Pre GE2025 Songwe: Katibu wa CCM avamiwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa miguu yote miwili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu!

Hekaheka zinazidi kuendelea katika kipindi hichi cha uchaguzi. Naona watu wasiojulikana wamehamia CCM mbona kazi ipo
===================

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itumba wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe, Huruma Ally amevamiwa na watu wasiojulikana na kumvunja miguu yote miwili.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili, Novemba 10, 2024 mjini Ileje, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wilayani hapa, Maoni Mbuba amesema uvamizi huo umetokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi, Novemba 9,2024, huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Mbuba amesema katibu huyo amevamiwa saa nne usiku, eneo la Shule ya Msingi Itumba na aliokotwa na wasamaria wema akiwa katika hali mbaya, baada ya kuvunjwa miguu na kupoteza fahamu.

Soma Pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Songwe

Amesema alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu, huku akisema kitendo hicho hakikubaliki na kimezua taharuki hususani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Mbuba amesema CCM Wilaya ya Ileje inalaani kitendo hicho, huku akiwataka wanasiasa na watu wa kada zote kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Visasi vya Kura za maoni
 
Hii ndo roho halisi ya waTZ,so sishangai wanavyofanyaga CCM maana wenzao wapinzani wanaweza fanya zaidi mradi waTZ ni wale wale.
Lowasa May 2015 na Lowasa October 2015 unatakiwa U-Compare na U-Contrast.
Maneno haya yanafikirisha sana kwa wenye Akili za kufikiria !
Mimi huwa najiuliza maswali mengi ninapowaona Watanzania wanavyompa kipondo kibaka labda amekwapua simu au viatu 😳
Huwa najiuliza hawa watu ndio hao wanaoitwa eti Watanzania ni wapole sana ???!!!
😳🙄😱
 
Safi sana.
Mvua huanza kama manyunyu?

Hakuna anayeweza kudokeza mwenendo wa kisiasa eneo hilo upoje, na hasa hasa huyo majeruhi anavyochukulia mwenendo huo uliovyo? Hii inaweza kujazia nyama kidogo kwenye mfupa ulio wekwa hapa jukwaani.
 
Wakuu!

Hekaheka zinazidi kuendelea katika kipindi hichi cha uchaguzi. Naona watu wasiojulikana wamehamia CCM mbona kazi ipo
===================

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itumba wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe, Huruma Ally amevamiwa na watu wasiojulikana na kumvunja miguu yote miwili.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili, Novemba 10, 2024 mjini Ileje, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wilayani hapa, Maoni Mbuba amesema uvamizi huo umetokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi, Novemba 9,2024, huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Mbuba amesema katibu huyo amevamiwa saa nne usiku, eneo la Shule ya Msingi Itumba na aliokotwa na wasamaria wema akiwa katika hali mbaya, baada ya kuvunjwa miguu na kupoteza fahamu.

Soma Pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Songwe

Amesema alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu, huku akisema kitendo hicho hakikubaliki na kimezua taharuki hususani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Mbuba amesema CCM Wilaya ya Ileje inalaani kitendo hicho, huku akiwataka wanasiasa na watu wa kada zote kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Wenyewe kwa wenyewe hapo
 
Tena

Hao makatibu kata hawana mishahara so hapo hadi apone kazi anayo.
 
Huu mzaha wa kukata majina ya wagombea wasifikiri Kuna mtu wanamfurahisha. Kidogokidogo inaweza ikatuingizia giza tanzania
 
Back
Top Bottom