Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
WINGU jeusi limetanda wilayani Mbozi katika Mkoa wa Songwe baada ya miili ya watu watano wasiofahamika kukutwa imetupwa kwenye msitu wa Mlima Senjele pembezoni mwa Barabara Kuu ya Tanzania na Zambia (TANZAM).
Miili hiyo ambayo ni ya wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30, inadaiwa kutupwa katika eneo hilo usiku wa kuamkia jana na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi (ACP) Theopista Mallya, alisema miili hiyo ilikutwa jana asubuhi na kuchukuliwa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi.
Alisema chanzo cha vifo vya watu hao hakijulikani na kwa sasa wanasubiri taarifa ya kitabibu kutoka kwa madaktari ili wajue kiini chake.
Chanzo: Gazeti la Nipashe