Somalia yawafukuza wanadiplomasia wote wa Kenya, yafunga ubalozi wake nchini Kenya

Somalia yawafukuza wanadiplomasia wote wa Kenya, yafunga ubalozi wake nchini Kenya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Serikali ya Somalia imetangaza kusitisha uhusiano wake na Kenya ikidai kwamba Serikali ya Kenya inaingilia kati masuala yake ya ndani.

Nchi hiyo jirani wa Kenya, imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wote wa Kenya na kuagiza wanadiplomasia wake wote walio Nairobi kurudi Mogadishu ndani ya siku saba kuanzia leo jumanne Desemba 15 2020.

Waziri wa habari wa Somalia Osman Abukar Dubbe, amesema katika hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja na televisheni ya serikali ya Somalia Jumatatu jioni kwamba hatua hiyo imechukuliwa kujibu uchokozi wa kisiasa wa kila mara unaofanywa na serikali ya Kenya kinyume na uhuru wa Somalia.

Serikali ya Kenya haijajibu madai wala hatua hiyo ya Somalia.

Somalia ilimuondoa Balozi wake nchini Kenya Novemba 29 na kuamuru balozi wa Kenya kuondoka Mogadishu.

Wakati huo, Somalia iliishutumu Kenya kwa kuingilia kati maswala yake ya ndani na siasa za nchi hiyo.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari, Somalia ilidai kwamba Kenya ilikuwa “inamshinkiza kisiasa” kiongozi wa eneo la Somali Ahmed Mohamed Islam maarufu kama Ahmed Madobe wa Jubaland, ili kutimiza malengo yake ya kisiasa na kichumi ndani ya Somalia.

Somalia inadai kwamba kutokana na ushawishi wa Kenya, Ahmed Madobe alilegeza msimamo wake kuhusu mkataba wa Septemba 17, kati ya serikali kuu na viongozi wa maeneo.

Mkataba huo ulikuwa wa kutoa fursa ya kufanyika uchaguzi usio wa moja kwa moja nchini Somalia lakini kiongozi wa Jubaland sasa anataka serikali ya Somali kuondoa wanajeshi wake katika eneo la Gedo ili utawala wake uandae uchaguzi. Hatua hiyo inapingwa na serikali kuu.

Kenya na Jubaland zimekanusha madai hayo.

Serikali ya Kenya imeeleza masikitiko kwamba “hatua ya Somalia ilikuwa ya kusikitisha” na kwamba madai hayo “yalikuwa yasiyo na msingi wowote.”

Mgogoro waongezeka zaidi

Mgogoro kati ya Somalia na Kenya umeongezeka zaidi kufuatia ziara ya rais wa Somaliland, ambayo ilijitangazia uhuru kutoka kwa Somalia Muse Bihi Abdi nchini Kenya.

Abdi alikutana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jumatatu.

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba viongozi hao wawili wamezungumzia maswala “ya muhimu yanayohusu nchi hizo mbili.”

Kenya imesema kwamba haina upendeleo wowote wa kidiplomasia nchini Somaliland lakini imetaja Somaliland kuwa mshirika muhimu sana katika pembe ya Afrika katika kupambana na ugaidi hasa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.

Kenya imesema kwamba inazingatia sana namna ya kuimarisha biashara na uekezaji kati yake na Somaliland.

Somaliland alijitangazia kujitawala kutoka kwa Somalia mnamo May 1991 lakini uhuru wake haujatambuliwa kimataifa.

Serikali ya Somalia inasisitiza kwamba Somaliland ni sehemu ya Somalia.

Mnamo July mwaka huu, Somalia ilisitisha uhusiano wake na Guinea, baada ya nchi hiyo ya Afrika magharibi kumkaribisha rais wa Somaliland mjini Conakry.

Licha ya uhusiano wa Kenya na Somalia kuwa mbaya katika siku za hivi karibuni, Kenya ina maelfu ya wanajeshi wake nchini humo, chini ya muungano wa Afrika – AMISOM, wanaopambana na wanamgambo wa Al-shabaab.

Nchi hizo mbili vile vile zina mzozo wa mpaka unaosubiri kutatuliwa na mahakama ya haki ya kimataifa.

Kesi hiyo ya mpaka imepangiwa kusikilizwa mjini Hague, March 2021.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

CHANZO: VOA

Note: Kenya ndio nchi pekee katika ukanda huu yenye kugombana na kukwaruzana na majirani zake wengi kutokana na kukosa busara vichwani mwa viongozi wao.
 
Somalia wameamua kama ni mbaya ni mbaya. Wamecut diplomatic ties with Kenya na kufunga embassy yao hapa Kenya. Hii ni kwa sababu ya Kenya kualika rais wa nchi ya Somaliland. Sasa naomba Kenya irecognise Somaliland as an independent country.

Kwa hivyo Uganda haijawahi kukwaruzana na Rwanda? Kwa hivyo Tanzania haijawahi kukwaruzana na Uganda? Uganda na Rwanda hazijawahi kukwaruzana na DR Congo?

Kenya ndio nchi pekee ukanda huu ambayo haijawahi kupigana vita na serikali ya nchi nyingine.
 
Sasa hapo lile neno la busara kichwani, ndipo linapotumika. Huwezi kutambua na kuikubali kitu inayoonekana haramu kwa mwenzako. Hapo hali, itakuwa mbaya zaidi.
 
Kwa hivyo Uganda haijawahi kukwaruzana na Rwanda? Kwa hivyo Tanzania haijawahi kukwaruzana na Uganda? Uganda na Rwanda hazijawahi kukwaruzana na DR Congo?
Kenya ndio nchi pekee ukanda huu ambayo haijawahi kupigana vita na serikali ya nchi nyingine.
Kama kawaida yako kusoma bila kuelewa, nimesema "yenye kukwaruza na majirani wengi zaidi kuliko nchi yoyote hapa EA"
 
Kama kawaida yako kusoma bila kuelewa, nimesema "yenye kukwaruza na majirani wengi zaidi kuliko nchi yoyote hapa EA"
Naona umekasirika hapo pa kupigana vita, si ni kweli kenya haijawai kupigana na nchi yyte afrika mashariki kiserekali.
 
Kwa hivyo Uganda haijawahi kukwaruzana na Rwanda? Kwa hivyo Tanzania haijawahi kukwaruzana na Uganda? Uganda na Rwanda hazijawahi kukwaruzana na DR Congo?
Kenya ndio nchi pekee ukanda huu ambayo haijawahi kupigana vita na serikali ya nchi nyingine.
Ethiopia na kenya walitwangana
 
Kama kawaida yako kusoma bila kuelewa, nimesema "yenye kukwaruza na majirani wengi zaidi kuliko nchi yoyote hapa EA"
Kukwaruzana gani hii ya maneno tu unaweza kweli kuilinganisha na nyinyi kupigana na kuuana na Uganda?
 
Huelewi dynamics za huu 'mgogoro' kati ya Kenya na Somalia. Rais Farmaajo anatumia hizo mbinu za kiboya kutafuta kura. Baada ya kuona kuna uwezekano mkubwa kwamba atashindwa kwenye uchaguzi wa Feb. 2021. Wasomali wenyewe wanamkemea kwa kukuza vitu ambavyo havipo. Ingekuwa kuna bifu ya kweli wabunge na wagombea urais wa Somalia hawangekuwa wamepiga kambi jijini Nairobi wakifanya kampeni zao. Farmajo’s attack on Kenya a survival tactic
 
Wa kenya muwe makini na hao watu wana weza wakaipindua Kenya.

Lazima kwanza muwaheshimu Somali maana kuna raia wengi wa kisomali ambayo tayar wana uraia wa kenya na baadhi wana hodhi nafasi kubwa za kiuongozi.

What if they act as puppet or spy on somali side, nyie mnao jiita sijui wa kikuyu, wa luo, kamba, and so forth mkae chini na hao watu wata wapindua soon.

Nakumbuka this years kuna wale viongozi wa bungenla kenya wenye asili ya somalia walikwenda somalia sijui kufanya jambo gan walipo rudi mkawapigia kelele sana hadi wengine mkawavua madaraka.
 
Kwa hivyo Uganda haijawahi kukwaruzana na Rwanda? Kwa hivyo Tanzania haijawahi kukwaruzana na Uganda? Uganda na Rwanda hazijawahi kukwaruzana na DR Congo?
Kenya ndio nchi pekee ukanda huu ambayo haijawahi kupigana vita na serikali ya nchi nyingine.
Kenya haijawahi vamiwa ila inatamani ivamie na ina kiherehere juu ya majirani na kujikuta nchi ya kizungu wakati ni nchi yenye watu weusi tii hapa East Africa.
 
Naona umekasirika hapo pa kupigana vita, si ni kweli kenya haijawai kupigana na nchi yyte afrika mashariki kiserekali
Hamna jeshi la kupigana na nchi yoyote hapa Africa Mashariki, Uganda wanawatia vidole huko Migingo lakini mnaogopa kufanya lolote, Alshabaab wanaingia na kutoka wapendavyo na hamuwezi kuwafanya lolote[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wa kenya muwe makini na hao watu wana weza wakaipindua Kenya.

Lazima kwanza muwaheshimu Somali maana kuna raia wengi wa kisomali ambayo tayar wana uraia wa kenya na baadhi wana hodhi nafasi kubwa za kiuongozi.

What if they act as puppet or spy on somali side, nyie mnao jiita sijui wa kikuyu, wa luo, kamba, and so forth mkae chini na hao watu wata wapindua soon.

Nakumbuka this years kuna wale viongozi wa bungenla kenya wenye asili ya somalia walikwenda somalia sijui kufanya jambo gan walipo rudi mkawapigia kelele sana hadi wengine mkawavua madaraka.
Nchi yao tu imewashinda ndio watakuja weza ya wengine, huu ni uandishi wa kinafiki sana.

Kwanza wasomali wanaoishi kenya hata hawatamani kurudi somali zaidi huwaza kwenda mambele, we unaleta ngano zako hapa.

Wasomali wanaoishi kenya unawajulia wapi life style yao zaidi ya kuwajulia tu vijiweni.
 
Kukwaruzana gani hii ya maneno tu unaweza kweli kuilinganisha na nyinyi kupigana na kuuana na Uganda?
Kwahiyo Amin alivyovamia ulitaka tukae kimya?, sisi sio Kenya, jeshi letu linaogopewa Africa nzima, ukitujaribu tunakutoa, uliza Idd Amin, M23 na Magaidi wa Msumbiji.

Sisi tunaishi vizuri na majirani zetu wote, tumepakana na nchi 8 lakini ni Kenya tu ndio hatuelewani nao, ninyi mnagombana na Somalia, Tanzania, Uganda, South Sudan na Ethiopia. Jirekebisheni.
 
Nchi yao tu imewashinda ndio watakuja weza ya wengine, huu ni uandishi wa kinafiki sana..
Kwanza wasomali wanaoishi kenya hata hawatamani kurudi somali zaidi huwaza kwenda mambele, we unaleta ngano zako hapa..

Wasomali wanaoishi kenya unawajulia wapi life style yao zaidi ya kuwajulia tu vijiweni
Jirekebisheni majirani wamewachoka
 
Back
Top Bottom