Songwe: Ahukumiwa jela miaka mitatu kwa kumtukana Rais Magufuli

Songwe: Ahukumiwa jela miaka mitatu kwa kumtukana Rais Magufuli

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Fadhili Silwimba, mkazi wa kijiji cha Nzoka Wilayani Momba Mkoani Songwe, amehukumiwa kulipa faini ya shillingi Millioni 5 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukutwa na hatia ya kumtusi Rais Wa Jamhuri ya Tanzania Dkt John Magufuli katika mtandao wa Facebook.

Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, Kassim Mkwawa amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 23(I)na (II) cha mwenendo wa makosa ya kimtandao namba 4 ya mwaka 2015.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali Flavian Leonard Chacha, alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo, mnamo Septemba 7, 2019, kwa kutuma ujumbe wa kumtusi Rais kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

1596547863773.png
 
Mwache aijue nchi hii. Sote siye ni wastaarabu hatutaki kutukanana acha zaidi sana, ati kumtukana mkuu wa nchi. Halafu ni katoto tu. Kwani huyo aliyemtukana waliibiana wapi mademu? Sio jika lake kabisaaaa. Huu ni utomvu wa adabuuu
 
Tungejikita kwanza kuwatafuta na kuwa adhibu waliotaka kumuuwa Lissu kwa kutumia silaha za kivita kwenye makazi ya viongozi area D. MAANA HAO WANA SILAHA HATAREE ZAIDI YA MATUSI.
 
hata yeye anatukana na kudhalilisha watu hasa wanawake kila anapopanda jukwaani
 
Utashangaa watu watamtetea, mtu yeyote anayetukana watu Hana adabu na anawaaibisha wazazi wake kwao malezi mabaya, haitakiwi kumtukana mtu yeyote awe wa chadema awe CCM awe mkubwa awe mdogo, hua nashangaa humu watu wanavyotukana najiuliza Hawa wamelelewaje
Kwanini asitetewe?
 
Back
Top Bottom