Somo la 6: tarehe muhimu unazopaswa kuzielewa wakati wa gawio

Joined
Aug 26, 2022
Posts
64
Reaction score
124
πŸ” Katika somo letu lililopita, tulijifunza kuhusu faida ya gawio β€” sehemu ya faida ya kampuni inayogawiwa kwa wanahisa.

πŸ“ Leo, tunachambua tarehe muhimu zinazotajwa kampuni inapokuwa imetangaza gawio, ambazo mara nyingi huwachanganya wawekezaji wapya.

1️⃣ Dividend Declaration Date – Tarehe ya Kutangaza Gawio
Hii ni siku ambayo bodi ya wakurugenzi wa kampuni inatangaza rasmi gawio litakalotolewa kwa mwaka husika.

🧾 Mfano: Kwa CRDB, tarehe ya kutangaza gawio ilikuwa 14 Aprili 2025 β€” na wametangaza kutoa TZS 65 kwa kila hisa.

2️⃣ Cum Dividend Period – Kipindi cha Hisa zenye Gawio:
Ni kipindi ambapo ukinunua hisa, unastahili kupokea gawio la mwaka huo.

πŸ—“οΈ Kwa CRDB, kipindi hiki ni 14 Aprili hadi 6 Mei 2025.
πŸ—“οΈ Kwa NMB, mwisho wa kupata gawio kwa ununuzi wa hisa ni 2 Juni 2025.

⚠️ Unaponunua hisa ndani ya kipindi hiki β€” hisa hizo zitahesabika kwenye gawio!

3️⃣ Ex-Dividend Date – Kipindi cha Hisa zisizostahili kupata Gawio.
Kuanzia tarehe hii, ukinunua hisa hazitahesabika kwenye gawio la mwaka husika.

🧾 Kwa CRDB, Ex-Dividend Date ni 7 Mei 2025
🧾 Kwa NMB, ni kuanzia tarehe 3 Juni 2025

πŸ”” Ni kosa la kawaida kwa watu kununua hisa baada ya tarehe hii wakidhani bado hisa walizonunua wakati huo zinastahili kuhesabika kwenye gawio.

4️⃣ Closure of Register – Kufunga Kitabu cha Wanahisa
Ni tarehe ya mwisho ambayo kampuni inafunga orodha ya wanahisa waliostahili kulipwa gawio.

πŸ—“οΈ Kwa CRDB ni 9 Mei 2025

5️⃣ Dividend Payment Date – Tarehe ya Malipo ya Gawio
Ni tarehe rasmi ambayo fedha ya gawio huingizwa kwenye akaunti yako ya benki.

πŸ—“οΈ Kwa CRDB: kuanzia 2 Juni 2025
πŸ—“οΈ Kwa NMB: 19 Juni 2025

πŸ’‘ Kama wewe ni mwekezaji mpya au kuna magawio yako ambayo hujawahi kupokea miaka ya nyumaβ€” hakikisha una-update na kutuma taarifa zako kwenye kampuni husika (Mawasiliano hupatikana kwenye tovuti za kampuni husika kwenye kipengele cha investors relation.

πŸ”„ Kumbuka:
Usinunue hisa kwa msisimko tu wa kuona tangazo la gawio! Elewa vizuri tarehe zinazohusika, ili usije ukajikuta umenunua hisa lakini hisa hizo zisihesabike kwenye gawio la mwaka husika.

🧠 Elimu kama hii ndiyo inakufanya siyo tu mwekezaji β€” bali mwekezaji mwenye maarifa.

Swali la siku:
Umeshawahi kukosa gawio kwa sababu hukujua tarehe hizi? Je, somo hili limekusaidia kuelewa vizuri zaidi?

Usikose somo lijalo 🫡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…