Songwe: Mkusanya mapato ashtakiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Tsh. Milioni 13

Songwe: Mkusanya mapato ashtakiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Tsh. Milioni 13

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Lington Mbuzi, anakabiliwa na tuhuma za Ufujaji na Ubadhirifu wa Tsh. 13,913,488/= mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe zilizofika kwenye himaya yake akiwa Mtumishi wa Umma.

Imeelezwa kuwa, kati ya Mei 5 2017 na Oktoba 10, 2019, Mtuhumiwa akiwa Mkusanya Mapato katika Halmashauri hiyo, alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kupeleka fedha hizo kwa Mhasibu wa Wilaya au kuweka kwenye akaunti ya Wilaya kwa nia ya kujipatia maslahi binafsi.

Mshtakiwa amekana Mashtaka yake na yupo nje kwa dhamana.

Chanzo: TAKUKURU
 
Milioni kumi na tatu ndio mnamtangaza, watu wanapiga mabilioni wanajiamini hawatangazwi na hakuna wa kuwawajibisha.

Hii dunia bwana ni kuonea wadogo tu ila wakubwa wanakaushiwa.
 
Wanaopiga mabilioni hawasemwi🤣🤣🤣.13M hata fuso used hanunui🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom