Alexander Lukashenko
JF-Expert Member
- Sep 9, 2017
- 4,140
- 9,667
Bana wewe Hesabia Sensa tuachie Songea Yetu, majungu hatutaki.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ongezea bombambili,seedfarm,Matarawe nkMfaranyaki, mateka, lizaboni etc long time sijafika songea
yule mama huwa ni bure kabisa ndo maana wanampendaMawaziri wa type ya Jenista Mhagama? wanajua kujaza matumbo yao na kusifia ili kulinda nafasi zao.
Hujasoma ukaelewa nilichoandika, hakuna M. kwenye kutamka siyo kuandika.Mkuu wewe ndio Umekosea sasa
Watu wa Mtwara hakuna M huko bali kuna N
Mtu wanasema ntu
Mwanamke wanasema Mwananke
Jamaa ni mzoefu anawafahamu
Lakini bado panazidi huko kusini[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Kagera kuna ujumbe wenu huku [emoji116]
Kwa hiyo Kusini kuna shika mkia kama Kagera? 😆😆Lakini bado panazidi huko kusini
Kagera na ruvuma Bora ruvuma mkuu. Kagera Ni masikini miaka yote pamoja na kuwa na wasomi wengi lakini washamba Sana wameshindwa kuendelea kwao.Lakin mbona NBS inautaja kuwa top five ya mikoa tajiri nchini kwa GDP kuzidi mikoa maarufu kama Kilimanjaro, kagera nk
NBS inataja mkoa wa Ruvuma kama mkoa wa nane nchini kwa maisha bora[emoji23] sasa sijui wanatumia vigezo vip
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Hili sio jukwaa la kiswahili na FasihiHujasoma ukaelewa nilichoandika, hakuna M. kwenye kutamka siyo kuandika.
Aisee huenda. Lindi imezindikwa ila Masasi sijasikiaKusini mwa Tz Kuna laana kule kulishazindikwa ndio maana nchi haikui hii.
Acha masihara mkuu ruvuma inatisha aiseKagera na ruvuma Bora ruvuma mkuu. Kagera Ni masikini miaka yote pamoja na kuwa na wasomi wengi lakini washamba Sana wameshindwa kuendelea kwao.
Kwa kuwa komba,Punda na nyani wanakimbikia mjini hiyo utalii hakuna🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤸🤸Nimefika mkoa wa Ruvuma hapa mjini Songea baada ya miaka 18 tangu mwaka 2004, sioni mambo mapya kabisa wala ukuaji wa mji.
Hapa mjini naona majengo ni yale yale tu zaidi majengo kidogo sana yameongezeka kama pale opposite na Bank ya NMB zamani tulisema ni eneo la TANESCO. Kitu gani kinazuia majengo marefu hapa Songea mjini?
Huu mji kwa maendeleo ya vitu naona ni negative growth hasa infrastructure, zaidi ya miaka 18 niliyoondoka huku no changes!
Boda boda zipo nyingi sana hapa mjini tofauti na wakati huo nilipoondoka, sijajua watu wanatembea kwa umakini kiasi gani maana boda boda na watu ni kama idadi sawa au ngoma droo hapa mjini.
Soko la majengo kule zamani tuliita mitumbani hakuna mabadiliko makubwa sana zaidi ya bara bara za hapa na pale lakini wakati huo kulikuwa na lami yenye mashimo mashimo.
Mjini hakuna barabara za maana zaidi ya barabara itokayo bombambili mpaka Mbinga huko. Mji haujapanuka kabisa, Unatembea nusu saa tu umemaliza, hakuna sehemu za kuvutia na sehemu za mitoko zaidi ya bar.
Songea ukisema leo natoka ni kwenda bar, hakuna amsha amsha niliyoiona hapa Songea mjini.
Wazoefu wa miji, huu mji una tatizo gani?
Nilipita Njombe imebadilika sana sana tofauti na Njombe ile ya miaka 18 iliyopita. Hii ni Songea mjini lakini ni kama upo kwenye wilaya za ndani ndani huko za baadhi ya mikoa.
Soko la hapa Songea Mjini hata silielewi vizuri ni kasoko kadogo sana na kamejibana sana, kwanini wasiliamishe soko hilo?!
Kulikuwa na kampeni za kujenga masoko na stand wakati wa JPM, sijajua kwanini waliamua kuacha soko la mtindo huu.
Kuna stand mpya lakini haivutii kabisa kabisa zaidi ya kuweka lami, hakuna jengo kubwa la maana la abiria kwenye stand mpya.
Wamejenga stand mpya mbele ya msamala ukitokea mjini lakini bado wamefeli vibaya sana ni kama kituo cha daladala hivi.
Bar zipo zipo sana labda ndio sehemu ya starehe lakini hazina quality inayotakiwa kwa watu wala bata na matanuzi.
Mikoa hii ya kusini kuna tatizo kama hata stand mikoa walipata nao pesa za mgao wamejenga stand nzuri na za kisasa sana.
Kwa hiyo Songea hata ukapeleka mabilioni ya pesa za Serikali bado huu mji unalala usingizi tu, Kwa miaka 18 niliyotoka nimesikitika sana.
Jumatatu naelekea Lindi, nipo mapumzikoni hivyo natembea tembea kwenye hii mikoa nilianzia safari Dodoma.
Pua ndefu tuu 🤔Kifupi kama umetokea dar huko kwingine kote ni vijijini mwaka Jana nilienda Mbeya Dec nikiamni nitaenjoy aisee nilichoka anyway kitu pekee nilifurahia ni upishi mzuri sana wa kitimoto nje ya hapo hakuna kitu
Nimekupata bila shakaGDP=Gross Domestic Products
GDP ni Jumla ya bidhaa au huduma zilizozalishwa kwa kipindi husika mara nyingi hupimwa kwa mwaka mmoja
Songea wanalima Mahindi na sio Songea tuseme Mkoa wa Ruvuma
Yawezekana wanalima sana lakini yanasafirishwa nje ya mkoa au nchi huku wakulima wakilipwa makombo na mkoa ukibakiwa na leftovers tu
GDP inakuwa assigned in Monetary terms yaani Value
Ndio maana kuna malalamiko mengi kuhusu Pato la mtu mmoja mmoja yaani per Capita income
Per capita income=GDP gawa kwa idadi ya watu P, Population
Sasa Yawezekana Kilimo cha mahindi Songea wamehodhi wafanyabiashara wachache wakubwa na hii inaathiri mahesabu ya GDP pamoja na Per capital income
Angalia idadi ya watu Songea mjini Halafu Angalia uzalishaji wao, Yawezekana idadi ya watu ni ndogo sana hivyo inafanya GDP ionekane kubwa sana
Mfano Mbinga ina Kahawa hata GDP yao Itakuwa kubwa kutokana na uuzaji wa Kahawa lakini Kiuhalisia maisha ya Mbinga kwa Raia ni hovyo hata wilaya yenyewe,
Je Katika bidhaa au huduma zinazozalishwa kiasi gani kinapatikani kujenga Songea, Yawezekana GDP ni kubwa kutokana na Kahawa Mbinga, Korosho Tunduru na Mahindi Namtumbo
Songea wao wanabakiwa na kitu gani au uwezo wa GDP ya Mbinga ndio inaathiri Songea ionekane hali nzuri
Mkuu vipimo vya GDP hivi ni economic theory na zina limitation nyingi na zina boreshwa kila siku, Sio halisia sana
Songea hakuna viwanda vya maana vinavyoajiri watu wengi na Kutengeneza uzalishaji, Uzalishaji mkubwa unao boost GDP yao ni Mahindi na Kahawa ya Mbinga, Lakini Mashamba makubwa Mbinga au ya Mahindi unakuta yanamilikiwa na watu wachache Wengine wanalima kidogo sana kwa chakula na kuuza hivyo inaathiri Maendeleo ya Songea
Soma tafiti zinasemaje, We don't have data's ndio maana nimeuliza mbona mkoa haupigi hatua upo pale pale miaka yote lakini hapa nimeuliza mji wa Songea sio mko wa Ruvuma
Uangalie vizuri ule mji wa Songea tu achana na mkoa wa Ruvuma , Songea kama mji kuna shida,Mjk hauna infrastructure za maana
Brother umetukosea Sana ila hakuna shida ucjariKwa kuwa komba,Punda na nyani wanakimbikia mjini hiyo utalii hakuna🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤸🤸
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza.Hili sio jukwaa la kiswahili na Fasihi
Nenda kwenye jukwaa la lugha utakutana na rafiki zako mkajadili Nomino, vitenzi, viwakilishi, irabu na mambo mengine mengi ya vitendawili tega
Hujafika mtwara, Wanachotamka ndio wanachoandika watoto wa shule