Son of Ex-Minister Malima in historic medical discovery

mkuu pasco saidia watubac
Mkuu Dada Safre, kwanza asante kunishauri nisaidie watu, ila dada, nisaidie watu kwenye nini?!.

NB, nimekuita dada moja kwa moja kutokana na graphology ya neno "bac" ulilotumia!, kama sio dada sorry in advance!.

Thanks.
Pasco
 
Mkuu Ali, asante. Yes, ila sio wa 90's ni wa late 80's enzi za Walume Ndago, 1990 ndio walianza kuingia wale watoto mayai!.
Thanks.
Pasco
Ile mi ni shule ya family ,baba mdogo kasoma pale(R.I.P) ,brother pale ,mimi pale ,mtoto wa brother yuko pale in short kila generation yetu imegusa pale from 70s i guess till now!
 
Umepata kusikia jina la Dk. Asanterabi Malima?

Jambo moja ambalo wanafunzi waliosoma naye nchini Tanzania hawabishani kuhusu Malima ni ukweli kwamba alikuwa ni mwanafunzi mwenye akili nyingi darasani.

Shafii Dauda ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam, anamkumbuka Asanterabi kama mwanafunzi mwenye akili aliyefanya vizuri sana katika masomo yake ya kumaliza kidato cha nne.

Shafii, ambaye sasa ni miongoni mwa watangazaji na wachambuzi maarufu wa mchezo wa soka hapa nchini alikuwa kidato cha kwanza wakati Malima alikuwa kidato cha nne.

Akili ile ya Malima imemfikisha nchini Marekani ambako sasa amefanya ugunduzi wa kidude chenye saizi ya pini ndogo (milimita 0.250) kinachoweza kubaini magonjwa ya kuambukiza, kansa na moyo katika hatua ya awali kabisa.

Ugunduzi huu, utakapofika mwisho wake, unaweza kuokoa maisha ya watu wengi duniani. Fikiria tu kwamba unakuwa na kifaa ambacho mojawapo ya magonjwa hayo yakikuanza unaubaini mapema na kwenda kutibiwa.

Mamilioni ya watu wataokolewa maisha yao na kijana huyu wa Kitanzania.

Pamoja na mambo mengine, kifaa hicho kitaweza kusababisha wataalamu kubaini endapo mtu yupo kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa ya kuambukizwa, kansa pamoja na yale ya moyo.

Huu ni ugunduzi ambao umeisisimua Marekani na unataraji kuisisimua dunia. Jambo zuri ni kwamba tayari wenzetu wameliona hilo na tayari wameanza kumtuza kijana huyo wa Kitanzania.

Ni ajabu kwamba serikali yake imekuwa kimya hadi leo kumtuza. Ukiondoa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambayo hata robo ya Watanzania hawaifahamu, serikali imekuwa kimya sana kwenye suala hili.

Kama Asanterabi angekuwa msanii, mwanamichezo au mwanasiasa, leo hii tungesikia maandamano makubwa yameandaliwa kwa ajili ya kumpongeza. Lakini kwa sababu ambazo haziko wazi, kuna ukimya umetanda kwa mgunduzi huyu.

Tumeshindwa kuona hata akialikwa Ikulu au kupongezwa tu na taasisi hiyo kubwa wakati tumeona watu waliofanya mambo ya kawaida kabisa wakipewa fursa hiyo. Tunaona kwamba hili ni tatizo kwa Taifa letu.

Namna pekee ambayo Taifa letu linaweza kuchochea vijana kupenda kusoma na kuamini kwamba mtu anaweza kuheshimika na kufanikiwa kimaisha endapo tu atasoma na kufanya kazi kwa bidii, ni kuwapa heshima watu kama Asanterabi.

Itasikitisha sana endapo serikali yetu itakaa kimya na kuacha suala hili liende hivihivi tu wakati tayari serikali ya Marekani imeona kijana huyu amefanya nini. Kama ugunduzi wake huu utapita, kuna kila dalili kwamba kijana huyu atakuja kuwa tajiri mkubwa.

Je, atawekeza katika nchi ambayo imempa ushirikiano na kuna uhakika wa kufanya biashara kuliko kwenye nchi nyingine ambayo uhusiano pekee alionao ni kwamba alizaliwa na kukulia huku?

UMEPATA kusikia jina la Dk. Asanterabi Malima?

Katika mahojiano yake na gazeti hili, aliweka wazi kwamba anaumizwa na hali ya elimu hapa nchini na atakutana na wenzake walio Marekani kuangalia ni kwa namna wanaweza kusaidia.

Sasa mtu kama huyu Taifa linawezaje tu kumwamgalia na kumuona kama mtu wa kawaida na asiyefaa kutuzwa japo kwa maneno tu?

Wakati Rais Jakaya Kikwete atakapokuwa akiwapa tuzo Watanzania mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9 mwaka huu, tutashangaa kama jina la Dk. Asanterabi Kighoma Malima halitakuwapo miongoni mwa watuzwaji.

bofya hapa kusoma zaidi: THE INNOVATION HOUSE : MTANZANIA ATAKAE OKOA ULIMWENGU
 
Watanzania wamejaliwa akili nyingi,lakini huonekana zaidi wakiwa nje ya nchi,hii niliisikia kwenye discussion moja live citizen tv
 
Hiyo habari imo humu kitambo sana.
 
imenisisimua sana, wa tz 2naweza sema akili zetu zote 2meziamishia kwenye siasa.
 
Kaka yake na huyu kijana ni yule waziri mdoogo aliyewahi kuibiwa nguo na pesa gesti Morogoro mjini
 
Kaka yake na huyu kijana ni yule waziri mdoogo aliyewahi kuibiwa nguo na pesa gesti Morogoro mjini

Jamaa bishoo kweli kweli lile, umewahi kumuona akiwa bungeni? Anatembea na cm zisizopungua5 na tablet2, kipindi kile aliibiwa laptop4 na misimu kibao. Bora mdogo wake ana-make changes huko Paradise ya ulimwengu
 
aisee huyu pasco ni muongo sana anadai amesoma drs moja na mtoto wa nyerere bila kumtaja drs moja na mtoto wa mkapa bila kumtaja na Hata mwinyi na jk ambae kwa madai ya hao watu anaodai amesoma ma nao kama watoto wa nyerere basi umri wa pasco ungewiana na jk leo anatuambia amesoma na mtoto wa jk au mzee jomo kenyata labda kina uhuru jamaa punguza uongo haf uongo wako hautegemei idadi ya wake au watoto au unaishi wapi mm sio mwandishi ni drs la saba tena la uswazi kiukweli tofauti kabisa na kiingereza ulichoandika na sijasoma hata na mtoto wa mjumbe wa nyumba kumi
 
Chonde chonde ndugu zangu wa TZ. Niko chini ya miguu yenu. Naomba tuache malumbano ya udini. Kwa kweli mataifa mengine yataanza kutushangaa kwamba kumbe na sisi tuko ovyo. Naomba kila mmoja wetu afikiri zaidi kabla ya kuandika humu. Sisi bado ni wa TZ na inatakiwa tupendane. Hilo ni la msingi na bila hilo hatuwezi kujenga taifa lenye nguvu na linalojiamini kushindana ma mengine. Katika hayo, udini hauna nafasi.

Naomba niweke quotation hii:
 
amani ndio Akili?? Nazungumzia Enzi za Sir K kule kwa "Walume Ndago"
 
Mkuu Kalyovatipi, sikutaja majina kwa kuheshimu kitu kinaitwa "right to privacy!"
Kwa wale wanaoijua shule ya "walume ndago" wanaelewa, na wanamuelewa mtoto wa Nyerere aliyesoma shule hiyo!. Mkapa yeye ana watoto wawili tuu, wote ni vidume, ila aliyesoma shule ya "walume ndago", anafahamika!. Mwinyi nae ana watoto wengi ila aliyesoma shule ya "Walume Ndago" ni mmoja tuu na anafahamika!, hapo ujue sijakutajia watoto wa Malecela ambao mmoja nilisoma nae primary, nilipojoin shule ya sekondari ya "Walume Ndago", nikiwa form I, mtoto mkubwa wa Malecela alikuwa A-Level na akatoka na DIV 1 ya point 3 (za summit) na kujoin UD!, tukiwa form III, binti wa Malecela akajoin shule hiyo ya "Walume Ndago". JK pia ana watoto wengi, ila aliyesoma UD ni mmoja, nikiwa UD tulikuwa nae faculty moja!.

NB. Naomba tofautisha kati ya
  1. Kusoma na mtu shule moja!
  2. Kusoma na mtu darasa moja!,
  3. Kusoma na mtu kozi moja
  4. Kusoma na mtu chuo kimoja
  5. Kusoma na mtu kozi moja!.
Thanks.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…