Soma upate mawili matatu: Mhitimu mambo ninayopitia kipindi hiki katika harakati zangu

Shukran sana mkuu
 
.
 
Pole sana kiongozi. Tulio wengi humu hizo nyakati tumepitia sana. Kwanza nikuondoe hofu, usijione mpweke kuna wakati Mungu anakupitisha katika mambo magumu ili upate cha kujifunza.

Mimi ishu yangu imetofautiana kidogo na wewe ila nimewahi pitia hizo nyakati ngumu pengine ni zaidi ya ulizopitia wewe.

Mimi nikuwa mwajiriwa serikalini...(Mwalimu wa sekondari) nilifanya kazi nikiwa na malengo niliojiwekea. Mungu alinifanikisha nikaanza kuishi katika ndoto zangu. Nilifanikiwa kufungua biashara kadhaa huku nikiendelee na kazi yangu. Hivyo ikafika wakati uchumi wangu ukaanza kuimarika.

Sasa kama unavyojua mazingira ya kazi ya uwalimu walio wengi wanaishi maisha ya kutegemea mwisho wa mwezi ndio wavimbe...sasa mnyamwezi navimba everyday jambo ambalo liliwafanya baadhi ya staff wenzangu kujiona wao ni wajinga maana mtu nilie wakuta kazini nawazidi maendeleo tena kwa kiasi kikubwa mno.
Kama unavyowajua walimwengu, choko choko zikaanza...nikaanza kutengenezewa zengwe za kila aina, ikafika hatua siifurahii tena kazi yangu.

Ikafika hatua kila mtu ni adui yangu nikiangalia sioni nilipowakosea. Nikaanza kutengwa...nikifika kazini stress zinakuwa nyingi mpaka headmaster akawa adui namba moja.

Mkuu kumbuka kipindi chote hicho nafanya kazi town hivyo mambo yangu yanasogea. Ikafika wakati tikanunua kagari kangu nikajiongeza nikawa napiga na ishu za u MC ndio mambo yakazidi kuwa bull bull upande wangu financially..jina likawa kuwa kuliko mwili wangu kichwa kikaongezeka upana.

Basi walipoona hawana pa kunishinda wakaanza kuuunda chokochoko ili nihamishwe nipelekwe chaka..huwezi amini jitihada zao zikafanikiwa.

Nikahamishwa nikapelekwa chaka hilo ambapo ningeahindwa kabisa kendesha mambo yangu ukizingatia shughuli zangu zote nilikuwa nazifanyia town.

Ikanibidi nifanye maamuzi magumu ya kuchagua kimoja ili niemdelee na maisha yangu. Nikajilipua nikachagua bisahara niachane na kazi ya kuchezea chaki.

Hapa ndipo mambo yalianza kubadilika. Mpaka leo sijawahi kujua kea nini niliporomoka kwa kasi kiasi kile. Miaka Miwili nilikuwa nimeshafilisika nimefunga biashara zangu zote...nikawa sipati tena deals za u MC, gari ilikuja kupata ajali ikaumia vibaya sana nikaiuza kwa bei ya hasara...kuanzia mwaka 2016 - 2018. Nimeishi kwa mateso makubwa sana...hiki ndio kipindi niliweza kutofautisha marafiki wa kweli na wanafki...idadi kubwa ya marafiki niliokuwa nao kipindi hicho nina kitu walikimbia.

Nimefanyakazi za kila aina. Nimeosha magari, nimeuza viatu vya mtumba, nimekuwa kibarua kwa fundi ujenzi, nimekuwa bodaboda...yn nimepiga kazi za kila aina ili kuhakikisha napata ugari wangu wa kila siku.

Ishu iliyokuja kunirudisha kwenye reli, nilikuja kujiingiza kwenye ishu ya udalali wa vyumba, nyumba na mashamba 2018 mwezi november nikapiga dili moja matata nikapata commission ya kama 15M...Mungu hamtupi mja wake[emoji120]

Ndio nikarudi katika ishu zangu za biashara...now namshukuru Mungu nipo pazuri kuliko hata nilivyokuwa mwanzo, lkn naishi kwa taadhari kubwa nikiamini kwamba kwenye maisha lolote linaweza kutokea hivyo nivyema kujiimarisha mapema pia sio kila mtu anafurahia maisha uliyonayo hata kama unamsaidia ila anatamani hapo ulipo ushuke uwe chini zaidi yake.

Wale wote walionicheka na kunidharau kipindi na henyeka now nikikutana nao wanajisikia aibu kubwa...wanaishia kuniita mpambanaji ila kwa namna yoyote sijui ni kitu gani kitanirudisha nikawe mwajiriwa tena sidhani.

Pole sana mkuu huu wakati ulio nao uchukulie kama darasa kwako.
 
Mkuu ulikosea sana kuacha ajira aiseh.....naamini hukohuko bush ungefanya maajabu ya mifugo na kilimo wakabaki kushangaa......tunajifunza kutokana na makosa.....
 
Asante sana mkuu
 

Mdomo huumba! Badilisha jina mkuu. [emoji23][emoji23]
 
Ni hatari sana mkuu
 
Sahh
 
Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…