Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
..Obote alirudi madarakani baada ya uchaguzi mkuu.
..Museveni hakukubaliana na matokeo hivyo akaingia msituni.
..sio kweli kwamba Obote alirudi kwa mbinu za Nyerere au Tanzania.
..nakushauri ujisomee kuhusu Moshi Accord ambayo ni mazungumzo na makubaliano ya makundi ya Waganda kuunda serikali ya mpito baada ya Iddi Amin kupinduliwa.
..mazungumzo hayo yalifanyika mjini Moshi Kilimanjaro na yalikuwa Mzee Mkapa akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa mwenyeji wao.
..Mazungumzo hayo yalizaa serikali ya mpito chini ya Prof.Yussuf Kironde Lule. Baada ya hapo akaingia Godfrey Lukongwa Binaisa. Huyo naye hakudumu akaja Paulo Muwanga.
..Baada ya uchaguzi mkuu wa vyama vingi ndio Milton Obote akarudi madarakani.
Asante kwa kulifafanua hilo [emoji120][emoji120]