Somo zuri kwa wamiliki wa AC pamoja na majokofu

buzitata

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2017
Posts
2,370
Reaction score
7,900
Leo nimeona nitoe somo dogo kuhusu mifumo ya upoozaji, hapa nitachanya vyote kwa lugha nyepesi ambayo haipo deep sana ili lengo litimie ila kwenye comment ntakuwa naenda deep zaidi kwa yule mwenye uelewa zaidi juu ya mifumo hii ya upoozaji

WAtu wengi wanamiliki majokofu na AC ila hawajui vinafanyaje kazi

Mfumo unafanyaje kazi, kazi ya AC ama jokofu ni kuondoa joto hali ambayo baadae inaleta ubaridi kwenye mfumo kupitia evaporator

Mfumo umeundwa na vitu vikuu ambavyo vinasaidiana ili kuweza kufikia lengo, vitu hivyo ni kama,

. compressor(kwaajili ya kukandamiza freon au gesi)

. Condensor(kwaajili ya kuondoa joto ambalo limebegwa na gesi aina ya freon)

. Expansion valve(kwaajili ya kupunguza pressure ya gesi ambayo ni freon ili iweze kuleta ubaridi

. Evaporator(hii ndio sehemu ambayo inapooza hewa ambayo unaivuta ili iweze kuwa ya baridi)

Vitu hivyo hapo juu ndio moyo wa kifaa chako endapo kimoja hakifanyi kazi sawa sawa basi mfumo mzima utaonekana una dosari ama ubaridi usipatikane kama ilivyotarajiwa

Nini kinafanyika?

Kuna aina maalumu ya gesi ambayo ni freon(zipo aina nyingi na hazichanganywi kila mfumo unahitaji freon yake ili iwe na ufanisi)

Freon inaingia kwanza kwenye compresor ili kukandamizwa, kikawaida joto litapanda ukijumlisha na lile joto ambalo la hewa unayoivuta hapo freon itakuwa na joto la juu kiasi, hilo joto lazima lipunguzwe na linapunguzwa baada ya kuingia kwenye condensor, hapa joto litapunguzwa japo haitakiwi lipungue lote kwasababu italeta shida kwenye ufanisi(subcooling).

Baada ya gesi kupunguzwa joto kwenye condensor itapita kwenye expansion valve ili iweze kupunguzwa pressure na kama tunavyojua ukipunguza pressure ya gesi kwa uharaka huwa joto nalo linapungua hii inapatikana zaidi ukisoma kidogo kwenye gas law pv=nrT(sio muhimu kuisoma ila kuelewa ni muhimu zaidi) unaweza upata picha

hyo gesi iliyotoka kwenye condensor haiwi gesi pure bali inakuwa katika hali ya unyevuunyevu ama tuite kimiminika japo ni gesi

KWaiyo kilichoingia kwenye exapansion valve ni kimiminika na baada ya kutoka kwenye expansion valve kinakua na hali ya ubaridi sana na sisi huo ubaridi ndio lengo letu kuu kwaiyo tunaweka kifaa kingine ili tuweza kuuvuna huo ubaridi

Hapa ndipo evaporator inapotumika yaani hewa ya nje ikiwa na joto inapitishwa kwenye coil za evaporator na kupelekea hewa hiyo kupungua joto lake kama tunavyojua joto lina tabia ya kutembea kutoka sehemu yenye joto kubwa kuelekea sehem yenye joto dogo(linaenda kunyonywa), wakati hayo yanaendelea ile hewa ya joto itapoteza joto lake na kuwa ya baridi(hiyo ndiyo hewa tunayoivuta kutoka kwenye AC.
(hayo yanafanyika kwenye mifumo yote ya AC)

kama ilivyo kwa vitu vyovyote vifanyavyokazi huwa havikosi changamoto

Ukiona AC yako haina ubaridi ujue moja kati ya hivyo vitu havifanyi kazi vizuri hivyo vinahitaji kurekebishwa ili kurudi kwenye ubora wake

Matatizo ya kawaida, mengi huwa yanasababishwa na upungufu wa freon Ama compressor kutofanya kazi vizuri au kuungua,

Friji lako halileti ubaridi basi jua tu ni freon chache ama imezidishwa, compressor mbovu, hufungi vizuri mlango wa friji lako na utajua kwa kuona friji lina barafu nyingi.

Kuna baadhi ya vitu nimeviruka sio kwamba havina umuhimu ila havina faida kwa mtumiaji labda kwa mafundi tu.

Kama unatatizo lolote juu ya hiyo mifumo unaweza kushare hapa ili tuweze kisaidiana.

Shukrani!
 
Je una namna ya kuongeza zaidi ubaridi? Mfano gari lina ubaridi wake wa kawaida unaweza ongeza zaidi?
 
Kwann wasema friji hutakiwi kulizima
 
Kwann wasema friji hutakiwi kulizima
Wanaosema hivyo wanalenga hoja ya kuokoa matumizi ya umeme kwasababu friji linalozimwa mara kwa mara linatumia nguvu nyingi kutengeneza ubaridi na kama unavyojua mara nyingi umeme unatumika zaidi kwenye kuanzisha mwendo, hivyo kwa kuzimama mara kwa mara utatumia umeme mwingi kama friji unataka vitu vyako viwe na baridi muda wote.

Friji limewekewa kifaa maalumu ambacho kikigindua ubaridi upo wa kutosha linajizima lenyewe na kujiwasha pale ubarid unapopungua
 
Je una namna ya kuongeza zaidi ubaridi? Mfano gari lina ubaridi wake wa kawaida unaweza ongeza zaidi?
Kila mfumo una limiti yake ya ufanyaji kazi na kila kifaa kimewekwa kwa hesabu maalumu i meen hawajakurupuka tu kuweka vitu bali vimepigiwa hesabu sahihi kwa uzalishaji wa ubaridi fulani ikiwa kama unataka kuongeza ubaridi basi itakubidi upige hesabu upya na kubadilisha baadhi ya vitu kwenye mfumo wako

I hope ukipigiwa gharama zake hutoweza kubadilisha.
Usisikilize sana mafundi wa mitaani wengi wao wana experience tu na wengi hawataki qualification kwenye kazi zao
 
Friji lako halileti ubaridi basi jua tu ni freon chache ama imezidishwa, compressor mbovu, hufungi vizuri mlango wa friji lako na utajua kwa kuona friji lina barafu nyingi.
Mkuu elezea kidogo hapa tafadhali.

"Friji halileti Ubaridi, na ili nijue halileti ubaridi nitaona Barafu nyingi." How?

Asante.
 
Kuna mambo mawili nimeyaweka pamoja

Friji kutoleta ubaridi unaoutaka wewe ijapokuwa linawaka vizuri na kila kitu kipo sawa sawa basi mara nyingi tatizo linakuwa kwenye mlango. Friji kwa kawaida halitakiwi kuwa na mgando wa barafu. Je ile barafu inatokea wapi? Ikiwa kuna upenyo mdogo wa hewa kuingia kwenye fridi lako basi ile hewa inayopenya huwa na unyevu unyevu, chukulia ule unyevuunyevu umekuwa wa muda mrefu hapo lazima utatengeneza matone ya maji kupitia hali ambayo inaitwa condensation, kwakuwa friji lako linafanya kazi vizuri yale matone yataganda na kuanza kuleta barafu.

Barafu sio nzuri ufanisi wa friji
 
Mkuu elezea kidogo hapa tafadhali.

"Friji halileti Ubaridi, na ili nijue halileti ubaridi nitaona Barafu nyingi." How?

Asante.
Cha kuongezwa pia, hata thermostat pia ikiwa mbovu kwenye friji inaweza kupelekea Hilo barafu kuwa nyingi na haitakiwi...Kama alivyosema mkuu hapo juu gesi ikiwa chache baridi haiwezi kuwa standard, hii inaweza kuwa kwasababu ya leakage kwenye pipes au gesi iliongezwa kidogo, kesi ya gesi kupungua yenyewe ni rare Sana, mostly iko sababu.
 
Back
Top Bottom