Songea to Mwanza: Mwamba katoa chuma na kaanzisha hii route

Songea to Mwanza: Mwamba katoa chuma na kaanzisha hii route

Hakika ubora wa miundombinu ya barabara ikiwa mizuri hakuna kinachoshindikana.

Muda huu ni saa 22:30 basi la kampuni ya Super Feo limeondoka Singida kuelekea Jiji la miamba Mwanza.

Wale wadau wa usafirishaji mnaionaje na imekaaje hii..?

đź§­ Yule anayetaka kujua umbali kwa mfumo wa picha nadhani hii ramani itakusaidia.


Zoom and fetch area you want.
View attachment 2003845
Kazi nzuri hongera kwake
 
Dar Songea ukipitia njia ya huku kusini Lindi /mtwara sio mbali sana na hakuna msongamano wa magari kama ukipitia hii ya kati, moro,iringa, njombe.
Tulipita ya moro iringa,songea saa 2
 
Ukipita lindi kwenda songea ni mbali zaidi kwani zinaongezeka kilometer kalibia 100 tofauti na njia ya iringa. Sema njia ya lindi ni tambalale milima unakuja kuikuta mchomoro huko wilaya ya namtumbo
Ni kweli,nilipitaga hiyo lindi, songea tulifika saa 6,mbinga saa 8 Super feo

Halafu wakipita hiyo ya lindi wanasimamasimama kama daladala
 
Hiyo ya mwanza to songea ni nzuri sana ila wajitahidi gari ziwepo kila siku,sio kama ilivyo kwa sasa mara 3 kwa week itasaidia sana,maana kuna siku unakuta hakuna gari kabisa una ishia kupanda isamilo,sabuni,fikoshi za mbeya unashuka makambako saa 7 au saa 8 usiku ina chosha sana.
 
Duh, Mdau siku nyingine ukienda mbamba bay nistue inbox uniletee wale samaki wanaofanana na kambale ila wao watamu balaa,,,wanaitwa mbufu, nitashukuru nimekuwa mbamba bay kitambo miaka hiyo nasikia siku hizi hadi kuna taa za barabarani, maisha yanaenda kasi sana
Karibu mbamba bay,
FB_IMG_16315368642922619.jpg
 
Ni sahihi, hata maofisa usalama barabarani si wengi kama ile ya iringa
Bado hiyo kilwa road haina ajali nyingi pamoja na askari kutokuwepo wengi,hapa kuna funzo kwamba askari anapolichelewesha basi kama adhabu ajue huo muda lazima ufidiwe.
 
Songea- mwanza masaa mangapi! Unafika unalazwa siku mbili eti,hii route Ni non stop au Kuna kulala sehemu ,waliosafiri route hii nijuzeni,afya mgogoro anahimili kweli?
 
Back
Top Bottom