Somo: Serikali hii inajihujumu yenyewe na kujitangaza vibaya.

Somo: Serikali hii inajihujumu yenyewe na kujitangaza vibaya.

CWR2016

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
2,773
Reaction score
6,349
Heshima kwenu wakuu.

Nimempigia simu jana Mzee mmoja huko kijijini.
Ni muda tulikuwa hatujawasiliana tangu January yani pale mwaka mpya.

Mimi: Mzee shikamoo
Mzee: Marahaba, hujambo mwanangu..
Mimi: Sijambo, sijui nyinyi hapo kijijini?
Mzee: Kiafya tu wazima, homa za hapa na pale mwanangu.
Mimi: Sawa Mzee nashukuru, nimekujulia hali tu.
Mzee: Mwanangu kuna jambo nikuulize nyie ndio mjini huko mnasoma mengi..
Mimi: Jambo gani Mzee wangu, niulize..
Mzee: Kuna mwanangu kaja hapa juzi anadai katolewa kufundisha shule za sekendari na amepelekwa shule za primary.
Mimi: Alikuwa mwalimu wapi hapo hapo wilayani au..
Mzee: Ndio mwanangu.. Shida ni nini hadi wamfanyie hivi binti yangu .. Amesoma degree amemaliza vizuri sasa leo wanampeleka shule ya msingi. Amefanya kosa gani?
Mimi: Hapana mzee wangu usimhukumu binti yako.
Mimi nilisikia ni utaratibu tu wa serikali. Na zipo wilaya ambazo walishahamishwa tangu February. Serikali inasema walimu wa sanaa kwa sekondari ni wengi na shule za msingi zina upungufu. Hivyo ni serikali chini ya wizara ya elimu na tamisemi waliandaa mpango huo. Lakini mshahara wao hautapungua mzee..

Mzee: Sawa, sasa mbona..
Mimi: Nakusikiliza mzee wangu.
Mzee: Mbona kuna mwanangu huyu wa mwisho kamaliza mwaka Jana chuo cha ualimu yupo tu hapa, hata simuelewi.
Mimi: kwa nini humuelewi mzee..
Mzee: Sasa kama kuna upungufu ..si huyu Magufuli angemuajiri huyu aliyemaliza chuo cha ualimu ambaye karibu anamaliza mwaka yupo tu hapa..
Kwa nini hawamuajiri huyu amemaliza?... (Mzee akauliza kwa msisitizo)

Mimi: Nawaza haraka haraka ntamjibuje Mzee....
Nachakata ubongo haraka haraka nimpe jibu....

Nikaishia kumwambia Mzee asubiri na yeye ataajiriwa tu...

Mzee: Lini wkt nafasi ya upungufu ndio hiyo wamemshusha hapo dada yake?!..

Mimi: Mzee basi wasalimie ntakupigia jumapili jioni..

Nawasilisha...
Mods tafadhali msiunge thread hii. Ni kisa halisi cha kutufunza.
 
Wakuu Salary Slip, Return of the undertaker, tindo, Chakaza, idawa, Saint Ivuga, Sky Eclat n.k. hii ni habari ya kuhamishiwa JF chit-chat.

Moderator, Paw, Invisible, Maxence Melo tafadhali basi tendeni haki ktk nyakati hizi ngumu ambazo ukweli unaminywa kila pahala.
Habari hii niliiweka jukwaa la siasa. Kwanza mkaiondoa na kuipoteza kabisa halafu badae naona mmeileta JF Chit-Chat...
Aisee mko serious kweli?!. Si bora mngeipeleka hata "hoja na habari mchanganyiko".
Mmenidharau sana na kuihukumu akili yangu kwamba nimeleta utani wkt kisa cha kweli.
Mungu atawalipia.
Uhuru tunaoupigania ndio huo huo usalama wa JF yenyewe. Kesho mtaelewa. Leo mnanifungia mlango ambao kesho na nyie mtaomba ufunguliwe.
 
Pole sana, hayo mambo sasa hivi ndiyo yana kera sana hapa JF. Mods wamekuwa wanafanya mambo mengine hadi yanashangaza.
Unaweza kuanzisha Uzi wakaamua kuunga na mwingine lakini wenye maudhui tofauti kisa tuu mnataja kitu kimoja na kuharibu kabisa maana halisi ya mjadala huo. Na kuna watu hawayaki watajwe kabisa hivyo wanaweza kuuchomoa Uzi kiaina.
Waweza kudhani kuwa wapo mods ambao wapo kwenye payroll ya hao jamaa kuwalinda.
Naweza nami nikashushiwa rungu kama lile LA Ndugai hivyo ngoja ninyamaze kwanza
 
Aisee hii mbaya sana. Na vitufe vya ban havipo mbali saivi
 
Hii amisha ya walimu inawacost sana wale wasio penda kujipendekeza kwa wakuu wa shule poleni walimu
 
Hii amisha ya walimu inawacost sana wale wasio penda kujipendekeza kwa wakuu wa shule poleni walimu
Aisee acha tu.. Kwani walimu wakuu ndio wanaopendekeza eeh
 
Hii amisha ya walimu inawacost sana wale wasio penda kujipendekeza kwa wakuu wa shule poleni walimu
Hii ya kujipendekeza imewa cost baadhi ya watu na zoezi likarudiwa ktk wilaya moja.
 
Back
Top Bottom