Godfrey- denis
Member
- Aug 26, 2022
- 64
- 124
🔁 Katika somo letu lililopita, tulijifunza kuhusu faida ya gawio — sehemu ya faida ya kampuni inayogawiwa kwa wanahisa.
📍 Leo, tunachambua tarehe muhimu zinazotajwa kampuni inapokuwa imetangaza gawio, ambazo mara nyingi huwachanganya wawekezaji wapya.
1️⃣ Dividend Declaration Date – Tarehe ya Kutangaza Gawio
Hii ni siku ambayo bodi ya wakurugenzi wa kampuni inatangaza rasmi gawio litakalotolewa kwa mwaka husika.
🧾 Mfano: Kwa CRDB, tarehe ya kutangaza gawio ilikuwa 14 Aprili 2025 — na wametangaza kutoa TZS 65 kwa kila hisa.
2️⃣ Cum Dividend Period – Kipindi cha Hisa zenye Gawio:
Ni kipindi ambapo ukinunua hisa, unastahili kupokea gawio la mwaka huo.
🗓️ Kwa CRDB, kipindi hiki ni 14 Aprili hadi 6 Mei 2025.
🗓️ Kwa NMB, mwisho wa kupata gawio kwa ununuzi wa hisa ni 2 Juni 2025.
⚠️ Unaponunua hisa ndani ya kipindi hiki — hisa hizo zitahesabika kwenye gawio!
3️⃣ Ex-Dividend Date – Kipindi cha Hisa zisizostahili kupata Gawio.
Kuanzia tarehe hii, ukinunua hisa hazitahesabika kwenye gawio la mwaka husika.
🧾 Kwa CRDB, Ex-Dividend Date ni 7 Mei 2025
🧾 Kwa NMB, ni kuanzia tarehe 3 Juni 2025
🔔 Ni kosa la kawaida kwa watu kununua hisa baada ya tarehe hii wakidhani bado hisa walizonunua wakati huo zinastahili kuhesabika kwenye gawio.
4️⃣ Closure of Register – Kufunga Kitabu cha Wanahisa
Ni tarehe ya mwisho ambayo kampuni inafunga orodha ya wanahisa waliostahili kulipwa gawio.
🗓️ Kwa CRDB ni 9 Mei 2025
5️⃣ Dividend Payment Date – Tarehe ya Malipo ya Gawio
Ni tarehe rasmi ambayo fedha ya gawio huingizwa kwenye akaunti yako ya benki.
🗓️ Kwa CRDB: kuanzia 2 Juni 2025
🗓️ Kwa NMB: 19 Juni 2025
💡 Kama wewe ni mwekezaji mpya au kuna magawio yako ambayo hujawahi kupokea miaka ya nyuma— hakikisha una-update na kutuma taarifa zako kwenye kampuni husika (Mawasiliano hupatikana kwenye tovuti za kampuni husika kwenye kipengele cha investors relation.
🔄 Kumbuka:
Usinunue hisa kwa msisimko tu wa kuona tangazo la gawio! Elewa vizuri tarehe zinazohusika, ili usije ukajikuta umenunua hisa lakini hisa hizo zisihesabike kwenye gawio la mwaka husika.
🧠 Elimu kama hii ndiyo inakufanya siyo tu mwekezaji — bali mwekezaji mwenye maarifa.
Swali la siku:
Usikose somo lijalo 🫵

Umeshawahi kukosa gawio kwa sababu hukujua tarehe hizi? Je, somo hili limekusaidia kuelewa vizuri zaidi?
Usikose somo lijalo 🫵