Songea to Mwanza: Mwamba katoa chuma na kaanzisha hii route

Kazi nzuri hongera kwake
 
Dar Songea ukipitia njia ya huku kusini Lindi /mtwara sio mbali sana na hakuna msongamano wa magari kama ukipitia hii ya kati, moro,iringa, njombe.
Tulipita ya moro iringa,songea saa 2
 
Ukipita lindi kwenda songea ni mbali zaidi kwani zinaongezeka kilometer kalibia 100 tofauti na njia ya iringa. Sema njia ya lindi ni tambalale milima unakuja kuikuta mchomoro huko wilaya ya namtumbo
Ni kweli,nilipitaga hiyo lindi, songea tulifika saa 6,mbinga saa 8 Super feo

Halafu wakipita hiyo ya lindi wanasimamasimama kama daladala
 
Hiyo ya mwanza to songea ni nzuri sana ila wajitahidi gari ziwepo kila siku,sio kama ilivyo kwa sasa mara 3 kwa week itasaidia sana,maana kuna siku unakuta hakuna gari kabisa una ishia kupanda isamilo,sabuni,fikoshi za mbeya unashuka makambako saa 7 au saa 8 usiku ina chosha sana.
 
Karibu mbamba bay,
 
Ni sahihi, hata maofisa usalama barabarani si wengi kama ile ya iringa
Bado hiyo kilwa road haina ajali nyingi pamoja na askari kutokuwepo wengi,hapa kuna funzo kwamba askari anapolichelewesha basi kama adhabu ajue huo muda lazima ufidiwe.
 
Songea- mwanza masaa mangapi! Unafika unalazwa siku mbili eti,hii route Ni non stop au Kuna kulala sehemu ,waliosafiri route hii nijuzeni,afya mgogoro anahimili kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…