ROJA MIRO
Member
- Jul 19, 2021
- 52
- 56
Kwa mujibu wa muhtasari wa somo la stadi za kazi kwa wanafunzi ambao umeadaliwa kutokana na mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la 3 hadi la 6 wa mwaka 2016 muhtasari ambao kwa sasa umefutwa,kupitia muhtasari huu mwanafunzi aligemewa kujenga stadi za usafi,mapishi tofauti,ujasiriamali,na kusanifu kazi za Sanaa na stadi hizi zitajengwa kwa kutenda shughuli anuwai.
Lengo la somo hili ni kumuwezesha mwanafunzi kujenga mwelekeo chanya kuhusu kazi zitakazomuwezesha kumudu mazingira ya kila siku,na somo linakusudia kubaini vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza, pamoja na kujenga misingi ya kujitegemea.
Kwa mfano tu wa kitabu cha somo la stadi za kazi kwa mwanafunzi wa darasa la saba cha mwandishi,J .S. Magogo ambacho kiliidhinishwa na EMAC tarehe 21 January mwaka 2011 kwa ajili ya darasa la saba kwa shule za Msingi nchini Tanzania,mada mbalimbali zimefafanuliwa kwa ajili ya mwanafunzi ili kumjengea misingi yake ya kujitegemea hapo baadae,mfano:-
Kwenye mada ya Kilimo kama ilivyochanganuliwa kupitia ukurasa wake wa 46 wa kitabu hicho mwanafunzi anatarajiwa kujifunza ustawishaji wa mazao bora ya biashara,namna ustawishaji wa mazao hayo na mengine yaliyoanishwa katika njia bora za ustawishaji wa mazao ya biashara.
Katika ukurasa wa 75 wa kitabu hicho pia kumejadiliwa mada ya uvuvi ambapo mwanafunzi atajifunza maana ua ufugaji bora,faida za uvfugaji bora,ufugaji bora wa nyuki,kuandaa mizinga ya nyuki pamoja na mengine yanayohusu ufugaji na uvuvi.
Nimalizie na ukurasa wa 115 hapa kumejadiliwa mada ya Biashara ndogondogo,hapa mwanafunzi atajifunza misingi ya biashara ndogondogo,Bashara ndogondogo za kufanya.
Hayo kwa uchache wa yale ambayo ambayo mwanafunzi anaweza kujifunza ila changamoto nitakazozianicha hapa chini zimekuwa zikitajwa kukwamisha ufundishaji wa usahihi kwa somo hili.
Makala hii ilifanya utafiti katika baadhi ya shule za Msingi nchini na katika mazungumzo ambayo nilifanya na baadhi ya wanafunzi pamoja na walimu waliibua changamoto zifuatazo:-
Kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia somo hilo kwa vitendo,mfano kama unataka kuwafundisha wanafunzi namna ya kudarizi kwa kutumia cherehani,kwanza lazima uwe na cherehani,uzi pamoja na vitambaa jambo ambalo linapelekea wanafunzi wajifunze kwa nadharia hivyo kupelekea kukosa ujuzi.
Hoja yangu inabebwa na kile kinachotokea pale baadhi ya wazazi, watoto wao wanaposhindwa kuendelea na masomo ya sekondari huwapeleka kwa mafundi mbalimbali wa kushona ili kujifunza,ushahidi ambao unaonesha tosha kwamba wanafunzi hawa kuna kitu wamekikosa tangu wakiwa shuleni,hivyo pesa ambayo mzazi angeitumia kumlipa fundi kama ada ya kumfundisha mwanae angeitumia kumnunulia cherehani na akaanza kushona kwa sababu atakuwa ameshajifunza shuleni.
Changamoto nyingine ambayo nimeiona na namna ambavyo wanafunzi wamejengwa kwamba cheti ndio elimu,sasa kwa sababu somo la stadi za kazi halijumuishwi kwenye mitihani ambayo mwanafunzi anafanya anapohitimu hupelekea kulisoma kama bahati mbaya,na wakati mwengine pia mwalimu anakazania masomo ambayo yanampa mwanafunzi alama za ufaulu ili matokeo ya mwisho yaje mazuri.
Hebu tuangalie baadhi ya watu ambao walipokuwa wanasoma walikuwa na vipaji vingine ila vyote vilikwenda kwa pamoja pengine si kwa sababu shule walizosoma zilikuwa na mifumo ya elimu za kujitegemea bali jitihada zao binafsi sasa tujilize je ingekuwa tuna miundo mbinu na mikakati ya masomo ya stadi za kazi tungekuwa wapi? Na hapa nitatolea mfano wachezaji wa soka wa ndani mmoja na baadhi kutoka nje ya nchi.
Mfano kwa Tanzania mchezaji wa Coastal Union Ayoub Semtawa akiwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) alipokuwa anachukua shahada ya utabibu, tayari alikuwa ni mchezaji wa klabu ya Ligi Kuu ya Bara.Kabla ya kuhamia klabu ya Coastal Union ya Tanga mwaka 2016 alisajiliwa na klabu ya Mbeya City.
Kuna namna mataifa mengine wenzetu wanavyojumuisha vipaji na elimu tuangalie mfano wa wachezaji wa nje waliosoma fani nyingine na ucheza mpira ina maana kimoja kingekosekana angepata ajira yake kupitia kingine yupo,Simon Mignolet,huyu ni mlinda lango wa Liverpool.
Mignolet ana Shahada ya masuala ya Sheria na Sayansi ya Kisiasa aliyoipata kwenye Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Leuven (Catholic University of Leuven) kilichopo Ubelgiji. Anaweza kuzungumza lugha nne kwa ufasaha: Kiingereza, Kifaransa, Kiholanzi na Kijerumani.
Edwin van der Sar,Golikipa huyu wa zamani wa Manchester United alikuwa na mafanikio makubwa akiwa Old Trafford ambapo aliweza kushinda mataji mengi kukiwemo Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu ya England. Hivi karibuni alikamilisha Shahada yake ya Uzamili ya kimataifa katika Uongozi wa Michezo. Sasa anatumika kama Mkurugenzi wa Masoko katika klabu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi,hiyo ni mifano micheche tu tena na nimetolea kwa upande wa wanasoka sijazungumzia vipaji vingine.
Nchini Tanzania kundi kubwa la wahitimu wakiwemo vijana wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu na hii ni kutokana na kukosa kitu mbadala wanachoondoka nacho zaidi ya kile ambacho wamesoma,mfano kwa mujibu wa ripoti ya karibuni ya Shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA inaonesha kwamba Kiasi cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 – 24 ni asilimia 13.4%. Ukosefu wa ajira upo juu kwa wanawake vijana vile vile ni 14.3%) kuliko kwa vijana wanaume wenye umri huo huo, ambao ni 12.3%.
Nini kifanyike?
Ni vyema serikali ikaongeza masomo yanayomjenga mwanafunzi katika misingi ya kujitegemea ili mwanafunzi kama atashindwa kuendelea na masomo ya juu zaidi au kama atafeli basi awe na misingi mizuri ya kujiajiri mwenyewe kuliko kutegemea ajira kwa kutegemea vyeti na kurudisha mfumo wa masomo ya zamani kama vile Sayansi Kimu ambayo yaliwasaidia wanafunzi wa wakati huo.
Hitimisho.
Naipongeza serikali katika mpango wake wa masomo ya ufundi kwa vijana mbalimbali nchini kupitia mpango uliofadhiliwa na ofisi ya waziri mkuu ambapo jumla ya vijana 12625 walichaguliwa,hii ni hatua kubwa sana na itafanya vijana kuona umuhimu wa ujuzi kuliko tu vyeti na hivyo kupunguza malalamiko ya vijana kukosa ajira baada ya kuhitimu.

Upvote
4