Songas to buy Dowans generators?

Songas to buy Dowans generators?

Iko mbaya gani. Shareholders watatu in red hapo juu ni private investors. Kwa hiyo Songas inaendesha shughuli zake kwa misingi ya kibiashara siyo kama mashirika yetu ya umma yanavyoendeshwa kwa misingi ya kisiasa.

Kufuatana na hali ya umeme nchini, this is a good business opportunity for anyone with brains kununua hiyo mitambo maana itahitajika tu hata Tanesco wanunue mitambo hiyo mipya.

Hapo Tanesco itapoanza kuwalipa capacity charges na Songas kuongeza faida yao, ndio wale wanaopinga ununuzi wa mitambo ya Dowans watapoona makosa waliyoyafanya. Na Bunge litaangalia hivi hivi bila kuwa na lolote la kufanya kwani halima mandate ya kuingilai utendaji wa Songas.

Msijidanganye TDFL ni mali ya Serikali! Hata kama leo tutadanganywa kuwa Commonwealth Development Corporation wana stake kubwa, lakini bado TDFL ni kampuni ya Serikali.

Miaka ya Nyerere ma GM wa TDFL, anza na Madete hata George Mbowe walikuwa ni uteuzi wa Nyerere!

so we are still being duped by our leaders!
 
Mkuu Semilong,

Unarahisisha mambo utafikiri hiyo kampuni ya kuuza nyanya?

Hayo makampuni mengine yana shareholders wengine wengi tu, wanafuata corporate governance na accounting principles. Unachokisema kinawezekana tu kwenye mashirika yetu ya umma yanayoendeshwa kisiasa.

Kama Songas watanunua huo mtambo ni kwasababu wameona opportunity ambayo sisi hatukuiona na wameamua kuitumia. Its the economy, stupid!

hivi wewe mtanzania
accounting principles - mwadui haijapataa faida for 8yrs kwa madai ya de beers, barick na makampuni kibao ya wawekezaji yanaiibia TZ

shell wanatapeli nigeria
mifano ipo mingi accross africa
wawekezaji wanachota africa watakavyo ndio maana yake nimeonya hamna watu corrupt kama wawekezaji
 
2009-03-21 - ipp media
By Bilham Kimati

As the heated debate on whether the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) should or should not buy the Dowans Power Plant comes to a close, it has been hinted that Songas Power Company is now the potential buyer of the machines, The Guardian has learnt allayed fears over power rationing should the weather forecasts behave accordingly.

shareholders wa songas ni

1.Globeleq
2.Tanzania Petroleum Development Corporation - TPDC (100% mali ya umma)
3.Tanzania Electricity Supply Company Limited - TANESCO (100%mali ya umma)
4.Tanzania Development Finance Company Limited - TDFL (32% mali ya umma)
5.FMO YA HOLLAND

>>>>> Songas Limited shareholders <<<<<

kutokana na hao shareholders hapo juu, TPDC, TANESCO NA TDFL ni mali ya yetu wenyewe hili sio GOLI LA KISIGINO KWELI?

SIO SERIKALI INATAKA KUNUNUA KUPITIA MLANGO WA NYUMA?

"SAY NO TO SONGAS"

CCM hawana pesa za kugharamia uchaguzi ujao. Rostam kishawaahidi labda 20% au zaidi kama atauza mitambo yake chakavu ya Richmond/Dowans kwa serikali. Hivyo serikali inajitahidi kupitia mlango wa nyuma ili kuhakikisha ununuzi wa mitambo hiyo bila woga wala aibu. Kwetu sisi Watanzania ni kuwa macho na kupinga ununuzi huo maana Songa mashareholders wake ni makampuni yanayomilikwa na Watanzania.

Huyu Rostam kwa jinsi alivyohusika na kashfa mbali mbali nchi hata kiburi cha kuongea hadharani angekuwa hana, lakini anajua Kikwete yuko mfukoni mwake na hawezi kusema au kufanya lolote dhidi yake ndiyo maana anapata kiburi kama alichokuwa nacho bahati mbaya hajui kwamba Watanzania sasa tumeamka tumeshachoshwa na mafisadi wanaotufisadi kila kukicha na kuwaacha Watanzania walio wengi wakiishi maisha ya dhiki kubwa. Tutapambana nao na kuhakikisha mtambo huo chakavu haununuliwi na Songa. Waungwana kama anayejua TANESCO, TPDC, TDFL na shirika lolote la Watanzania yanamiliki asilimia ngapi ya shares za Songa aweke hapa mchanganuo huo.

Alutta Continua!
 
Mkuu Semilong,

Unarahisisha mambo utafikiri hiyo kampuni ya kuuza nyanya?

Hayo makampuni mengine yana shareholders wengine wengi tu, wanafuata corporate governance na accounting principles. Unachokisema kinawezekana tu kwenye mashirika yetu ya umma yanayoendeshwa kisiasa.

Kama Songas watanunua huo mtambo ni kwasababu wameona opportunity ambayo sisi hatukuiona na wameamua kuitumia. Its the economy, stupid!

Waswahili husema kizuri cha-jiuza kibaya cha-jitembeza. Hizo generators zingekuwa na "opportunity" unayozungumzia wewe wala hakungekuwa na kulazimishana kuuziana kama ilivyo sasa. Tafadhali wacheni kutulazimisha kununua vimeo vyenu.....
 
Watu walishaseiku nyingi hapa hata tukipiga kelele namna gani mitambo lazima inunuliwe kwani kutonunuliwa nihasara kwa CCM, Mtake msitake mitambo lazima inunuliwe.

Lakini nashangaa kitu kimoja kwanini mkuu wa nchi yuko kimya kwenye issue ya hii mitambo? au anangoja inunuliwe baada ya miaka 2 iharibike ndio aje na tume ya kuchunguza ununuzi wa mitambo ya RD
 
tk.... hivi haya majenereta yenu mmekosa kabisa sehemu ya kuyauza??

Used Generators ziko nyingi sana tuu, hata ukitaka website za kuuza zipo. Sasa wao kuuza itakuwa kazi sana na bei ndio kama wanayosema ndio kabisaa.
 
Iko mbaya gani. Shareholders watatu in red hapo juu ni private investors. Kwa hiyo Songas inaendesha shughuli zake kwa misingi ya kibiashara siyo kama mashirika yetu ya umma yanavyoendeshwa kwa misingi ya kisiasa.

Kufuatana na hali ya umeme nchini, this is a good business opportunity for anyone with brains kununua hiyo mitambo maana itahitajika tu hata Tanesco wanunue mitambo hiyo mipya.

Hapo Tanesco itapoanza kuwalipa capacity charges na Songas kuongeza faida yao, ndio wale wanaopinga ununuzi wa mitambo ya Dowans watapoona makosa waliyoyafanya. Na Bunge litaangalia hivi hivi bila kuwa na lolote la kufanya kwani halima mandate ya kuingilai utendaji wa Songas.

ungetegemea mawazo ya aina hii yatoke kwa mtu asiye Mtanzania,na asiye na uchungu na nchi iitwayo Tanzania....inasikitisha sana kuona hadi leo baadhi ya Watanzania wenzetu wanajifanya hawasikii maumivu ya ufisadi.

Eti "IKO MBAYA GANI"....Ina maana hujui kwamba Dowans ni Richmond-kampuni ya kitapeli iliyopelekea Lowassa,Msabaha na Karamagi kuachia ngazi?Labda kwako hapo HAKUNA MBAYA kwa vile it seems it's OK kwa wewe na wenye mtazamo kama wako kwa nchi yetu kufanyiwa daylight robbery huku wahanga wakiwa mimi na wewe na walalahoi wengine (tax payers).

NI MBAYA kwa vile baada ya mafisadi kugundua kuwa janja yao ya kununua mitambo ya Dowans kupitia Tanesco inaelekea kukwama,sasa wanatumia mlango wa uani through Songas.Dowans ni kampuni ya kijambazi,and so are its mitambo yake.Hii ni sawa na wewe kuibiwa gari lako,kisha likapelekwa showroom baada ya kubadilishwa rangi,then ukauziwa tena!Kama hiyo sio MBAYA KWAKO then you are highly unlikely to be a true Tanzanian!

Private investment is in no way whatsoever a free pass for economic sabotage.
 
17th October 2001

In a $310-million project, the Songo Songo gasfield, off the Tanzanian coast, will be developed; gas will be processed at a plant on the nearby Songo Songo island, and the product (in gas form) transported through a pipeline to Dar es Salaam, Tanzania's capital. Power generated from the gas could also be exported to neighbouring countries, and the extension of the pipeline to Mombasa can supply energy to the Kenyan market.

In Dar es Salaam the gas will be used to fuel gas turbines for power generation.

The project will generate its revenue from the sale of electricity to the state-owned utility Tanzania Electric Supply Company Limited (Tanesco).

Songas is a Tanzanian company created to develop the Songo Songo gas-to-electricity project, and to own and operate all of the project facilities. The lead sponsors of the project are the AES Corporation, based in Arlington, Virginia, US, and the PanAfrican Energy Corporation, based in Jersey, on the Channel Islands. The project has been developed in partnership with the Ministry of Energy and Minerals of the Tanzanian government, Tanesco, and Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), the state-owned oil and gas exploration company &#8211; all of which are partners and shareholders in Songas. The lenders are the World Bank and the European Investment Bank.

The developer expects to reach financial closure on the project this month, and to have Songo Songo natural gas in Dar es Salaam in the fourth quarter of 2003. The McConnel Dowell/Grinaker LTA joint venture, consisting of Australian and South African companies respectively, have been prequalified for the gas processing and marine pipeline engineering, procurement and construction contract; as well as the land pipeline engineering, procurement and construction contract.

For more information, see Engineering News Oct 5 to 11, 2001, or contact Songas, Jim McCardle, tel +255-22-211-7313 or at info@songas.com
 
maskini Watanzania............hakuna mtu wa kuwatetea.....tunapigwa makonde kila upande........dah

TDFL ni shirika/kampuni la/ya Serikali
 
Si jambo la busara both in moral and legal authority kwa Tanesco kujihusisha kwa namna moja au nyingine kununua mitambo hiyo kwa mlango wa nyumba...

Tumeambiwa hapo juu kwamba Tanzania Electricity Supply Company Limited ina 100% shares, hivyo hatujui kama wao ni moja ya majority au preferancial sharehoders

Tunachojua ni kwamba- TANESCO ni public utility company 100% publicly owned na kutokana na yaliyokwisha tokea , It is tantamount to public interest kwa Tanesco kujihusisha na manunuzi hayo hayo...

sijui ni kwanini Tanesco wanang'ang'ana sana na mamitambo hayo yenye na yaliyowafanyia nuski kwa kiasi kikubwa sana, mbona hawaamuki? Jameni hebu tuambieni sababu za msingi kwa Tanesco kutaka kununua kwa udi na uvumba maana inabidi wakuu wake wawajibishwe kwa kutotimiza majukumu yao ipasavyo...

Tanesco wana monopoly ya power supply NCHI NZIMA lakini hadi wakati huu niandikapo, jukumu lao la kusambaza umeme mpaka kijijini kwetu bado hawajalitimiza...

Watafute basi vyanzo mbadala kama maji maana mito iko lukuki Tanzania na kinachohitajika ni recycling tu ya hayo maji, Kiangazi pia masika umeme hakuna Giza Nchi NZIMA...

asante....
 
Jamani hivi kuna mtu anaweza kuni PM namba ya Mhe. Zitto maana nafikiri nahitaji labda kuondolewe ukilaza huu, wat's so special kwa hii mitambo ihali ni mitumba? Kwanini serikali inaing'ang'ania na haiweki wazi sababu za msingi kwa wananchi? Im starting to smell something and it smells unpleasant as far as this creature is concerned (Dowans)
 
2009-03-21 - ipp media
By Bilham Kimati

As the heated debate on whether the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) should or should not buy the Dowans Power Plant comes to a close, it has been hinted that Songas Power Company is now the potential buyer of the machines, The Guardian has learnt allayed fears over power rationing should the weather forecasts behave accordingly.

shareholders wa songas ni

1.Globeleq
2.Tanzania Petroleum Development Corporation - TPDC (100% mali ya umma)
3.Tanzania Electricity Supply Company Limited - TANESCO (100%mali ya umma)
4.Tanzania Development Finance Company Limited - TDFL (32% mali ya umma)
5.FMO YA HOLLAND

>>>>> Songas Limited shareholders <<<<<

kutokana na hao shareholders hapo juu, TPDC, TANESCO NA TDFL ni mali ya yetu wenyewe hili sio GOLI LA KISIGINO KWELI?

SIO SERIKALI INATAKA KUNUNUA KUPITIA MLANGO WA NYUMA?

"SAY NO TO SONGAS"

kama kuna mtu anajua % ya shares za songas, kwa kila kampuni tuwekee please

Conflict of interest. Mgongano wa maslahi.
 
Jamani Globeleq ni leading shareholder anamiliki 59% akifuatiwa na TANESCO anamiliki 21% na TPDC wao wanamiliki 12% na TDFL wana 4% na zilizobaki ni hao jamaa wa Holland na hizi ni za kweli kwamba Songas wame bid kutaka kununua hiyo mitambo ya Dowans,habari ndo hiyo
 
ungetegemea mawazo ya aina hii yatoke kwa mtu asiye Mtanzania,na asiye na uchungu na nchi iitwayo Tanzania....inasikitisha sana kuona hadi leo baadhi ya Watanzania wenzetu wanajifanya hawasikii maumivu ya ufisadi.

Eti "IKO MBAYA GANI"....Ina maana hujui kwamba Dowans ni Richmond-kampuni ya kitapeli iliyopelekea Lowassa,Msabaha na Karamagi kuachia ngazi?Labda kwako hapo HAKUNA MBAYA kwa vile it seems it's OK kwa wewe na wenye mtazamo kama wako kwa nchi yetu kufanyiwa daylight robbery huku wahanga wakiwa mimi na wewe na walalahoi wengine (tax payers).

NI MBAYA kwa vile baada ya mafisadi kugundua kuwa janja yao ya kununua mitambo ya Dowans kupitia Tanesco inaelekea kukwama,sasa wanatumia mlango wa uani through Songas.Dowans ni kampuni ya kijambazi,and so are its mitambo yake.Hii ni sawa na wewe kuibiwa gari lako,kisha likapelekwa showroom baada ya kubadilishwa rangi,then ukauziwa tena!Kama hiyo sio MBAYA KWAKO then you are highly unlikely to be a true Tanzanian!

Private investment is in no way whatsoever a free pass for economic sabotage.

Mlalahoi.
Mimi nadhani Watanzania wenye mawazo kama yako bado wamelala usingizi. Naona mnadhani nchi hii bado ni ya kijamaa. Mnazungumza tu habari ya uzalendo kwa kupiga mdomo wakati wenzenu wanafanya kazi zao chini ya mfumo wa sasa wa sera ya nchi kuwa ni private sector ndiyo itakayo endesha uchumi wa nchi hii na serikali itajenga tu mazingira mazuri ya kuiwezesha private sector kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Sasa watu kama ninyi badala ya kutafuta njia ya kujipenyeza ndani ya private sector, bado mnazembea kuchangamka mnadhani ni enzi zile za Nyerere na Ujamaa. Mambo yamebadilia Mzee. Katika ubepari mwenye kisu kikali ndio hula nyama.

Ninyi mmekaa tu na kupiga kelele Dowans! Dowans! Ufisadi ! Ufisadi!, wakati wenzenu wanafanya mambo yao and within the law kama hao Songas. Hebu soma hiyo article ya Babu Ataka Kusema huenda ikakuzibua maskio.

Najua Watanzania kama mmoja mmoja hawana uwezo, lakini badala ya kupoteza muda wetu kutoa theories za ndoto kwa nini msifanye jambo la maendeleo kwa mfano kuiga mfano wa NICO? Jiungeni katika vikundi vya kiuchumi na muanze kushiriki katika uchumi wenu. Huo mdomo mdomo wenu utawaacha muwe kila siku maboi wa wawekezaji. (Nasaha tu ndugu yangu usikasirike)
 
Jamani Globeleq ni leading shareholder anamiliki 59% akifuatiwa na TANESCO anamiliki 21% na TPDC wao wanamiliki 12% na TDFL wana 4% na zilizobaki ni hao jamaa wa Holland na hizi ni za kweli kwamba Songas wame bid kutaka kununua hiyo mitambo ya Dowans,habari ndo hiyo

Asante kwa taarifa hizi, sasa cha muhimu ni kuzingatia pia kuwa kama 37% iko katika mikono ya serikai kwa njia moja au nyingine na Tanesco ndo mteja wa Songas basi wana-influence kubwa zaidi.
Anyway, Tanzanians have a stake in Songas through Tanesco, kwa hiyo tunawezakushinikiza na kusema kuwa Songas kama Songas haiwezi kununua mitambo ya Dowans kwa kutumia pesa za Tanesco - dividend yake, capital yake etc. Labda hizo pesa wazitoe Uholanzi. Otherwise there is no change from the original plan and the government is putting money into buying Dowans.
BTW kwa wale wanaotetea ununuzi naomba kuuliza kwa nini Songas hawakununua mitambo ya Aggreko? Na kwa nini serikali haikung'ang'ania kununua mitambo ya Aggreko?
 
Sasa naanza kuelewa ukimya wa serikali na rais la kukaa kimya pasipo kuchukua hatua zozote za kuatafuta alternative katika tatizo hilo mbali na dowans wakati tumeisha tishiwa ya kua taifa litabaki gizani.Serikali ilisha amua zamani kununua mitambo hiyo nasitashanga ya kwamba uwenda kuankiasi cha pesa kimeishalipwa!Hilo soo lililokua likiendelea is just formality.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mlalahoi.
Mimi nadhani Watanzania wenye mawazo kama yako bado wamelala usingizi. Naona mnadhani nchi hii bado ni ya kijamaa. Mnazungumza tu habari ya uzalendo kwa kupiga mdomo wakati wenzenu wanafanya kazi zao chini ya mfumo wa sasa wa sera ya nchi kuwa ni private sector ndiyo itakayo endesha uchumi wa nchi hii na serikali itajenga tu mazingira mazuri ya kuiwezesha private sector kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Sasa watu kama ninyi badala ya kutafuta njia ya kujipenyeza ndani ya private sector, bado mnazembea kuchangamka mnadhani ni enzi zile za Nyerere na Ujamaa. Mambo yamebadilia Mzee. Katika ubepari mwenye kisu kikali ndio hula nyama.

Ninyi mmekaa tu na kupiga kelele Dowans! Dowans! Ufisadi ! Ufisadi!, wakati wenzenu wanafanya mambo yao and within the law kama hao Songas. Hebu soma hiyo article ya Babu Ataka Kusema huenda ikakuzibua maskio.

Najua Watanzania kama mmoja mmoja hawana uwezo, lakini badala ya kupoteza muda wetu kutoa theories za ndoto kwa nini msifanye jambo la maendeleo kwa mfano kuiga mfano wa NICO? Jiungeni katika vikundi vya kiuchumi na muanze kushiriki katika uchumi wenu. Huo mdomo mdomo wenu utawaacha muwe kila siku maboi wa wawekezaji. (Nasaha tu ndugu yangu usikasirike)

Mkuu TK,

Umenena yote. Hawa Wazalendo wa maneno huku kwenye matendo hakuna wanachofanya
kusaidia kutatua hili suala la umeme na matatizo mengine ya nchi, kwa kweli ni politics.

Tanesco wametangaza tender ya kununua generators, mimi nawashauri wazalendo nyie wa TZ anzisheni kampuni yenu ili muweze ku bid na kushinda tender ya kuwaletea Tanesco generators. Wazalendo nyie si mnajua wapi hiyo mitambo inauzwa bei chee? Badala ya maneno matupu nafikiri huu ndio muda muafaka wa matendo.

Uchumi na siasa haviendi pamoja. Ukijaza siasa kwenye uchumi, unaishia kama Mugabe. Mwalimu alijaribu alipoona yanamshinda, alikuwa na akili, akakubali ukweli na kumwachia Mwinyi afanye mabadiliko.

Its no brainer kujua kwamba demand ya umeme kwa TZ ni kubwa na hata uwe na mtambo wa zamani bado utapata faida na kurudisha pesa zako haraka. Songas wameangalia huo ukweli na kwasababu ni mabepari watahakikisha wanapata hiyo mitambo kwa bei nzuri, watatengeneza umeme na kutuuzia sisi Wadanganyika kwa bei ya juu na faida yake kubwa kuitoa nje ya nchi. Sisi tutaendelea kuimba wimbo wetu wa uzalendo wa maneno huku wananchi wetu wengi hawana kazi, viwanda havizalishi ipasavyo shauri ya matatizo ya umeme, ajira kwa vijana mbovu, pato la taifa linashuka.

Amkeni ndugu zangu, tangulizeni mbele uchumi kuliko siasa.

Hivi ule mwongozo wa Tanu ulikuwa unasemaje? "Kitendo chochote kinachomwongezea mtu uwezo/uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe, ni kitendo cha maendeleo hata kama hakiongozi tija wala pato" Kwi kwi kwi!!!
 
Back
Top Bottom