mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Barabara hii ya Mtwara - Lindi-Dar es Salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange vizuri utunzaji sio mzuri.
Mmeniudhi Wizara ya Ujenzi, sijafurahia. Nimetoka na machungu kwa kumzika Mzee Mkapa, lakini hapa Somanga napo nimepata machungu kwa kukuta barabara hii haijatengenezwa”
Barabara hii ya Mtwara-Lindi-Dar es salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange, utunzaji sio mzuri.Hii barabara imeharibika, huwezi ukaamini kama tuna Waziri wa Ujenzi. Kilometa 90 zote nilikuwa nahesabu zimeharibika - Rais Magufuli
Rais Magufuli ametoa Shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi Somanga baada ya mwanafunzi wa shule hiyo Rehema Mikidadi Ngenje kumwambia Changamoto za Shule hiyo. Pia Rais amemzawadia mwanafunzi huyo Tsh 100,000.
"Nisikilize Mzee wangu, baba yangu ameshatangulia mbele ya haki,umetoa jogoo,siku ukienda chato nitakukabidhi mama yangu na wewe uwe baba,haya kamlete huyo jogoo" - Rais Magufuli