Soma upate mawili matatu: Mhitimu mambo ninayopitia kipindi hiki katika harakati zangu

Soma upate mawili matatu: Mhitimu mambo ninayopitia kipindi hiki katika harakati zangu

Ona hii kunguni!!!!!

Nyie ndo wale mnaokaa mnasubiri miujiza!! Mkuu labda tu nikwambie,NILIANZA KUTOAMINI KATIKA VITU KAMA NYOTA, MIUJIZA, SIJUI BAHATI nikiwa chuo Baada ya kuanza Kusoma vitabu, nikakutana na hii statement iliyobadilisha maisha, naomba kkunukuu

"There is a law of cause and effect. Nothing happens by chance or miracle. Every thing that happens has it's cause. Even those things you see as miracles it is because their causes are beyond your understanding and consciousness. So if you want something to happen, make sure you you cause them to happen, and those who will see the results to your causes will consider you to be lucky"


Mkuu ujue kuwa nilijichanga Sana na Yale maboom, nilikuwa naishi maisha Yale kuonekana HUNA SWAGA, nimekula Sana mihogo ili tu nisave hela. Hivi unapoambiwa kujichanga unaelewa??
hk ktabu chenye hii quote inaonesha n kizur vipi kinaitwaje waweza share softcopy yake humu?
 
Nikifikiriaga maisha ya chuo, najiona nilicheza Kama pele. Sijawahi kuonja hata sek 1 ya u-jobless. Nimefika tu home (mkoani kwa broo alipokuwepo, siku hiyo hiyo nikakabidhiwa mradi tuliouanzisha kwa pamoja kipindi nipo miezi ya mwisho mwisho ya chuo, nikaanza kazi siku hiyo hiyo, Hadi Leo mm ndo CEO, MANAGER, MSIMAMIZI, n.k wa mradi huo.

Sitafuti hela ya kula, bali hela ya kupiga hatua kimaisha.

Kula, kulala, kuvaa na bill Kama Kodi, umeme n.k Ni uhakika nabaki nasotea hela ya kupiga hatua kimaisha.

Asante Mungu Mkuu
Sasa huko ni kujisifu wewe,, punguza sifa
 
Habari yenu wanaJF

Poleni na Majukumu ya kila siku, Leo nimekuja kusimulia mawili matatu nayopitia katika harakati zangu nishare nanyi ndugu zangu.

Wanajf mimi Ni muhitimu wa BSc Education, kama post zangu nyingi zilivyojieleza huko nyuma. Nilihitimu mwaka 2019 November, nilijaribu walau Kuomba tempo katika sekondari mbalimbali hapa mjini Songea lakini sikufanikiwa kupata kwa wakati ule, (labda kwavile Sikua hata na vyeti vya Masomo yangu).

Nilifanikiwa kufungua tuition centre ya Muda wa Likizo December, Nilifanikiwa kupata wanafunzi wa kutosha kwa Kipindi kile ikizingatia nilifanya promotion ya kutosha, mwaka 2020 niliendelea kufundisha tuition centre mbalimbali Nikipata kipato walau cha kununulia mswaki na matumizi mbalimbali, niliweza kufundisha hata Watoto wa Wakubwa wa Mkoa majumbani Mwao.

Muda wa Likizo ya corona nilijichanganya katika kazi ngumu ya kuopoa na kuchimba mchanga kwasababu hata tuition hazikuruhusiwa tena, ilibidi nijivue kutoka mwalimu hadi mchimba mchanga, ni muda ambao nimejifunza mengi sana na nimekutana na wengi sana.

Ipo siku ambayo Nilipata mteja wa mchanga ambaye alikuja kuchukua mchanga kwa tractor ukizingatia tractor haliwezi kubinua ilibidi nichukue Buku ya kushushia mwenyewe, nilipokua nikishusha nyumbani kwa boss nilishangazwa kuona naitwa "teacher" na msichana Mdogo aliyetokea ndani kwa boss Ni mtoto wa boss, nilishusha mzura hadi machoni nikijua atahisi kanifananisha lakini aliita tena kwa msisitizo,.

Hakuamini kuniona pale, Mzee wake alishangaa kuitwa vile, Nilimwambia hujambo Dogo, nikachukua changu nikatembea.

Ipo siku nilipeleka mchanga site nilishangaa kukutana na headmaster wa Shule fulani niliyofanyia field akiwa ndio muhusika inabidi anipatie Pesa, nilifanya maujanja hatimaye hakuweza Nitambua.

Nilikua napakia mchanga wa mwenzangu sikumoja ( nipate 2000 ta haraka) nilishangaa boss akiletwa na bodaboda ambaye nilikua nikimkimbizia Mathematics O-level, alishangaa aliniita mkuu vipi tena? Nilipandisha mzura nikamtazama Nikamwambia Tutaongea boss.

Leo hii nimepeleka mchanga sehemu nimeshangaa kukuta fundi Mkuu ni Dogo aliecha Shule miaka ile akiwa pale sekondari, aliniuliza Bro Upo Huku sikuhizi, Nilimwambia ndio Nipe Dili hizo Niishi.

Kuna MUDA inanibidi niulize kati ya form four tuliohitimu Pamoja hivi nani ni dereva ili walau AKIPATA trip za mchanga anikumbuke na Mimi.

Unajua HAYA maisha hayana huruma, unakuta sometimes unachimba mchanga na Mzee wangu labda mnauza mnapata 50 ,000 Ila unamwambia Basi Mzee Wewe Chukua 20000 mimi Nibaki na 30000 kwa sababu mimi bado najipanga kimaisha, lakini Mzee anakaza anataka 50% anakwambia yeye ndio kaleta gari, no way utafanyaje Sasa.

Maisha yana mengi sana ya kujifunza, unajua ukishamaliza Chuo kama hivi home nako wanajua unaenda kuajiriwa soon, Kuna Muda unamwambia Mzee nipatie hizi Mbao nikachonge kitanda anakwambia Je ukipangiwa kazi Mwanza utaenda nacho? Sasa najiulizaga na nisipopangiwa Mzee itakuaje?

Wazazi wengi wetu wanaamini WANAO tutaajiriwa, yaa Ni kweli, lakini mtuwezeshe PIA kwa Kipindi hiki ambacho hatuna KITU,.

Hakuna mtu asiyependa goodlife, "we need money to go, to do our family matters".

Wanajf kama umefanikiwa usimcheke asiefanikiwa, kama unauwezo basi muwezeshe, kwa kazi nazopiga mtu mwingine mwenye degree kama mimi anaweza kataa kabisa akiona ni kujidharirisha, lakini Naamini mafanikio hayana SIRI.

Naamini katika kusubiri million basi unapaswa utafute Buku.

Unaweza teseka DUNIANI na mbinguni PIA.
Ni Mimi Ndondocha mkuu.

Karibuni kwa mchanga mgumu Songea

0738853634
View attachment 1492611
Umeandika kwa hisia sana mkuu walioshiba hawawezi kukuelewa unless wawe wamepita kwenye njia hizi, penye nia pana njia
 
Hivi nyie huwa mnaongelea jamii za aina gani? Ujue kuna mambo ukiyajua uhalisia wake huwezi kusema kitu kama hii, unataka kuniambia kuwa jamaa hana Focus kweli?
Unaujua msoto mkuu?,yani unataka jamaa afocus katika kuanzisha may be shule yake wakati huo awe anakufa njaa mtaa eti kisa tu yeye kafocus katika kuanzisha shule ambayo hajui hata pesa ya dawati moja ataipata lini na wakati huo inampasa akatafute pesa ya kula,n.k.

Acha Mwamba ajichange pesa za kujikimu maisha yake kwanza then hayo mambo ya FOCUS yatakuja baadae.

unataka kusema mimi siujui huo msoto? Majina yangu yapo hapo waweza nifuatilia popote ili ujue
 
ndugu sikupi pole bali nakupa pongezi maana ni heri wewe ambae unajishulisha na chochote. wako wtu kama wewe hawajathubutu kufanya aina ya kazi kama hio ufanyayo kwa sababu za aibu au maswali kama hayo eti mimi na digree yangu siwezi kulima ama kuchimba mchanga!
nakuhakikishia utafika mbali mkuu kwa kiasi usichodhania, Mungu awe mbele yako.
 
Vema umejua mafanikio yanapitia baadhi ya michakato ndiyo maana walioishia darasa la Saba wanaanza kupitia michakato mbalimbali hadi yule waliesoma nae kama alienda chuo lazima amkute std seven ameshapitia challenge nyingi na inakuwa kawaida kwake kuelekea mafanikio sa we graduate ndo kuanza unaanza hatua moja unakuta mwenzako Yuko ya tano nakuendelea, ukileta lelema kuitegemea elimu darasa lazima kimafanikio uchemshe. Mafanikio ni mchakato tulijue Hilo.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pambana mkuu,
nasemaga kuna wakati mtu anakutafuta anakwambia umtumie hata buku 3.
Kama iko ndani ya uwezo wako aisee wee msaidie hujui kabanwa kiasi gani.
Muhimu Ubadili hilo jina pia mkuu si zuri. Kuna mada ilishaga letwa inasema mara nyingi ukichunguza majina tuliyojipa humu hatujajiita kwa bahati mbaya. Hata wewe chunguza, hili liko kisaikolojia na kiroho hivi. Niko serious hilo jina badili.
 
Pambana mkuu,
nasemaga kuna wakati mtu anakutafuta anakwambia umtumie hata buku 3.
Kama iko ndani ya uwezo wako aisee wee msaidie hujui kabanwa kiasi gani.
Muhimu Ubadili hilo jina pia mkuu si zuri. Kuna mada ilishaga letwa inasema mara nyingi ukichunguza majina tuliyojipa humu hatujajiita kwa bahati mbaya. Hata wewe chunguza, hili liko kisaikolojia na kiroho hivi. Niko serious hilo jina badili.
Sawa mkuu
 
Vema umejua mafanikio yanapitia baadhi ya michakato ndiyo maana walioishia darasa la Saba wanaanza kupitia michakato mbalimbali hadi yule waliesoma nae kama alienda chuo lazima amkute std seven ameshapitia challenge nyingi na inakuwa kawaida kwake kuelekea mafanikio sa we graduate ndo kuanza unaanza hatua moja unakuta mwenzako Yuko ya tano nakuendelea, ukileta lelema kuitegemea elimu darasa lazima kimafanikio uchemshe. Mafanikio ni mchakato tulijue Hilo.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huna Focus, hilo tuu ndilo linalowaumiza vijana wengi wa Kiafrika. Siku ukiwa na Focus maisha yatakunyookea, usipokuwa na Focus maisha yatakupeleka peleka yatakavyo
Hebu mfundishe wewe mwenye focus. Amekwambia alikuwa anafundisha tuition baada ya tuition kuzuiwa akaamua aingie kwenye mchanga.

Ulitaka aje kula kwenu? Usiongee mambo kirahisi rahisi.



Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Chief
Ww ni Msomi,nakupa hongera kwa maamuzi uliyochukua,najua unapita katika kipindi kigumu,ila nakupa bishara njema...si muda utatoboa
Mwanzo ulikaa darasani na kucheza na wino pamoja na karatasi,
Sasa upo katika darasa la maisha,hapa unajengwa ukomavu na kujitambua

Ninahakika
Watt wako utakaowapata,utawajengea mazingira mazuri ya kutotegemea ajira
Wazazi wetu weeengi hawakusoma,wakati wanatusomesha sisi,kauli mbiu yao ni ajira ajira ajira....Walikuwa hawajui wanachokisema hususan kulingana na zama hizi tulizonazo
Au kwa ufupi,hawakusoma alama za nyakati na hawakuwa na macho yenye uwezo wa kutoboa ukuta

Big Up Chief
Pambana....Usijilaumu wala kulaumu mtu,Bali fahamu upo katika mafunzo ya ziada katika maisha

Barikiwa sana Chief
 
Back
Top Bottom