Songas to buy Dowans generators?

Songas to buy Dowans generators?

Jamani Globeleq ni leading shareholder anamiliki 59% akifuatiwa na TANESCO anamiliki 21% na TPDC wao wanamiliki 12% na TDFL wana 4% na zilizobaki ni hao jamaa wa Holland na hizi ni za kweli kwamba Songas wame bid kutaka kununua hiyo mitambo ya Dowans,habari ndo hiyo

Kocha tupe, Songas wame bid kununua kwa shillingi ngapi?
 
Asante kwa taarifa hizi, sasa cha muhimu ni kuzingatia pia kuwa kama 37% iko katika mikono ya serikai kwa njia moja au nyingine na Tanesco ndo mteja wa Songas basi wana-influence kubwa zaidi.
Anyway, Tanzanians have a stake in Songas through Tanesco, kwa hiyo tunawezakushinikiza na kusema kuwa Songas kama Songas haiwezi kununua mitambo ya Dowans kwa kutumia pesa za Tanesco - dividend yake, capital yake etc. Labda hizo pesa wazitoe Uholanzi. Otherwise there is no change from the original plan and the government is putting money into buying Dowans.
BTW kwa wale wanaotetea ununuzi naomba kuuliza kwa nini Songas hawakununua mitambo ya Aggreko? Na kwa nini serikali haikung'ang'ania kununua mitambo ya Aggreko?

Mkuu Susuviri,

Nakuelewa hapo juu una maana gani lakini kwenye supply and demand relationship, nguvu ya Tanesco ni ndogo sana kwasabu suplliers wa umeme ni wachache kuliko mahitaji ya Tanesco.

Wewe unahitaji umeme kwasababu nusu ya nchi iko kwenye giza, kweli utakuwa hata na uwezo wa kumwuliza mzalishaji, huu umeme umeutoa wapi?

Njia tulizotumia kuuza mashirika yetu sitashangaa hata kuona huko Songas sehemu kubwa kwenye management ni wageni na maamuzi yote yanategemea wao. Pia wao wana ni majority shares.

Kuhusu hiyo mitambo mingine, hivi na wenyewe walikuwa wanauza? Mimi nafikiri Aggreko wameamua kuihamishia mitambo yao sehemu nyingine, hawauzi. Dowans hawana kwa kukimbilia, yaani kama ni mimi nanunua hiyo mitambo, nitapata kwa bei ya chini mno. Songas watapata deal kubwa kwenye hili suala ndio maana wameamua kuingiza vichwa vyao pamoja na kujua kwamba huenda sehemu kubwa ya Watanzania wako against, kwenye PR uamuzi kama huo unaweza kuwa dissaster, lakini kwenye kiuchumi unaweza kuwa bora mno.
 
Mkumbuke kuwa kuna Brigedia alitoa $ milloni mbili kumfadhili muungwana ili kufaniakisha kupata ufalme nae AMEAHIDI KUWA LIWE NALIWALO LAZIMA MITAMBO ITANUNULIWA;kwahiyo lazima zitafutwe njia zozote zile haramu ili kufanikisha zoezi hili; EBO!! mnafikili muungwana alipitia Dubai kufanya nini? Kunywa kahawa sio?
 
bado nafikiri huenda likawa ni goli la kisigino, ni namna tu ya kuiosha (launder) Dowans kwa kupitia Songas. Baada ya hapo tuitasikia Songas iinataka kuiuzia mitambo Tanesco -- na mjadala kurudi back to square one. Mafisadi wanapodhamiria, na hasa wakiwa na backing ya kutoka top, basi kila mbinu zitatafutwa na kuzitekeleza.

Tatizo mwenye hiyo mitambo anataka fedha na ameiahidi CCM kuwa 2010 ni ngumu kupata hela za chee -- hakuna tena EPA, Deep Gree, Meremeta, Twin Towers au nini. Mradi wa Vitambulisho pia umekwama, kwani tunasikia wafadhili wamemwambia JK huko London aachane nao ama sivyo asionekane tena maeneo ya huko na bakuli lake. Kilichobakia ni Dowans, DOWANS, DOWANS, DOWANS, maana hela zipo kutoka Hazina za kumpa huyu bwana na kuiokoa CCM1
 
bado nafikiri huenda likawa ni goli la kisigino, ni namna tu ya kuiosha (launder) Dowans kwa kupitia Songas. Baada ya hapo tuitasikia Songas iinataka kuiuzia mitambo Tanesco -- na mjadala kurudi back to square one. Mafisadi wanapodhamiria, na hasa wakiwa na backing ya kutoka top, basi kila mbinu zitatafutwa na kuzitekeleza.

Tatizo mwenye hiyo mitambo anataka fedha na ameiahidi CCM kuwa 2010 ni ngumu kupata hela za chee -- hakuna tena EPA, Deep Gree, Meremeta, Twin Towers au nini.
Mradi wa Vitambulisho pia umekwama, kwani tunasikia wafadhili wamemwambia JK huko London aachane nao ama sivyo asionekane tena maeneo ya huko na bakuli lake.
Kilichobakia ni Dowans, DOWANS, DOWANS, DOWANS, maana hela zipo kutoka Hazina za kumpa huyu bwana na kuiokoa CCM1

habari ndio hiyo ya vitambulisho
 
Mkuu Semilong,

Unarahisisha mambo utafikiri hiyo kampuni ya kuuza nyanya?

Hayo makampuni mengine yana shareholders wengine wengi tu, wanafuata corporate governance na accounting principles. Unachokisema kinawezekana tu kwenye mashirika yetu ya umma yanayoendeshwa kisiasa.

Kama Songas watanunua huo mtambo ni kwasababu wameona opportunity ambayo sisi hatukuiona na wameamua kuitumia. Its the economy, stupid!

Mtanzania, hakuna viable business opportunity katika ununuzi wa mitambo ya Dowans rather than political lobbying and corruption. Naifahamu kampuni ya Globeleq ni moja ya kampuni kubwa sana na hiyo Songo gas ni just a subsidiary company ya Globeleq. Mkataba wa Songogas still haujakaa vizuri hata kidogo so songogas hata wakiwa lobbed kununua kwa prevailing shit price still they cant make loss but rather constrain profit level to normal profit given current contract. Hivyo hoja yako haijustify kuwa maamuzi ya kupinga ununuzi hayakuzingatia maslahi ya nchi.
 
Hili la TANESCO kuwa na hisa kwenye Songas na hata TPDC na TDFL linanipa shida.

Hivi washinddani wa Songas, nikiwa na maana Agrekko, ITPL, Kiwira, Dowans an PPEL watasemaje kuona kuwa mshindani wao Songas anamilikiwa kwa kiasi fulani na mteja wao Tanesco na wachuuzi kama TPDC?

Hiyo si Konfliti of Interest au bado tunafumbia macho?

No wonder bei za umeme Tanzania ni kubwa na za kutisha!
 
Hili la TANESCO kuwa na hisa kwenye Songas na hata TPDC na TDFL linanipa shida.

Hivi washinddani wa Songas, nikiwa na maana Agrekko, ITPL, Kiwira, Dowans an PPEL watasemaje kuona kuwa mshindani wao Songas anamilikiwa kwa kiasi fulani na mteja wao Tanesco na wachuuzi kama TPDC?

Hiyo si Konfliti of Interest au bado tunafumbia macho?

No wonder bei za umeme Tanzania ni kubwa na za kutisha!

Nadhani kitu ambacho kingestahili kuwepo nikuwa, kwa kuwa Serikali ina interest kwenye Songas though Tanseco, TPDC and partly TDFL, then apart from dividends, (kama ipo), nchi ingebidi kupata additional benefit, through hiyo association, kwa Songas not to charge capacity charges au ku charge proportionetly less compared to haya makampuni ambayo ni 100% private.
 
Iko mbaya gani. Shareholders watatu in red hapo juu ni private investors. Kwa hiyo Songas inaendesha shughuli zake kwa misingi ya kibiashara siyo kama mashirika yetu ya umma yanavyoendeshwa kwa misingi ya kisiasa.

Kufuatana na hali ya umeme nchini, this is a good business opportunity for anyone with brains kununua hiyo mitambo maana itahitajika tu hata Tanesco wanunue mitambo hiyo mipya.

Hapo Tanesco itapoanza kuwalipa capacity charges na Songas kuongeza faida yao, ndio wale wanaopinga ununuzi wa mitambo ya Dowans watapoona makosa waliyoyafanya. Na Bunge litaangalia hivi hivi bila kuwa na lolote la kufanya kwani halima mandate ya kuingilai utendaji wa Songas.

Umefanya homework yako vizuri.
Ukiwa biased wakati wa analysis, YOU WILL ALWAYZ MISS SOME IMPORTANT POINTS.....
 
Mkuu TK,

Umenena yote. Hawa Wazalendo wa maneno huku kwenye matendo hakuna wanachofanya
kusaidia kutatua hili suala la umeme na matatizo mengine ya nchi, kwa kweli ni politics.

Tanesco wametangaza tender ya kununua generators, mimi nawashauri wazalendo nyie wa TZ anzisheni kampuni yenu ili muweze ku bid na kushinda tender ya kuwaletea Tanesco generators. Wazalendo nyie si mnajua wapi hiyo mitambo inauzwa bei chee? Badala ya maneno matupu nafikiri huu ndio muda muafaka wa matendo.

Mtanzania,
Kampuni tayari tumeshaanzisha, inaitwa TANESCO. Tatizo ni kuwa mafisadi unaowashabikia wamejaribu kuiteka nyara ili wao wawe ni ma-Middle Men kwenye manunuzi yoyote Tanesco inayotaka kufanya.

Kama ni used generators ziko kibao, mpya hazichukui zaidi ya miezi sita. Kwa mfano, kwa haraka tu nime-google na kupata hawa jamaa;

Gas Turbines Generators 30Mw-55Mw

GAS TURBINES INTERNATIONAL - Ground Power Packages

 
17th October 2001

In a $310-million project, the Songo Songo gasfield

kwani serikali ilishindwa kufanya yenyewe ukizingatia faida yake sasa hivi siwangekua wamerudish $310m

Hawataki kuendeleza nchi wanachotaka ni kuiibia tu kwa kutumia kalamu.

Fikiria, hatuku-invest $310million kwenye Songo Songo gas lakini;
  1. Tuliweza $200million kwenye Twin Towers
  2. Na sasa tunataka kupoteza $150 millioni kwenye ambavyo hata US, RSA n.k, hawana na 80% ya Tanzania haina umeme wa kuvisoma,
  3. Hapo usiseme pesa za EPA, BOT, IPTL, Richmond n.k.
Tanzania tungekuwa mbali sana kama Mkapa wa kabla ya Nyerere kufariki angeendelea kuongoza nchi. Bahati mbaya alifanya 180 degree na kumrudisha Lowassa, mengine ni historia.
 
Hapo Tanesco itapoanza kuwalipa capacity charges na Songas kuongeza faida yao, ndio wale wanaopinga ununuzi wa mitambo ya Dowans watapoona makosa waliyoyafanya. Na Bunge litaangalia hivi hivi bila kuwa na lolote la kufanya kwani halima mandate ya kuingilai utendaji wa Songas.
Jamani naomba kueleweshwa kidogo. Labda nianze kwakutumia example say:

Kampuni A = dalali wa kuuza magari
Kampuni B = kampuni yaku azimisha magari (car hire firm)
Tatizo X = magari ya wizi kutoka Africa Kusini

Je kama Serekali imejaribu kununua magari kutoka kwa Kampuni A kwa maitaji ya dharula(ka mkutano wakimataifa).

Wanaichi wamepiga mayowe kwamba hayo magari ya Kampuni A yasinunuliwe kwasababu ni MITUMBA.
Sheria za ununuzi zinasema Serekali lazma inunue magari "Brand New" kama wanataka.

Wakati mvutano unaendela, inakuja kugundulika kwamba magari ya Kampuni A yana Tatizo X, kosa ambalo aliruhusiwi kwenye procument process ya nchi(na kuweza kubatilisha mkataba kama ukifanyika).

Kuna uwezekano mkubwa pia kwamba Kampuni A inaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa
hilo(Tatizo X).

Serekali imekodishwa magari kwa mkataba na Kapuni B kwa mda ili kumudu matumizi yakawaida.

Kapuni A imeshindwa kumuuzia Serekali magari yake kwasababu ni MITUMBA na Tatizo X bado lipo lakini limechuniwa.

Kapuni A inasuka mpango na wahusika kumuuzia Kapuni B magari yake.ilikukwepa kipengele cha ununuzi wa "Brand New" Serekalini.

Kapuni B ikinunua hayo magari nakutaka kunigia kwenye mkataba mwingine na Serekali, lakini huu mkataba mpya uwe wa-mda kumudu dharula Serekalini.

Je huo mkataba mpya na Serekali utakua umeliondoa kosa ya kwamba hayo magari bado yana Tatizo X?
 
Jamani naomba kueleweshwa kidogo. Labda nianze kwakutumia example say:

Kampuni A = dalali wa kuuza magari
Kampuni B = kampuni yaku azimisha magari (car hire firm)
Tatizo X = magari ya wizi kutoka Africa Kusini

Je kama Serekali imejaribu kununua magari kutoka kwa Kampuni A kwa maitaji ya dharula(ka mkutano wakimataifa).

Wanaichi wamepiga mayowe kwamba hayo magari ya Kampuni A yasinunuliwe kwasababu ni MITUMBA.
Sheria za ununuzi zinasema Serekali lazma inunue magari "Brand New" kama wanataka.

Wakati mvutano unaendela, inakuja kugundulika kwamba magari ya Kampuni A yana Tatizo X, kosa ambalo aliruhusiwi kwenye procument process ya nchi(na kuweza kubatilisha mkataba kama ukifanyika).

Kuna uwezekano mkubwa pia kwamba Kampuni A inaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa
hilo(Tatizo X).

Serekali imekodishwa magari kwa mkataba na Kapuni B kwa mda ili kumudu matumizi yakawaida.

Kapuni A imeshindwa kumuuzia Serekali magari yake kwasababu ni MITUMBA na Tatizo X bado lipo lakini limechuniwa.

Kapuni A inasuka mpango na wahusika kumuuzia Kapuni B magari yake.ilikukwepa kipengele cha ununuzi wa "Brand New" Serekalini.

Kapuni B ikinunua hayo magari nakutaka kunigia kwenye mkataba mwingine na Serekali, lakini huu mkataba mpya uwe wa-mda kumudu dharula Serekalini.

Je huo mkataba mpya na Serekali utakua umeliondoa kosa ya kwamba hayo magari bado yana Tatizo X?

Naona kuna dosari katika equation yako nayo ni tatizo "X". Hakuna wizi hapa ama sivyo hayo magari ya Afrika kusini, kama yangekuwa ya wizi, yangekwisha kamatwa. Sema hivi "tatizo X = Magari yaliyo nunuliwa na mtu asiyetakiwa na wabunge A,B,C.
Hapo utaona kuwa hakuna dosari yoyote kwa kampuni B kununua hayo magari na kuyakodisha maana yako nchini kisheria. Ingekuwa ya wizi yangekwisha kamatwa.
 
Mlalahoi.
Mimi nadhani Watanzania wenye mawazo kama yako bado wamelala usingizi. Naona mnadhani nchi hii bado ni ya kijamaa. Mnazungumza tu habari ya uzalendo kwa kupiga mdomo wakati wenzenu wanafanya kazi zao chini ya mfumo wa sasa wa sera ya nchi kuwa ni private sector ndiyo itakayo endesha uchumi wa nchi hii na serikali itajenga tu mazingira mazuri ya kuiwezesha private sector kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Sasa watu kama ninyi badala ya kutafuta njia ya kujipenyeza ndani ya private sector, bado mnazembea kuchangamka mnadhani ni enzi zile za Nyerere na Ujamaa. Mambo yamebadilia Mzee. Katika ubepari mwenye kisu kikali ndio hula nyama.

Ninyi mmekaa tu na kupiga kelele Dowans! Dowans! Ufisadi ! Ufisadi!, wakati wenzenu wanafanya mambo yao and within the law kama hao Songas. Hebu soma hiyo article ya Babu Ataka Kusema huenda ikakuzibua maskio.

Najua Watanzania kama mmoja mmoja hawana uwezo, lakini badala ya kupoteza muda wetu kutoa theories za ndoto kwa nini msifanye jambo la maendeleo kwa mfano kuiga mfano wa NICO? Jiungeni katika vikundi vya kiuchumi na muanze kushiriki katika uchumi wenu. Huo mdomo mdomo wenu utawaacha muwe kila siku maboi wa wawekezaji. (Nasaha tu ndugu yangu usikasirike)

Mkuu TK,

Umenena yote. Hawa Wazalendo wa maneno huku kwenye matendo hakuna wanachofanya
kusaidia kutatua hili suala la umeme na matatizo mengine ya nchi, kwa kweli ni politics.

Tanesco wametangaza tender ya kununua generators, mimi nawashauri wazalendo nyie wa TZ anzisheni kampuni yenu ili muweze ku bid na kushinda tender ya kuwaletea Tanesco generators. Wazalendo nyie si mnajua wapi hiyo mitambo inauzwa bei chee? Badala ya maneno matupu nafikiri huu ndio muda muafaka wa matendo.

Uchumi na siasa haviendi pamoja. Ukijaza siasa kwenye uchumi, unaishia kama Mugabe. Mwalimu alijaribu alipoona yanamshinda, alikuwa na akili, akakubali ukweli na kumwachia Mwinyi afanye mabadiliko.

Its no brainer kujua kwamba demand ya umeme kwa TZ ni kubwa na hata uwe na mtambo wa zamani bado utapata faida na kurudisha pesa zako haraka. Songas wameangalia huo ukweli na kwasababu ni mabepari watahakikisha wanapata hiyo mitambo kwa bei nzuri, watatengeneza umeme na kutuuzia sisi Wadanganyika kwa bei ya juu na faida yake kubwa kuitoa nje ya nchi. Sisi tutaendelea kuimba wimbo wetu wa uzalendo wa maneno huku wananchi wetu wengi hawana kazi, viwanda havizalishi ipasavyo shauri ya matatizo ya umeme, ajira kwa vijana mbovu, pato la taifa linashuka.

Amkeni ndugu zangu, tangulizeni mbele uchumi kuliko siasa.

Hivi ule mwongozo wa Tanu ulikuwa unasemaje? "Kitendo chochote kinachomwongezea mtu uwezo/uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe, ni kitendo cha maendeleo hata kama hakiongozi tija wala pato" Kwi kwi kwi!!!

Naendelea kushawishika kuwa wenye mawazo ya kutetea majambazi basi aidha nao ni majambazi au wananufaika na ujambazi huo.Eti private sector!Kwani private sector ndio kibali cha kuiibia Tanzania?

Anyway,naamini kuwa mioyoni mwenu mnaungana nami kuwa hawa majambazi wa Dowans et al lazima wakaliwe kooni LAKINI nashawishika kumini kuwa utetezi wenu ni sehemu za mkakati wa kufikia malengo yenu.Mtasema kila kitu,from private sector to kufa kwa ujamaa lakini UFISADI ni UFISADI tu.Yeah,inawezekana kelele zetu haziwanyimi usingizi Mafisadi na vibaraka wao (most of whom ni walalahoi wanaojikomba ilimradi tu mkono uende kinywani) lakini hiyo sio sababu ya sie kukaa kimya....ndio maana Jesus na Muhammad hawaku-give up kueneza neno la Mungu ati kwa vile tu kulikuwa na vichwa ngumu flani waliogoma kukubali.

Second to UFISADI,ni NJAA za vibaraka wa mafisadi.
 
Second to UFISADI,ni NJAA za vibaraka wa mafisadi.

Ahsante sana kwa kashfa yako. Sisi umetufikiria hivyo, sijui wewe nawe ukichunguzwa utakutwa kwenye kundi gani. Ni Mlalahoi kweli au umejaa kishenzi, isipokuwa tu malalamiko yako kwa hao mafisadi ni washindani wako wa kishughuli tu (kama kulangua viwanja!!). Conflic of interest???
 
Tk,
Mkuu hayo ya kutopendwa na wabuinge A B C nadhani sasa tuseme hivi.. maanake imekuwa ujinga sasa.. Hiyo kampuni A ni ya Mwarabu, Muislaam na wote tunaopinga ununuzi ni Weusi na Wakristu..nadhani itakuwa tamu zaidi ktk hoja za Conflict of Interest..
Ni mawazo ya kipuuzi kama haya siku zote yanaturudisha nyuma kiasi kwamba hata rais akimchagua mtu kuongoza shirika mnatazama kwanza dini yake, kabila yake badala ya uwezo wa mtu huyo..yaani kila siku mnachomba mtu undani wake badala ya uwezo wake na faida inayoweza tokana bali tunagawana umaskini na hasara tupu..
Tunacholalamika sisi wananchi ni kwamba Richmond walikuwa hawana Uwezo, halikuwa shirika la ku supply umeme kama tulivyodanganywa na tukaliondoa nchini.. Hoja hii haihitaji mwakyem,be awe na mradi wa umeme au hana.. Dowans pia ni yale yale ya Richmond kiasi kwamba tunauziwa nyama ya mbuzi ktk gunia..na kwa sababu ya njaa yako unachokiona wewe ni nyama na yeyote anayepinga uhalali wa nyama hii unamwona mchawi..
Nitakueleza kwa mapana zaidi mkuu wangu.. Project ya Mwakyembe kama nivyofahamu mimi ni project ya Mabillioni.. huyo Mwakyembe na washirika wake wote hawawezi kuwekeza ktk mradi huu kwa fedha zao toka mfukoni.. haiwezekani kabisa ikiwa target ni ku produce 1800MW..
Mtaji unaohitajika ni zaidi ya bajeti yetu ya mwaka mmoja kama sio miwili, hivyo huyo Mwakyembe hata kama mradi utasimama ili shirika liweze kuona matunda yake itachukua zaidi ya miaka 40, by the time nani anajua kwamba huyu Mwakyembe atakuwa hai bado..Kifupi ni idea ambayo wanaweza kuiwakilisha bank kuu au Benki ya Kiafrika, nchi wahisani na ikakubali kirahisi sana kutokana na kwamba ni mradi unaokwenda na wakati.. kuondokana na Polutions na mavitu kibao ambayo hayakubaliki kwa leo..
Na tukitazama on the positive side ya project hii ni kwamba wakati wote Watanzania na kizazi kijacho wataondokana na tatizo kubwa la Umeme.. uwezekano wa kuviwezesha viwanda vikubwa nchini utakuwa mkubwa kwani maendeleo yote ya karne hii hutanguliwa na Umeme..Kufikiria hivyo tu binafsi nampongeza Mwakyembe ambaye ni mbunge tu lakini kaweza kufikiria project ambayo itatuwezesha nchi nzima kupiga hatua ya mwanzo muhimu..

Kwa hiyo kinachotakiwa kwetu sisi ni kumpongeza mtu kama Mwakyembe kuweza kusimamisha project ambayo kila bank duniani itaweza kusimama nasi kuuwezesha mradi huu kusimama. haijalishi nani mwenye mali hii kwani kama leo tunagombana hapa kwa sababu ni mali ya Mwarabu na mkaona uhalali wake iweje muone vibaya kwa mwafrika ati kwa sababu yupo katika kamati ya nishati na madini lakini huyo mwarabu aliyeko ktk kamati zinazohusiana na fedha hana hatia ya hisia zetu.. au kwa sababu yeye sio mzalendo kiasi kwamba hizo Conflict zinamgusa mweusi na sio mwarabu ambaye alikuwa mbunge, mweka fedha wa chama CCM, mjumbe wa kamati kubwa za chama na serikali zilizomwezesha kupanga kuingia kwa Richmond na Dowans nchini..Huyu ni msafi au kama mchafu basi uchafu wake anasameheka kwa sababu katuletea mitambo lakini kuna mchafu mweusi mwenye interest ktk uwekezaji ktk umeme..come on now!

Hapana mkuu wangu kama wewe huoni shimo hili sisi wengine twaliona vizuri kwa sababu hata Songos wakinunua mitambo hiyo sisi Tanzania hatuna mkataba na GE hivyo hatuna guarantee ya maintanance yoyote itakayohitajika acha mbali swala la mitambo hiyo kuwekwa collateral..
Na kama hatuna guarantee ya maintanance labda nikukumbushe kwamba hao Songas mwezi September mwaka jana waliharibikiwa turbines 3 na ilichukua zaidi ya miezi miwili kuifanyia repairs pamoja na kwamba ilikuwa ndani ya mkataba na watengenezaji turbines hizo (GE)...leo tukaingie kununua mitambo ambayo kwanza sisi wenyewe hatuna mafundi, pili tukitaka GE wazifanyie ukarabati wakati hatuna mktaba nao itatugharimu kiasi kwamba ni afadhali kukunua mitambo mipya kabisa.. mkuu najua jinsi watu hawa wanavyofanya kazi mkuu wangu kama huna guarantee hao GE watakumaliza...Fikiria gharama za kuwaleta mafundi, kuwapa huduma zote kwa siku zote watakazokuwepo nchini mbali na gharama za matengenezo..

Tuwe smart wakuu zangu hata kidogo tusiwe tumegubikwa na blanketi la tukashindwa kuona mwanga nje zaidi ya kubishana hapa kuhusiana na Mwakeymbe.. This problem is beyond Mwakyembe au Rostam..
 
tk, huo ulikua mfano tu ambapo "Tatizo X" stands for tatizo tu na si lazma lifanane kabisa na hii situation ya ma generators.

Lakini kama itakua rahisi kuiongelea literally,
say Tatizo X is
Utata hauko kwenye usajili wa Richmond na Dowans tu. Utata umejaa kila kona. Kuna utata kuhusu ubora wa mitambo, kuwaka leo haimaanishi kwamba itawaka kwa muda wa kutosha kama mitambo mipya. Unaweza kununua sasa baada ya muda kidogo ikararibika. Wangapi wameuziwa magari yanayotembea yamepakwa rangi vizuri kumbe ni mitumba vimeo? Sasa utata unazuka kwa kuwa kampuni iliyohakiki ubora wa mitambo yenyewe inatiliwa shaka, lakini pia imeletwa na TANESCO yenyewe ambayo inapigia debe Dowans. Utata uko kwenye umiliki wa hiyo kampuni pia, yule Al Adawi amesema yeye ndio mmiliki pekee kama alivyonukuliwa na Tanzania Daima. Lakini taarifa za BRELA zianonesha tofauti hivyo ni mtu mwongo mwongo. Ukiuziwa mali na mtu mwongo ni hatua kuelekea kutapeliwa. Utata uko kwenye bei ya mitambo. Bei inayotajwa ni kubwa kuliko bei ya mitambo mipya. Utata uko kwenye malipo ambayo mpaka sasa tumewalipa na kiasi tunachowadai. Utata uko kwenye tuhuma kwamba kampuni hii inadaiwa. Utata uko sisi na wao ndio maana tumefunguliana kesi. Sasa kama kuna utata wote huu kwanini tujiingize katika biashara tata wakati biashara nyingine zipo nzuri tu?

Ata kama Dowans wakikwepa kumuuzia mitumba ya generator Tanesco kwakumuuzia Songas instead. Hilo tatizo hapo juu (Tatizo X) litakuwepo tu na itabidi libebwe tu na mtu. Kama investors wa Kiwira wamekimbia kwasababu ya politics, nita washangaa sana Songas kujiingiza katika mzigo very risky kama huu wakununua mitambo ya Dowans ambayo politically ni very sensitive nchini. Sidhani kama Songas watataka kujiiniza kwenye situation just for 100Mw and jeopardise investments zao. Kwahio this deal does not make sense, unless hii habari imetumika as spin kuwalegeza wananchi ambao will take this at face value. Watu kufikiri kwamba kama Songas inaweza kununua hii mitambo, basi option ya Tanesco haina capacity charges. Na hapo baadae emergency la giza nene likiingia, itakua rahisi kwa sisi ananchi kukubali hali kwa Tanesco kununua hii mitambo toka kwa Dowans.
 
Last edited:
Dawakali,
Mkuu hizi ni tetesi tu Songas inaongozwa na wazungu na nakuhakikishia hawawezi kununua mitambo ya Dowans kwa sababu ambazo sisi tumezitaja, Haiwezekani! hawaihitaji mitambo hiyo isipokuwa sisi ndio tunalazimisha..ni swala la logic tu kwa mfanya biashara..
Na kama mnafikiria yatakuwa basi tusubiri ukweli unless Tanesco wenyewe wananunua kwa kutumia hadithi ya kwamba Songas wamenunua..
 
songas wananunua ile mitambo na watatuuzia grid megawatt100 za umeme wanarudisha pesa yao ndani ya mwaka mmoja,sisi si tumekalia siasa,na kupinga au kukubali hoja kwa kumuangalia aliyetoa hoja usoni!!!

kitu chochote kizuri kinasemwa na ccm akisema mpinzani mnaleta siasa,hakuna mfanyabiashara atakayekataa fursa ya kutengeneza pesa ya bure haraka haraka ..kwani ni wazi solution ya serikali itachukua zaidi ya mwaka mmoja na yeye atakuwa amesharudisha pesa na anaendelea kuuza umeme kwa kuwa mahitaji yanakuwa,ule mtambo hata ukidumu miaka 5 mbele kabla ya kuhitaji matengenezo makubwa ayakuwa ameshanunua mitambo mipya miwili na wanahisa wake kupata faida kubwa......
 
Back
Top Bottom