia broo nunua pikipiki tukuletee hela. Nawaambia madogo mm sina kitu naunga unga maisha tu. Story zikinoga wanaanza kusimulia jinsi wanavyowaibia mabosi pikipiki wanazopewa mkataba. Ndio nikajisemea bora nifungue goli niuze matunda tu. Kiufupi usimpe kazi mtu ambaye sio mkeo, mwanao au mumeo
 
Simama. Nenda kwenye kioo kikubwa. Jiangalie kwa muda. Tabasamu... sema kwa sauti.. asante Mungu mimi bado mzima na nina afya tele na mikono yangu na akili zangu ni timamu. Nitie nguvu Mungu wangu.... nasonga mbele na wewe utanipigania na ninaamini nitapata zaidi ya hizi nilizotapeliwa.
Jivike ujasiri... jisahaulishe yaliyopita... anza kupanga mipango mipya ya kujikwamua kwa imani.
Usiendelee kuwaza na kuumia sana.... utauumiza moyo na hutaweza kuutibu! Songa mbele.
Time healing
 
Milioni 6.
Tofali 800= 800000
Cement 10= 150000
Mchanga = 150000
Nondo= 150000
Bati = 500000
Madirisha manne = 800000
Mbao = 300000
Ufundi = 500000
Chumba na sebule umehamia na chenji
We jamaa
 
Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi, nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Unapandaje daladala na 6.4? Ungechukua usafiri mwingine. Na huko kwenye daladala ulisinzia au ilikuwaje?

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom