Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WATU MASHUHURI KATIKA UHURU WA TANGANYIKA
Vitabu hivi vina historia ya kusisimua ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika katika chama cha TANU lakini historia imewasahau.
Ukianza kufungua ukurasa wa kwanza hutokiweka chini hadi umemaliza kukisoma.
Soma mazungumzo ya Tewa Said Tewa na Abdul Sykes usiku wa tarehe 16 April 1953 kuamkia siku ya uchaguzi wa Rais wa TAA Ukumbi wa Arnautoglo kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere.
Abdul kidogo alikuwa na hofu ya kukikabidhi chama kwa mtu ambae hawamjui vizuri sana.
Soma mkutano wa siri wa mkakati wa kuwashinda wapinzani wa Kura Tatu, Sheikh Suleiman Takadir, Zuberi Mtemvu na wengineo uliofanyika Tanga mwaka wa 1958 baina ya Sheikh Rashid Sembe, Hamisi Kheri na Julius Nyerere.
Soma historia ya Zuberi Mtemvu alivyohama TANU kuunda chama cha Congress kupinga Kura Tatu.
Haya ni katika kitabu cha kwanza.
Kitabu cha pili utamsoma Peter Mhando ambae baada ya kufanikiwa kuunda TANU Tanga alipewa uhamisho kwenda TANU Makao Makuu kuongeza nguvu.
Peter Mhando ndiye aliyeshauri Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka 1958 uliojadili Kura Tatu ufanyike Tabora.
Msome Salum Mpunga kutoka Lindi aliyekuja Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa TANU wa kwanza Hindu Mandal Hall mwaka 1955.
Salum Mpunga ndiye aliyemwingiza Julius Nyerere na TANU Southern Province kulikokuwa na upinzani mkubwa wa TANU kwa kuwatia hofu wananchi kuwa TANU inatayarisha vita vingine vya Maji Maji dhidi ya Waingereza.
Soma utambue ni nani walikuwa wanaeneza fitna na propaganda hii dhidi ya ukombozi wa Tanganyika.
Soma pia historia ya mzalendo mwenzake Yusuf Chembera waliokuwa pamoja katika kuineza TANU kusini na kupigania uhuru wa Tanganyika.