Heshima kwenu wakuu.
Nimempigia simu jana Mzee mmoja huko kijijini.
Ni muda tulikuwa hatujawasiliana tangu January yani pale mwaka mpya.
Mimi: Mzee shikamoo
Mzee: Marahaba, hujambo mwanangu..
Mimi: Sijambo, sijui nyinyi hapo kijijini?
Mzee: Kiafya tu wazima, homa za hapa na pale mwanangu.
Mimi: Sawa Mzee nashukuru, nimekujulia hali tu.
Mzee: Mwanangu kuna jambo nikuulize nyie ndio mjini huko mnasoma mengi..
Mimi: Jambo gani Mzee wangu, niulize..
Mzee: Kuna mwanangu kaja hapa juzi anadai katolewa kufundisha shule za sekendari na amepelekwa shule za primary.
Mimi: Alikuwa mwalimu wapi hapo hapo wilayani au..
Mzee: Ndio mwanangu.. Shida ni nini hadi wamfanyie hivi binti yangu .. Amesoma degree amemaliza vizuri sasa leo wanampeleka shule ya msingi. Amefanya kosa gani?
Mimi: Hapana mzee wangu usimhukumu binti yako.
Mimi nilisikia ni utaratibu tu wa serikali. Na zipo wilaya ambazo walishahamishwa tangu February. Serikali inasema walimu wa sanaa kwa sekondari ni wengi na shule za msingi zina upungufu. Hivyo ni serikali chini ya wizara ya elimu na tamisemi waliandaa mpango huo. Lakini mshahara wao hautapungua mzee..
Mzee: Sawa, sasa mbona..
Mimi: Nakusikiliza mzee wangu.
Mzee: Mbona kuna mwanangu huyu wa mwisho kamaliza mwaka Jana chuo cha ualimu yupo tu hapa, hata simuelewi.
Mimi: kwa nini humuelewi mzee..
Mzee: Sasa kama kuna upungufu ..si huyu Magufuli angemuajiri huyu aliyemaliza chuo cha ualimu ambaye karibu anamaliza mwaka yupo tu hapa..
Kwa nini hawamuajiri huyu amemaliza?... (Mzee akauliza kwa msisitizo)
Mimi: Nawaza haraka haraka ntamjibuje Mzee....
Nachakata ubongo haraka haraka nimpe jibu....
Nikaishia kumwambia Mzee asubiri na yeye ataajiriwa tu...
Mzee: Lini wkt nafasi ya upungufu ndio hiyo wamemshusha hapo dada yake?!..
Mimi: Mzee basi wasalimie ntakupigia jumapili jioni..
Nawasilisha...
Mods tafadhali msiunge thread hii. Ni kisa halisi cha kutufunza.