Uchaguzi 2020 Somo la bure kwa Vyama vya Upinzani mwaka huu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Vyama vya upinzani vimeegemea kuamini kuwa wananchi wanaichukia sana serikali ya CCM kutokana na mambo mawili: mzunguko wa pesa kupungua mitaani, na serikali ya CCM kuwabana sana watu wafuate sheria na kusimamia sana raslimali za nchi bila kuwasikiliza watu wa nje. Hizo ndizo mada za ATC-Wazalendo, CUF na CHADEMA.

Tatizo ni kwamba Wakati CCM inakutana na wapiga kura kwenye kata 11; CHADEMA imekutana na wakazi kata moja tu, na ACT ilikutana na kata mbili tu.

Katika mazingira hayo inakuwa ni obvious kuwa CCM iko mbele. Inabidi vyama vya upinzani viongeze nguvu ya kukutana na wapiga kura; watu wanaotoa support kubwa sana mtandaoni siyo watakaokwenda kwenye vituo vya uchaguzui kupiga kura.

halafu nimeona mikutano ya Magufuli anatumia karibu nusu ya muda wake kuawanadi pia wagombea wa ubunge na udiwani wa CCM, wakati mikutano ya Lissu anatumia karibu nusu ya muda wake kumsema Magufuli na jinsi yeye alivyopigwa risasi.

 
Hiyo fiesta yenu isiwadanganye.
Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu inabamba sana.
Watu wengi wameshafanya maamuzi wanasubiri tarehe tu.
 
Hahahaha facts nyingine zinachekesha sana, nimezunguka vijiji vingi sana Tanzania, nimekuta watu wako committed na upinzani sijapata kuona hadi unajiuliza, wamelishwa nini hawa?

Mfano, nani anakumbuka wale wana Tukuyu (jina la sehemu limenitoka), ambao baada ya kiongozi wao kufungwa gerezani walijikusanya na kwenda kuandaa shamba lake, wakalima na kumpandia viazi? Na picha zilikuepo. Nimefikia Mambwemkoswe Sumbawanga Vijijini nimekuta Chadema wakiwa strong, nilifika Ludewa, nimefika Makete, Nimefika Runzewe, nimefika Bunda vijijini, nimefika Musoma huko kwenye visiwa vya dagaa, nimeshangaa note huku kukuta upinzani wenye nguvu na imara!!

Anayesema vitu ambavyo viko kwenye maandishi na mwandishi wa hivyo vitu ana vinasaba na CCM then ukamuamini basi tuna tatizo.

Ccm haishindi kwa kura za kwenye sanduku, huu ndio ukweli mchungu! Kuna kitu vingesemwa watu wangeogopa...kuwa kumbe hii ndio CCM! Tunajua, juzi jamaa yangu huko Dar kapeleka Gospel videos zake kwenye moja ya kituo cha Television, akajibiwa kuwa labda kama ingekua ni gospel yenye kusifia MTU wangeweza kupokea! Ushihidi upo!

Yupo mwingine ambaye ndio mmiliki wa kituo cha redio maarufu tu huko Dar, kawaambia kabisa hakuna kuongea mambo ya upinzani labda kama yanazungumzwa negatively.

Hapa JF yupo jamaa yule (nimesahau ID yake ila ya muda mrefu na twitter anatumia ID hio hio) aliwahi kueleza jinsi walivyokuwa wanafanya huko Bukoba I think kuhujumu vyama vingine. Ndugu zangu kuna mengi tusiyoyafahamu wengine. Tupendane tu maana kuna maisha baada ya siasa

All these nonsense then utegemee kitu gani?
 
Usitusemeeee.

Mimi nipo mahali ambapo Tundu Lisu hajawahi wala hajawaza kufika , lakini raia zinasema Magufuli wameshamchoka. Miaka mitano inatosha.

hata mimi kwenye kijiji cha asili yetu inawezekana hakuna hata mgombea atafika; ila sasa ukiangalia infrastructure ya CCM ni kubwa mara tatu ya vyama vyote vya upizani. Yaani iwapo mwenyekiti wa kijiji akihudhuria mkutano wa magufuli, atafikisha ujumbe ule kwa wakazi wa eneo lake lote, wakati Chadema haina infrastructure hiyo.Usinishambulie kama ilivyozoeleka hapa bali tuambizane ukweli tu; hayo ni maoni yangu.
 
Hiyo fiesta yenu isiwadanganye.
Uhuru , Haki na Maendeleo ya watu inabamba sana.
Watu wengi wameshafanya maamuzi wanasubiri tarehe tu.
Huo uhuru na haki mnavitaka nyie hapo ufipa tena kwa viongozi wenu tu!

Lakini watanzania hayo walishayapata toka miaka 60 iliyopita
Kwa hiyo wanawashangaa mnapozinduka leo na kuja na slogani ya miaka 60 iliyopita.

Jibu mtalipata oktoba
 
Siasa ya Tanzania imebadilika sana, kuna tofauti kubwa sana kimtazamo ndani ya miaka3 iliyopita.

Vimefanyika vingi wananchi wengi wa vijijini walivyotaka, sera za vyama ziko kwenye makaratasi wananchi hawahitaji kusomewa peke yake wanachotaka ni kuona mambo yao muhimu yanaenda kama elimu, maji, nishati, barabara, hospitali, wananchi wengi wamefikiwa na wachache wanafanyiwa kazi.

Nguvu ya wajumbe iliyoonekana mwaka huu ni kubwa mnooo kwenye mashina waliko wapiga kura.

CCM inashinda kwa kura
Jumla ya wapiga kura 29M
Wanachama CCM 15M
Wanachama chadema 2M
Na wajumbe walihakikisha kila mwanachama wao amejiandikisha kupiga kura pale anapoishi

October sio mbali tutajua mbivu na mbichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…