Soma upate mawili matatu: Mhitimu mambo ninayopitia kipindi hiki katika harakati zangu

hk ktabu chenye hii quote inaonesha n kizur vipi kinaitwaje waweza share softcopy yake humu?
 
Sasa huko ni kujisifu wewe,, punguza sifa
 
Umeandika kwa hisia sana mkuu walioshiba hawawezi kukuelewa unless wawe wamepita kwenye njia hizi, penye nia pana njia
 

unataka kusema mimi siujui huo msoto? Majina yangu yapo hapo waweza nifuatilia popote ili ujue
 
ndugu sikupi pole bali nakupa pongezi maana ni heri wewe ambae unajishulisha na chochote. wako wtu kama wewe hawajathubutu kufanya aina ya kazi kama hio ufanyayo kwa sababu za aibu au maswali kama hayo eti mimi na digree yangu siwezi kulima ama kuchimba mchanga!
nakuhakikishia utafika mbali mkuu kwa kiasi usichodhania, Mungu awe mbele yako.
 
Vema umejua mafanikio yanapitia baadhi ya michakato ndiyo maana walioishia darasa la Saba wanaanza kupitia michakato mbalimbali hadi yule waliesoma nae kama alienda chuo lazima amkute std seven ameshapitia challenge nyingi na inakuwa kawaida kwake kuelekea mafanikio sa we graduate ndo kuanza unaanza hatua moja unakuta mwenzako Yuko ya tano nakuendelea, ukileta lelema kuitegemea elimu darasa lazima kimafanikio uchemshe. Mafanikio ni mchakato tulijue Hilo.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pambana mkuu,
nasemaga kuna wakati mtu anakutafuta anakwambia umtumie hata buku 3.
Kama iko ndani ya uwezo wako aisee wee msaidie hujui kabanwa kiasi gani.
Muhimu Ubadili hilo jina pia mkuu si zuri. Kuna mada ilishaga letwa inasema mara nyingi ukichunguza majina tuliyojipa humu hatujajiita kwa bahati mbaya. Hata wewe chunguza, hili liko kisaikolojia na kiroho hivi. Niko serious hilo jina badili.
 
Sawa mkuu
 
 
Huna Focus, hilo tuu ndilo linalowaumiza vijana wengi wa Kiafrika. Siku ukiwa na Focus maisha yatakunyookea, usipokuwa na Focus maisha yatakupeleka peleka yatakavyo
Hebu mfundishe wewe mwenye focus. Amekwambia alikuwa anafundisha tuition baada ya tuition kuzuiwa akaamua aingie kwenye mchanga.

Ulitaka aje kula kwenu? Usiongee mambo kirahisi rahisi.



Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Chief
Ww ni Msomi,nakupa hongera kwa maamuzi uliyochukua,najua unapita katika kipindi kigumu,ila nakupa bishara njema...si muda utatoboa
Mwanzo ulikaa darasani na kucheza na wino pamoja na karatasi,
Sasa upo katika darasa la maisha,hapa unajengwa ukomavu na kujitambua

Ninahakika
Watt wako utakaowapata,utawajengea mazingira mazuri ya kutotegemea ajira
Wazazi wetu weeengi hawakusoma,wakati wanatusomesha sisi,kauli mbiu yao ni ajira ajira ajira....Walikuwa hawajui wanachokisema hususan kulingana na zama hizi tulizonazo
Au kwa ufupi,hawakusoma alama za nyakati na hawakuwa na macho yenye uwezo wa kutoboa ukuta

Big Up Chief
Pambana....Usijilaumu wala kulaumu mtu,Bali fahamu upo katika mafunzo ya ziada katika maisha

Barikiwa sana Chief
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…