Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
Jamani Globeleq ni leading shareholder anamiliki 59% akifuatiwa na TANESCO anamiliki 21% na TPDC wao wanamiliki 12% na TDFL wana 4% na zilizobaki ni hao jamaa wa Holland na hizi ni za kweli kwamba Songas wame bid kutaka kununua hiyo mitambo ya Dowans,habari ndo hiyo
Asante kwa taarifa hizi, sasa cha muhimu ni kuzingatia pia kuwa kama 37% iko katika mikono ya serikai kwa njia moja au nyingine na Tanesco ndo mteja wa Songas basi wana-influence kubwa zaidi.
Anyway, Tanzanians have a stake in Songas through Tanesco, kwa hiyo tunawezakushinikiza na kusema kuwa Songas kama Songas haiwezi kununua mitambo ya Dowans kwa kutumia pesa za Tanesco - dividend yake, capital yake etc. Labda hizo pesa wazitoe Uholanzi. Otherwise there is no change from the original plan and the government is putting money into buying Dowans.
BTW kwa wale wanaotetea ununuzi naomba kuuliza kwa nini Songas hawakununua mitambo ya Aggreko? Na kwa nini serikali haikung'ang'ania kununua mitambo ya Aggreko?
bado nafikiri huenda likawa ni goli la kisigino, ni namna tu ya kuiosha (launder) Dowans kwa kupitia Songas. Baada ya hapo tuitasikia Songas iinataka kuiuzia mitambo Tanesco -- na mjadala kurudi back to square one. Mafisadi wanapodhamiria, na hasa wakiwa na backing ya kutoka top, basi kila mbinu zitatafutwa na kuzitekeleza.
Tatizo mwenye hiyo mitambo anataka fedha na ameiahidi CCM kuwa 2010 ni ngumu kupata hela za chee -- hakuna tena EPA, Deep Gree, Meremeta, Twin Towers au nini.Kilichobakia ni Dowans, DOWANS, DOWANS, DOWANS, maana hela zipo kutoka Hazina za kumpa huyu bwana na kuiokoa CCM1Mradi wa Vitambulisho pia umekwama, kwani tunasikia wafadhili wamemwambia JK huko London aachane nao ama sivyo asionekane tena maeneo ya huko na bakuli lake.
Mkuu Semilong,
Unarahisisha mambo utafikiri hiyo kampuni ya kuuza nyanya?
Hayo makampuni mengine yana shareholders wengine wengi tu, wanafuata corporate governance na accounting principles. Unachokisema kinawezekana tu kwenye mashirika yetu ya umma yanayoendeshwa kisiasa.
Kama Songas watanunua huo mtambo ni kwasababu wameona opportunity ambayo sisi hatukuiona na wameamua kuitumia. Its the economy, stupid!
Hili la TANESCO kuwa na hisa kwenye Songas na hata TPDC na TDFL linanipa shida.
Hivi washinddani wa Songas, nikiwa na maana Agrekko, ITPL, Kiwira, Dowans an PPEL watasemaje kuona kuwa mshindani wao Songas anamilikiwa kwa kiasi fulani na mteja wao Tanesco na wachuuzi kama TPDC?
Hiyo si Konfliti of Interest au bado tunafumbia macho?
No wonder bei za umeme Tanzania ni kubwa na za kutisha!
Iko mbaya gani. Shareholders watatu in red hapo juu ni private investors. Kwa hiyo Songas inaendesha shughuli zake kwa misingi ya kibiashara siyo kama mashirika yetu ya umma yanavyoendeshwa kwa misingi ya kisiasa.
Kufuatana na hali ya umeme nchini, this is a good business opportunity for anyone with brains kununua hiyo mitambo maana itahitajika tu hata Tanesco wanunue mitambo hiyo mipya.
Hapo Tanesco itapoanza kuwalipa capacity charges na Songas kuongeza faida yao, ndio wale wanaopinga ununuzi wa mitambo ya Dowans watapoona makosa waliyoyafanya. Na Bunge litaangalia hivi hivi bila kuwa na lolote la kufanya kwani halima mandate ya kuingilai utendaji wa Songas.
Mkuu TK,
Umenena yote. Hawa Wazalendo wa maneno huku kwenye matendo hakuna wanachofanya
kusaidia kutatua hili suala la umeme na matatizo mengine ya nchi, kwa kweli ni politics.
Tanesco wametangaza tender ya kununua generators, mimi nawashauri wazalendo nyie wa TZ anzisheni kampuni yenu ili muweze ku bid na kushinda tender ya kuwaletea Tanesco generators. Wazalendo nyie si mnajua wapi hiyo mitambo inauzwa bei chee? Badala ya maneno matupu nafikiri huu ndio muda muafaka wa matendo.
17th October 2001
In a $310-million project, the Songo Songo gasfield
kwani serikali ilishindwa kufanya yenyewe ukizingatia faida yake sasa hivi siwangekua wamerudish $310m
Hawataki kuendeleza nchi wanachotaka ni kuiibia tu kwa kutumia kalamu.
Fikiria, hatuku-invest $310million kwenye Songo Songo gas lakini;
Tanzania tungekuwa mbali sana kama Mkapa wa kabla ya Nyerere kufariki angeendelea kuongoza nchi. Bahati mbaya alifanya 180 degree na kumrudisha Lowassa, mengine ni historia.
- Tuliweza $200million kwenye Twin Towers
- Na sasa tunataka kupoteza $150 millioni kwenye ambavyo hata US, RSA n.k, hawana na 80% ya Tanzania haina umeme wa kuvisoma,
- Hapo usiseme pesa za EPA, BOT, IPTL, Richmond n.k.
Jamani naomba kueleweshwa kidogo. Labda nianze kwakutumia example say:Hapo Tanesco itapoanza kuwalipa capacity charges na Songas kuongeza faida yao, ndio wale wanaopinga ununuzi wa mitambo ya Dowans watapoona makosa waliyoyafanya. Na Bunge litaangalia hivi hivi bila kuwa na lolote la kufanya kwani halima mandate ya kuingilai utendaji wa Songas.
Jamani naomba kueleweshwa kidogo. Labda nianze kwakutumia example say:
Kampuni A = dalali wa kuuza magari
Kampuni B = kampuni yaku azimisha magari (car hire firm)
Tatizo X = magari ya wizi kutoka Africa Kusini
Je kama Serekali imejaribu kununua magari kutoka kwa Kampuni A kwa maitaji ya dharula(ka mkutano wakimataifa).
Wanaichi wamepiga mayowe kwamba hayo magari ya Kampuni A yasinunuliwe kwasababu ni MITUMBA.
Sheria za ununuzi zinasema Serekali lazma inunue magari "Brand New" kama wanataka.
Wakati mvutano unaendela, inakuja kugundulika kwamba magari ya Kampuni A yana Tatizo X, kosa ambalo aliruhusiwi kwenye procument process ya nchi(na kuweza kubatilisha mkataba kama ukifanyika).
Kuna uwezekano mkubwa pia kwamba Kampuni A inaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa
hilo(Tatizo X).
Serekali imekodishwa magari kwa mkataba na Kapuni B kwa mda ili kumudu matumizi yakawaida.
Kapuni A imeshindwa kumuuzia Serekali magari yake kwasababu ni MITUMBA na Tatizo X bado lipo lakini limechuniwa.
Kapuni A inasuka mpango na wahusika kumuuzia Kapuni B magari yake.ilikukwepa kipengele cha ununuzi wa "Brand New" Serekalini.
Kapuni B ikinunua hayo magari nakutaka kunigia kwenye mkataba mwingine na Serekali, lakini huu mkataba mpya uwe wa-mda kumudu dharula Serekalini.
Je huo mkataba mpya na Serekali utakua umeliondoa kosa ya kwamba hayo magari bado yana Tatizo X?
Mlalahoi.
Mimi nadhani Watanzania wenye mawazo kama yako bado wamelala usingizi. Naona mnadhani nchi hii bado ni ya kijamaa. Mnazungumza tu habari ya uzalendo kwa kupiga mdomo wakati wenzenu wanafanya kazi zao chini ya mfumo wa sasa wa sera ya nchi kuwa ni private sector ndiyo itakayo endesha uchumi wa nchi hii na serikali itajenga tu mazingira mazuri ya kuiwezesha private sector kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Sasa watu kama ninyi badala ya kutafuta njia ya kujipenyeza ndani ya private sector, bado mnazembea kuchangamka mnadhani ni enzi zile za Nyerere na Ujamaa. Mambo yamebadilia Mzee. Katika ubepari mwenye kisu kikali ndio hula nyama.
Ninyi mmekaa tu na kupiga kelele Dowans! Dowans! Ufisadi ! Ufisadi!, wakati wenzenu wanafanya mambo yao and within the law kama hao Songas. Hebu soma hiyo article ya Babu Ataka Kusema huenda ikakuzibua maskio.
Najua Watanzania kama mmoja mmoja hawana uwezo, lakini badala ya kupoteza muda wetu kutoa theories za ndoto kwa nini msifanye jambo la maendeleo kwa mfano kuiga mfano wa NICO? Jiungeni katika vikundi vya kiuchumi na muanze kushiriki katika uchumi wenu. Huo mdomo mdomo wenu utawaacha muwe kila siku maboi wa wawekezaji. (Nasaha tu ndugu yangu usikasirike)
Mkuu TK,
Umenena yote. Hawa Wazalendo wa maneno huku kwenye matendo hakuna wanachofanya
kusaidia kutatua hili suala la umeme na matatizo mengine ya nchi, kwa kweli ni politics.
Tanesco wametangaza tender ya kununua generators, mimi nawashauri wazalendo nyie wa TZ anzisheni kampuni yenu ili muweze ku bid na kushinda tender ya kuwaletea Tanesco generators. Wazalendo nyie si mnajua wapi hiyo mitambo inauzwa bei chee? Badala ya maneno matupu nafikiri huu ndio muda muafaka wa matendo.
Uchumi na siasa haviendi pamoja. Ukijaza siasa kwenye uchumi, unaishia kama Mugabe. Mwalimu alijaribu alipoona yanamshinda, alikuwa na akili, akakubali ukweli na kumwachia Mwinyi afanye mabadiliko.
Its no brainer kujua kwamba demand ya umeme kwa TZ ni kubwa na hata uwe na mtambo wa zamani bado utapata faida na kurudisha pesa zako haraka. Songas wameangalia huo ukweli na kwasababu ni mabepari watahakikisha wanapata hiyo mitambo kwa bei nzuri, watatengeneza umeme na kutuuzia sisi Wadanganyika kwa bei ya juu na faida yake kubwa kuitoa nje ya nchi. Sisi tutaendelea kuimba wimbo wetu wa uzalendo wa maneno huku wananchi wetu wengi hawana kazi, viwanda havizalishi ipasavyo shauri ya matatizo ya umeme, ajira kwa vijana mbovu, pato la taifa linashuka.
Amkeni ndugu zangu, tangulizeni mbele uchumi kuliko siasa.
Hivi ule mwongozo wa Tanu ulikuwa unasemaje? "Kitendo chochote kinachomwongezea mtu uwezo/uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe, ni kitendo cha maendeleo hata kama hakiongozi tija wala pato" Kwi kwi kwi!!!
Second to UFISADI,ni NJAA za vibaraka wa mafisadi.
Utata hauko kwenye usajili wa Richmond na Dowans tu. Utata umejaa kila kona. Kuna utata kuhusu ubora wa mitambo, kuwaka leo haimaanishi kwamba itawaka kwa muda wa kutosha kama mitambo mipya. Unaweza kununua sasa baada ya muda kidogo ikararibika. Wangapi wameuziwa magari yanayotembea yamepakwa rangi vizuri kumbe ni mitumba vimeo? Sasa utata unazuka kwa kuwa kampuni iliyohakiki ubora wa mitambo yenyewe inatiliwa shaka, lakini pia imeletwa na TANESCO yenyewe ambayo inapigia debe Dowans. Utata uko kwenye umiliki wa hiyo kampuni pia, yule Al Adawi amesema yeye ndio mmiliki pekee kama alivyonukuliwa na Tanzania Daima. Lakini taarifa za BRELA zianonesha tofauti hivyo ni mtu mwongo mwongo. Ukiuziwa mali na mtu mwongo ni hatua kuelekea kutapeliwa. Utata uko kwenye bei ya mitambo. Bei inayotajwa ni kubwa kuliko bei ya mitambo mipya. Utata uko kwenye malipo ambayo mpaka sasa tumewalipa na kiasi tunachowadai. Utata uko kwenye tuhuma kwamba kampuni hii inadaiwa. Utata uko sisi na wao ndio maana tumefunguliana kesi. Sasa kama kuna utata wote huu kwanini tujiingize katika biashara tata wakati biashara nyingine zipo nzuri tu?