Songea Kunufaika na Mradi wa Maji wa Bilioni 145

Songea Kunufaika na Mradi wa Maji wa Bilioni 145

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

NW MAJI ENG. MARYPRISCA MAHUNDI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA - SONGEA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA 145 BILLIONI

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi (Mb) tarehe 10 Machi, 2023 akiwa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ameshuhudia utiaji saini mkataba mradi mkubwa wa Maji wenye thamani ya shilingi 145 Billioni utakaotekelezwa kwa miezi Thelathini na Mbili na kampuni ya Kichina.

Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi alimwakilisha Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, Na amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa katika miji 28 nchini ukiwemo Songea utakaopandisha upatikanaji wa Maji kutoka asilimia 83 hadi asilimia 95.

Katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha nyingi katika Wizara ya Maji akiwa na dhamira thabiti ya kumtua mama ndoo kichwani.

Katika hatua nyingine Wizara imenunua mitambo mitano ya utafiti wa maji na magari Ishirini na Tano kwa ajili ya kuchimba visima. Wizara pia imejielekeza kuchimba mabwawa kwa ajili ya kuvuna maji yanayotokana na mvua ili maji hayo yakivunwa yasaidie kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji.

Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi amempongeza Mbunge wa Songea Mhe. Dkt. Damas Ndumbalo kwa ufuatiliaji ili kuona wananchi wake wanapata maji safi na salama. Aidha amewataka vijana kujitokeza kufanya kazi katika mradi huo ili kujiongezea kipato.

#KaziIendelee
#MajiNiUhai
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.05(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.05(2).jpeg
    38.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.06(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.06(1).jpeg
    55 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.06.jpeg
    63.8 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.07(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-11 at 07.22.07(1).jpeg
    59 KB · Views: 4
Back
Top Bottom