Songea mbona haibadiliki? Kuna tatizo gani na mmekuwa na Mawaziri toka miaka ya 1960?

Hivi ni kweli kuna Mtanzania aliesoma Shule hata ya msingi tu, tena ndani ulimwengu wa Smart Phone hajui kuandi kwa usahihi jina la kila mkoa Tanzania. ingekua kutamka sishangai maana kuna makabila kutamka baadhi ya herufi ni ngumu kutokana kiluga chao. Eti N'twara ha ha.
 
Naomba unisadie kunijibu Hilo swali uliloniuliza🀣🀣🀣
 
Mkuu wewe ndio Umekosea sasa
Watu wa Mtwara hakuna M huko bali kuna N

Mtu wanasema ntu

Mwanamke wanasema Mwananke

Jamaa ni mzoefu anawafahamu
 
Naomba unisadie kunijibu Hilo swali uliloniuliza[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
GDP=Gross Domestic Products

GDP ni Jumla ya bidhaa au huduma zilizozalishwa kwa kipindi husika mara nyingi hupimwa kwa mwaka mmoja

Songea wanalima Mahindi na sio Songea tuseme Mkoa wa Ruvuma

Yawezekana wanalima sana lakini yanasafirishwa nje ya mkoa au nchi huku wakulima wakilipwa makombo na mkoa ukibakiwa na leftovers tu

GDP inakuwa assigned in Monetary terms yaani Value

Ndio maana kuna malalamiko mengi kuhusu Pato la mtu mmoja mmoja yaani per Capita income

Per capita income=GDP gawa kwa idadi ya watu P, Population

Sasa Yawezekana Kilimo cha mahindi Songea wamehodhi wafanyabiashara wachache wakubwa na hii inaathiri mahesabu ya GDP pamoja na Per capital income

Angalia idadi ya watu Songea mjini Halafu Angalia uzalishaji wao, Yawezekana idadi ya watu ni ndogo sana hivyo inafanya GDP ionekane kubwa sana

Mfano Mbinga ina Kahawa hata GDP yao Itakuwa kubwa kutokana na uuzaji wa Kahawa lakini Kiuhalisia maisha ya Mbinga kwa Raia ni hovyo hata wilaya yenyewe,

Je Katika bidhaa au huduma zinazozalishwa kiasi gani kinapatikani kujenga Songea, Yawezekana GDP ni kubwa kutokana na Kahawa Mbinga, Korosho Tunduru na Mahindi Namtumbo

Songea wao wanabakiwa na kitu gani au uwezo wa GDP ya Mbinga ndio inaathiri Songea ionekane hali nzuri

Mkuu vipimo vya GDP hivi ni economic theory na zina limitation nyingi na zina boreshwa kila siku, Sio halisia sana

Songea hakuna viwanda vya maana vinavyoajiri watu wengi na Kutengeneza uzalishaji, Uzalishaji mkubwa unao boost GDP yao ni Mahindi na Kahawa ya Mbinga, Lakini Mashamba makubwa Mbinga au ya Mahindi unakuta yanamilikiwa na watu wachache Wengine wanalima kidogo sana kwa chakula na kuuza hivyo inaathiri Maendeleo ya Songea

Soma tafiti zinasemaje, We don't have data's ndio maana nimeuliza mbona mkoa haupigi hatua upo pale pale miaka yote lakini hapa nimeuliza mji wa Songea sio mko wa Ruvuma

Uangalie vizuri ule mji wa Songea tu achana na mkoa wa Ruvuma , Songea kama mji kuna shida,Mjk hauna infrastructure za maana
 
Shida hamna muingiliano wa watu yan wapo wangoni na makabila mengine ya huko ila serikali ingejenga vyuo hata vitatu pangekuwa na watu mbali mbali na mzunguko ungekuwa mkubwa na maendeleo ila itabaki hiv hivo mpka nyerere arudi viongozi wanawaza matumbo kama ilivo wilaya ya Namtumbo hovyo kabsa
 
Sasa kama ww utaki kulata maendeleo unaisi nani ataleta aza ww jenga hotel moja zuri na vitu vingine nawengine watafanya ivyo
 
HAPO KWENYE GDP SIO KWELI ETI INAIZIDI KILIMANJARO?!!!
GDP INAITAJA KILIMANJARO KWENYE NAFASI TATU ZA JUU.
FUATILIA VIZURI UHAKIKISHE.
 
Jenga wewe hayo maghorofa na sisi tuyaone
 
Yaani unajiongelesha wakati unafahamu walau kuna mabadiliko ya msingi kama hizo barabara zote za kuingia na kutoka mkoani zote ni lami,zamani hazikuwepo..

Barabara za mjini hapo nk.

Mambo ya majengo marefu huwa hayajengwi kama Pambo Mzee ni biashara..

Pamoja na kupondea huko kwenu mimi bado naona Songea itakuwa na fursa kubwa Sana tuu mara baada ya barabara za kuingia Msumbiji kuwa lami na pia barabara ya kutokea Morogoro ikikamilika..

Mwisho airport mpya imejengwa, hospital mpya ya Mkoa imejengwa nk nk.
 
Mtoa mada anataka eti akute kuna maviwanja ya kula Bata kama Dar,Arusha,Dom,Mwanza,Mbeya hivyo yaani kwamba ndio kigezo cha maendeleo πŸ˜†πŸ˜†..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…